Tetesi: Vodacom Tanzania wasitisha utoaji wa Line mpya za Uwakala za M-Pesa

Itakuwa wanafanya maboresho au idadi ya wateja wa mobile money wamepungua sana.
 
Hili suala lilikuwepo tangu mwezi wa sita, kabla hata ya kutangazwa kwa TOZO. Binafsi wakati nasajili line ya uwakala, wakala mkuu wa lile eneo alinidokezea jambo hilo.

Ya kwamba ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni, wangesitisha zoezi la kusajili mawakala wapya.
 
Labda hakusema shida nini mkuu?
 
Labda hakusema shida nini mkuu?
Inawezekana labda wanataka kubadili mfumo wa maombi ya uwakala. Ila binafsi naamini hii ishu haina mahusiano na kupanda kwa tozo!

Ingawa ni ukweli usio na shaka, biashara ya miamala imeyumba katika baadhi ya maeneo, tangu zilipo ongezwa tozo. Kama sisi mawakala wapya, ndiyo tunaisoma namba kweli kweli!
 
Back
Top Bottom