Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Kitu kinacho nishangaza kwenye mtandao wa vodacom ni kwamba mteja anayetumia sana huduma zenu ndo anapandishiwa gharama kwenye vifurushi vyake tofauti na mtu anaetumia line yenu mara moja moja, yani mke wangu ni mteja wa mtandao mwingine anatumia voda kwa mwezi mara 3 au 8 package zake very cheap compared na mimi niliye na line yenu kwa muda wote.

Huwa siwaelewi formula yenu, nilitegemea mteja wa muda mrefu mtampunguzia mzigo. Mke wangu mwenyewe nashangaa voda anasema hawa wafanyakazi wa voda wanafikiria kwa makalio nini.
 
Habari Vodacom Tz;
Mimi Ni Mtumiaji Mzuri Sana Wa Huduma Zenu Hasa M-Pesa,Naomba Kujuzwa/Kufahamishwa/Kuelekezwa Namna Tunavyoweza Kujiunga Kama Kikundi Kwenye Huduma Ya Kuweka Fedha Kila Mwezi Then Kila Mwisho Wa Mwaka Au Pakitokea Tatizo Tunatoa Kiasi Fulani,Ila Kama Kundi Na Kila Anaechangia Kila Mshirika/Mwanakikundi Anaona,Maelekezo Tafadhali.
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

  • Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
  • Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
  • Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
  • Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
  • Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Hii namba ni ya tapeli anayejifanya anapiga kutoka Vodacom. Sikilizeni simu alizopiga mtamsikia.

Good enough huyu tapeli sauti yake ni very common lakini hafanywi chochote.

Sasa kupitia ukurusa huu natoa taarifa kwenu mchukulieni hatua haraka na muache kulea hawa matapeli maana uwezo wa kuwakamata mnao.

Namba ni hii +255679999321 @vodacomtanzania

Hiyo namba msiifungie tu, MKAMATENI!
 
Kitu kinacho nishangaza kwenye mtandao wa vodacom ni kwamba mteja anayetumia sana huduma zenu ndo anapandishiwa gharama kwenye vifurushi vyake tofauti na mtu anaetumia line yenu mara moja moja, yani mke wangu ni mteja wa mtandao mwingine anatumia voda kwa mwezi mara 3 au 8 package zake very cheap compared na mimi niliye na line yenu kwa muda wote. Huwa siwaelewi formula yenu, nilitegemea mteja wa muda mrefu mtampunguzia mzigo. Mke wangu mwenyewe nashangaa voda anasema hawa wafanyakazi wa voda wanafikiria kwa makalio nini.
Sijui wananini hawa jamaa aiseee
 
Vodacom mnazingua upande wa lipa kwa m.pesa ukinunua luku inagoma kulikoni.
Hamuoni kama mnapishana na hela?alafu mnachanganya wateja menu ni kiswahili ukifikia karibu na kulipa sasa inakuletea kizungu hivi hamuoni mnawachanganya wateja?sio wote lugha inapanda badilikeni mtakosa wateja kwa kosa kidogo tuu
 
voda com NI majambazi ya mwendo Kasi.
Mlinipiga 2,500 yangu.
Na Mimi nikawapiga kwenye nipige tafu.
Na laini nikavunja
 
Mbona internet ipo slow kama konokono, yaani nusu ya kifurushi chenu ninacho nunua kwa bei ghali kinaenda bure kabisa
 
Mambo ya kunitumia sms zenu za kipuuzi SITAKI, na kuna mara mbili mmenikata pesa eti nimejiunga kwenye kujibu sms zenu manina zenu.
Kuna siku nitakuja na RPG hapo mlimani
 
Voda nirudishieni hela yangu matapeli nyie yaani mnanikata wakati sijakopa ila nitawakomoa tu
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

  • Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
  • Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
  • Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
  • Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
  • Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania

Vodacom mna tatizo la internet? Wiki yote hii internet yenu imekuwa slow kupita kiasi na nimenunua kifurushi cha supa speed, kuweni wakweli
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

  • Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
  • Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
  • Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
  • Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
  • Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Kero zaidi niionayo kutoka kwenu ni muda unaopotea kusubiri laini ya M-PESA
 
Yaani hamnipati tena huu mtindo wenu wa vifurushi mtu ananunua kifurushi mfano cha 2500 cha wiki mnapa dk 200 kati ya hizo dk120 za kupiga masaa yote,dk 80 eti nipige kuanzia saa sita usiku mpaka saa kumi na dk 59 alfajiri, yaani niache kulala nianze kupiga simu na nitampigia Nani usiku huo.

Huo ni wizi hamnipati ng'o
 
Wekeni kifutushi cha mchanganyiko ambacho kinakuwa na data nyingi ndani yake mfano dakika 250 meseji 100 na 1Gb kwa bei fulani lakini kwasasa ni hatari sana dakika 250 sms 100 na 10 mb

Nawapenda Vodacome nanaitumia tangu 2005 lakini hizi zimesababisha tutafuta chip mbadala kwaajili hizo Gb's
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

  • Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
  • Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
  • Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
  • Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
  • Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Naomba kujua kama naweza kupata settings za MMS kwenye simu yangu.
Namba: 0767918675
 
Kitu kinacho nishangaza kwenye mtandao wa vodacom ni kwamba mteja anayetumia sana huduma zenu ndo anapandishiwa gharama kwenye vifurushi vyake tofauti na mtu anaetumia line yenu mara moja moja, yani mke wangu ni mteja wa mtandao mwingine anatumia voda kwa mwezi mara 3 au 8 package zake very cheap compared na mimi niliye na line yenu kwa muda wote. Huwa siwaelewi formula yenu, nilitegemea mteja wa muda mrefu mtampunguzia mzigo. Mke wangu mwenyewe nashangaa voda anasema hawa wafanyakazi wa voda wanafikiria kwa makalio nini.
wanamvuta mdogomdogo baada ya Muda wanampandishia mazima
 
Vodacom,

Huduma yenu ya Magic voice.

Wote sio watoto wadogo mmenitumia.ujumbe mara nyingi sijajishughulisha, menipigia simu nimeongea na wahudumu wenu nimewaambia kabisa, najua ni huduma yenu na mnahitaji wateja ila mimi sitaki.

Sasa hii ni mara ya pili, nawapigia juu ya kulalamika mnanikata sh. 200 kwenye salio langu. Na mbaya ni salio balokuwa nimeweka for emergency. Nikisema kununua vifurushi hamkati. Nikisema niweke likae tu mnalitafutia sababu.

Process ya kujiunga na huu ujinga wa mavoice ni mrefu sana.. kwa mtu kama kutokujua kama nimejiunga au la. Jibu ni mnaniunganisha nyie. Sasa nawaambia sitaki. Kesho nitawatumia email. Iwe kumbukumbu mkitudia tena tutakutana TCRA.

Muache wizi.
 
Back
Top Bottom