Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Sera ya TTCL ingebadilishwa ili iendane na wakati tulionao hivi sasa wa kibiashara ya mawasiliano SIM nchini sera hiyo inyotumika hivi ni toka shirika ninanzishwa miaka hiyo likiwa halina mshindani kumtegemea mh Rais awapigie Debe bila kutangaza huduma zenu kwa watumiaji wa sim nchini itakuwa ngum kwenu kupambana wapinzani wenu sokoni mitandao ya SIM inajitangaza Sana kuhusu huduma zao nyinyi nyinyi uongozi WA ttcl mnamtegemea mh rais na mshatoa gawio matangazo badiliken na sera badilisheni indane na wakati tulionao sasa
 
HARUFU YA UTAPELI/UDANGANYIFU WA VODACOM NA M-KOBA YAO

Habari wakuu!

Kuna nini nyuma ya pazia kwenye hii M-Koba ya Vodacom? Naitafsiri kama wizi/utapeli/udanganyifu, inaonekana ni njia wanayoitumia kukusanya hela za watu pengine na kuzifanyia biashara ama kazi zingine za kiuchumi.

Haiwezekani kwenye akaunti kuna hela lakini kuitoa haitoki licha ya kufuata taratibu zote za kutoa pesa (Katibu kuanzisha muamala, wajumbe wawili kuidhinisha, Mhazini kuidhinisha na mwisho mwenyekiti kuidhinisha). Lakini hakuna hela inayohama. Na kwa sasa ni mara ya tatu sasa bila mafanikio, nikiwauliza wanasema hela haikwenda jaribu tena.

Kingine, wanasema kuhamisha pesa kutoka hiyo Akaunti ya M-Koba kwenda kwa mwanachama ni bure lakini tulifanikiwa kufanya muamala wa kwanza na ndio ukawa wa mwisho hadi sasa, ujumbe wa salio ulioletwa ukawa tofauti na salio tulilolitarajia maana ilipungua 10,000. Baada ya kuwauliza wanasema ujumbe umekuja kimakosa lakini salio halijapungua kwenye lile tulilolitarajia (kilichonistua ni kwamba mfumo wao haujui hesabu? Maana ujumbe wa kuhamishwa pesa ulienda kwa wajumbe wote na kias cha salio lililobaki kwenye akaunti).

Ku-deposit hela kwenyewe hakuna shida, hela zinaingia vizuri mno kutoka M-pesa kwenda hiyo M-Koba. Kuitoa sasa ndio udanganyifu unapoanzia. Wanasubili hadi waifanyie biashara kwanza ndio watoe?

Anayeweza kuwa-tag tafadhali.
 
@Vodacom Tanzania
 
Katika watu wasiojielewa basi ni nyinyi hasa hilo duka lenu la victoria,muna nyodo na njaa.......

Yaani munataka mteja awabembeleze nyinyi aiseeeehhhh

Nimeenda kusajili line kwa alama za vidole bahati mbaya mwanzo nilisajili na kitambulisho cha kupiga kura na kwasababu picha zinaonekana tofauti kwa mbali kutokana hii nimepiga miezi miwili iliyopita na nyingine nilipiga miaka mitano iliyopita eti wanadai affidavit.....hawawezi kunisajiri hahahahah

Wakati tigo,airtel na halotel wamenisajiri bila vikwazo.......

Aiseeeeh hiyo imekula kwenu
 
Kama huu ukurasa bado Voda mnapitaga napenda kuwajulisha kuwa kuna hujuma inafanyika ofisini kwenyu kwa mtu/watu walio zamu kuanzia saa kumi kamili hadi saa kumi na moja na dakika ishiri leo hii 2/11/2019.

Sitasema hapa ni ni lakini hii ni hatua ya kwanza ikiwa ni taarifa itakayofanyiwa kazi
 
Habari mm nina tatizo kwenye network inaonyesha mtandao upo lakini nikiingia tu mtandao unakata sijui tatizo nn
 
voda punguzeni kututumia SMS ambazo hazina ulazima zinakera... kila cku mnarudia SMS zilezile alafu zinaingia nyingi dah!
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
mna gharama kubwa sana kila siku bei za vifurush na makato ya mpesa yanazd kua makubwa...kwa cc tusiokua na kaz mnatuumiza
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Katika kifurushi cha Kaskazini Offer kuna chaguo la dk 150 voda-voda, dk 15 mitandao yote na mb 1024 kwa siku tatu, kwa shs 1,500/=. Leo ni mara ya tatu nanunua kifurushi hiki lakini ukiangalia salio baada ya muda mfupi tu unaambiwa una dk 0 mitandao yote ambapo nakuwa bado sijapiga simu yoyote.

Ina maana kwamba kwa siku tatu hizi nimeuziwa kifurushi hewa cha dk 45 mitandao yote, licha ya kwamba leo nimepewa ofa ya dk 15 voda-voda lakini nilipouliza salio nikaambiwa nina dk 10 voda-voda! Kama ndivyo mnavyowafanyia wateja wote basi bila shaka mnatuibia pesa nyingi sana. Sikupenda kutumia lugha hii, ila sioni kama hii inatokea kwa bahati mbaya.

Naomba mtoe maelezo ya kutosheleza juu ya huu udanganyifu ili kurejesha imani yetu kwenu kwamba hamkuwa na nia mbaya nyuma ya pazia, na tutendeeni haki kadri mnavyoelekeza kwenye menu zenu za mauzo.
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania

Toka muda wa saa moja asubuhi mganza kagera mawasiliano hakuna tatizo litakua ni nini?
 
Kwanini tunapopiga 100 tunasikiliza mambo mengi yasiyotuhusu mfano mtu unataka kuongea na wahudumu utapita michakato miingi ingekuwa vizuri tuweze kuongea na wahudumu kwa urahisi
 
Nataman sana lifanyiwe kazi tuweze enjoy katika nyanja mbalimbal za mawasiliano
*NAYASHITAKI MAKAMPUNI MANNE YA SIMU.*

*BASHIR YAKUB, Wakili.*
0714047241

Naishitaki Tigo, Airtel, Vodacom na Halotel. Kwa mujibu ya Sheria Namba 12/2003 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania mashtaka ya aina hii natakiwa kuyaandikia makampuni hayo taarifa kuyataka yarekebishe ndani ya siku 30 ninacholalamikia yakishindwa naendelea mbele,ambapo nimeshayaandikia makampuni hayo.

Kwenye mashitaka yangu ninaomba mambo matano.

*JAMBO LA KWANZA.* Vifurushi vyote havipaswi kuexpire. Kitu pekee ambacho kinapaswa kumaliza kifurushi inatakiwa iwe ni wewe kuongea hadi dakika zako zikaisha.

Si haki kukata kifurushi cha mtu ambaye dakika zake za kuongea,za data, au sms bado zipo kwa kigezo cha kuexpire au muda wake wa wiki,masaa12,nk kuisha. Nchi nyingi hii kitu imeondolewa imebaki kwetu na pengine pachache.

Mathalan, umejiunga kifurushi cha 1000 na umepewa dakika 10 ndani ya masaa 12. Umetumia dakika 3 tu ambazo thamani yake kifedha ni shilingi 300, na masaa 12 yameisha. Maana yake kwenye 1000 yako zilibaki dakika 7 ambazo thamani yake kifedha ni shilingi 700, ambazo hizo sasa shilingi 700 kampuni ya simu inajirudishia kwa kigezo cha muda kuexpire. Nachelea kuiita huu wizi lakini initoshe kusema hii haiwezi kuwa haki.

Lakini pia ninapolipa 500 na wewe ukaniuzia kifurushi si nimekulipa hela yako yote na wewe hunidai. Sasa kwanini tena unachukua kilekile nilichonunua kwako na hela yako yote nimeshakulipa.

Ni hivi,unaponunua kifurushi ni sawa na umenunua bidhaa, na ukishanunua bidhaa hakuna mtu mwingine yeyote, akiwemo aliyekuuzia bidhaa hiyo, mwenye haki ya kuichukua tena bidhaa hiyo yote au sehemu yake isipokuwa wewe uitumie mpaka iishe.

Tizama Tanesco na LUKU. Tanesco akishakuuzia umeme/units ukamlipa basi hatma ya units zako ni utumie mpaka umalize.Hawezi kuikata na kujirudishia kwasababu anajua alikuuzia bidhaa na wewe ukamlipa na hivyo una haki ya kutumia bidhaa yako mpaka umalize. Hii ndiyo HAKI.

Kinachofanywa na makampuni ya simu ni sawa ununue mkate dukani na mwenye duka umlipe hela yake yote. Halafu mwenye duka huyohuyo akwambie kwamba usipokula mkate huo kufikia saa 12 za jioni au ndani wiki au mwezi nitakuja tena kuuchukua nyumbani kwako, na aje kweli auchukue iwe mali yake tena kwa mara ya pili.

Zaidi ya hayo,ukweli halisi ni kuwa kifurushi kwa muundo wake si bidhaa inayoexpire. Ukinunua mkate ukiexpire utauona, utaona kabisa kwa macho umeoza kadhalika bidhaa nyingine zenye sifa ya kuexpire. Lakini kifurushi kwa uhalisi wake si bidhaa inayoexpire au yenye sifa ya kuexpire.

Hili neno kuexpire limetengezwa ili kuficha neno kupora au uporaji. Ukweli ni kwamba kifurushi kinaporwa makusudi kwa kigezo hovyo kabisa na dhahania cha kuexpire, sijui masaa yako 12, sijui wiki yako, sijui mwezi wako umeisha nk. Kifurushi kinaishaje kabla dakika zangu nilizolipia kwa ukamilifu sijazitumia zikaisha ?.

Yapo haya nayo lazima yaeleweke, mtu amejiunga lakini yuko safarini hawezi kutumia mda wake , mwingine alipo hakuna network, mwingine hajatumia mda wake alikuwa bize na kazi zake, mwingine simu haikuwa na chaji siku nzima, mwingine umeme ulikatika alikosa mawasiliano nk nk, hawa wote pesa zao walizolipia na hawajazitumia au wametumia kidogo zinakatwa na makampuni ya simu yanajirudishia pesa hizo bila kujali.

Nimefungua kesi kuondoa unyonyaji huu na lazima uondoke.Hatuwezi kuendelea kuwa viwanda vya kutengeneza ukwasi wa makampuni ya simu.

*JAMBO LA PILI*. Haki ya kutochanganyiwa kifurushi na muda wa kawaida wa maongezi bila ridhaa.

Nitatoa mfano, unakuta mtu ameweka shilingi 1000 kwenye simu ambapo anajiunga 500 na 500 inabaki kama muda wa maongezi wa kawaida. Wakati anapokuwa akizungumza au akitumia data kupitia ule muda aliojiunga na ukaisha basi simu haikatiki bali inaunganisha moja kwa moja na ile 500 ya muda wa maongezi wa kawaida ambayo alikuwa hajajiunga.

Hii si sawa hata kidogo na ni vitu ambavyo vinatengenezwa maksudi ili kujipatia fedha bila kujali mtumiaji anaumia kiasi gani. Ni hivi, mtu anapoamua kujiunga 500 na akabakisha 500 bila kuiunga ana maana yake kubwa tu.Hakushindwa kuunganisha 1000 yote.Amechagua 500 kwa maksudi maalum. Sasa iweje unamlazimisha kutumia akiba yake ya 500 hata bila ridhaa yake.

Inatakiwa kuwe na chaguo(option) iwapo mtu anahitaji huduma ya aina hiyo au hapana. Au inatakiwa muda wa kifurushi ukiisha simu ikate halafu kama anataka kuendelea kutumia muda wa kawaida achague mwenyewe kuendelea kuutumia na sio kampuni ya simu kumchagulia.

Au kama anataka kujiunga na hiyo 500 iliyobaki basi ajiunge. Isiwe biashara ya kuviziana kama ilivyo sasa. Hili nalo lazima waliondoe.

*JAMBO LA TATU*, Haki ya kujua matumizi ya kifurushi.Malalamiko ya vifurushi vya watu kuliwa isivyo kawaida ni mengi mno.

Unanunua dakika 20 unaongea 10 unaambiwa kifurushi kimeisha, unabaki kushangaa. Ni lazima waweke mfumo wenye kutoa taarifa sahihi na za wazi(transparency) ili kumwezesha mtumiaji kumonita matumizi ya kifurushi chake.

Malalamiko ya watu ya kutumia vifurushi chini ya kile walichonunua yanaongezeka siku hadi siku. Kuwaachia makampuni ya simu wao wawe ndio wauzaji wa vifurushi, na wao hao hao ndio wakueleze umetumia nini,kama umemaliza au hujamaliza, huku wewe mteja ukiwa kipofu/gizani ukisubiri kupokea lolote wanalolisema wao, kupigwa hakuwezi kukwepeka.

Waweke mfumo ambao wao pamoja na mteja watamonita matumizi ili mteja aweze kuhoji. Teknolojia imekua hili ni dogo sana.

*JAMBO LA NNE.* Haki ya kuhamisha kifurushi.

Nimesema hapo juu kifurushi ni mali yako na ndo maana unailipia pesa na hivyo kuwa na haki ya kuitumia kwa uhuru.

Kwa msingi huu makampuni ya simu ni lazima yaweke mfumo unaomwezesha mtu kumhamishia mtu mwingine kifurushi kama ilivyo kwenye muda wa kawaida wa maongezi. Maana yake nikinunua kifurushi cha 1000 labda dakika 10 za maongezi, Mb 100, na sms 50.

Niwe na uwezo wa kumgawia yeyote ninayemtaka kiasi cha muda wangu wa maongezi,sms au Mb. Na hii inafanyika nchi nyingi na inawezekana zaidi kugawiana watu wa mtandao mmoja.Tunahitaji uhuru huu kwetu.

*JAMBO LA TANO.* Haki ya kupewa tahadhari kuhusu kifurushi au muda wa hewani unapokaribia kuisha. Kuna makampuni wana huduma hii lakini wanaitoa kwa hiari sana na wengine wameacha kabisa. Wengine wanatoa tahadhari muda unapoisha na sio unapokaribia.

Tunataka watoe unapokaribia ili mtu ajipange. Ni haki mtu kupewa tahadhari wakati akizungumza,akiwa kwenye mtandao, au sms, kuhusu dakika zake kukaribia kuisha. Sio sahihi wala ustaarabu simu kukatika ghafla bila tahadhari.

Na wanafanya hivyo maksudi wakijua unapokatakiwa na mawasiliano ghafla ni lazima tu utakuwa hujamaliza haja yako na hivyo utalazimika kuongeza vocha ili umalizie na wao wapate mauzo zaidi.

Wanajua ukipewa tahadhari unaweza tu kufupisha mazungumzo yako na wakati simu inakatika ukawa tayari umemaliza na hivyo usihitaji tena kuongeza vocha. Tabia za hovyo kabisa za kuviziana.

Unawezaje kunipa tahadhari ya muda kuisha ukashindwa kunipa ya muda kukaribia kuisha. Hili nalo tunataka lifanyiwe kazi.

*SHERIA*
Mambo haya kwa ujumla wake ni kinyume na Katiba ya JMT Ibara ya 18( c ) inayotaka uwepo wa mawasiliano bila kuingiliwa, lakini yanakiuka Kanuni za Kielektroniki na Mawasilano ya Posta kuhusu viwango vya Tozo GN. No 22/2018 hasa Kanuni ya 4 ( 1na 2) inayotaka viwango vyote vya tozo za simu kuwa vya haki na kadri(just and reasonable), yanakiuka Kanuni ya 4 ya Kanuni za Kielektroniki na Mawasiliano ya Posta GN No.61/2018 kuhusu kumlinda mlaji inayotaka mlaji kupewa taarifa kwa usahihi ya matumizi ya huduma muda wote, yanakiuka Sheria ya Ushindani namba 8/2003 inayotaka mtoa huduma kutoa huduma kwa kuzingatia zaidi maslahi ya watu wa hali ya chini, na sheria nyingine nyingi zimekiukwa.

Na tuelewane vizuri hapa, hakuna kitu kinaitwa VIGEZO NA MASHARTI KUZINGATIWA. Sheria iko wazi kuwa neno,maneno,sentensi au msemo wowote wenye lengo la kusigina haki ya mtu/watu ni batili.

Basi nitaviomba vyombo vya maamuzi vitusaidie kuyaweka sawa haya matano.Tutazidi kupeana taarifa kadri inavyokwenda.
 
Mamlaka ya udhibiti wa mawasiliano Tanzania,ifuatilie kwa makini muda na ubinyaji wa vifurushi unaofanywa na mitandao ya mawasiliano nchini kama vile Vodacom ,kumekua na ubinyaji wa makusudi wa muda na kasi ya bando za internet

imetokea mara nyingi unanunua kifurushi cha bando la internet mfano 1 GB na kuendelea wanachofanya wanafanya data limit na muda unazidi kwenda hata ukiingia katika kuitumia inakuletea 0.0/KBS kwa muda mrefu sana huwezi kutafuta au kupakua unachostahili katika mtandao husika, hiyo ni aina fulani ya kuwaibia wananchi watumiaji wa vifurushi husika,hivyo mamlaka ya mawasiliano Tanzania fuatilieni hilo maana haina maana ya kusema wanyonge wakati mitandao inawanyonya wananchi.
 
Achana nao njoo Halotel ule bata
Mamlaka ya udhibiti wa mawasiliano Tanzania,ifuatilie kwa makini muda na ubinyaji wa vifurushi unaofanywa na mitandao ya mawasiliano nchini kama vile Vodacom ,kumekua na ubinyaji wa makusudi wa muda na kasi ya bando za internet,imetokea mara nyingi unanunua kifurushi cha bando la internet mfano 1 GB na kuendelea wanachofanya wanafanya data limit na muda unazidi kwenda hata ukiingia katika kuitumia inakuletea 0.0/KBS kwa muda mrefu sana huwezi kutafuta au kupakua unachostahili katika mtandao husika, hiyo ni aina fulani ya kuwaibia wananchi watumiaji wa vifurushi husika,hivyo mamlaka ya mawasiliano Tanzania fuatilieni hilo maana haina maana ya kusema wanyonge wakati mitandao inawanyonya wananchi.
 
Back
Top Bottom