Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Acha kuchongea watu wafukuzwe kazi, kama anamapungufu ongea nae umweleze
Vodacom! Kuna mfanyakaz wenu anaitwa Mary Grory ni Supervisor! Kiukwel huyo mdada hastaili kuwepo ktk position ya kuhudumia! Mfano unaweza kuwa na tatizo la system, Yan kuja kulitatua inaweza kupita hata miezi 4! Sasa kwa kufanya hivyo wateja wanaokuja ktk hizi voda shops au voda desk wakikuta huduma zinazohitaji system hakuna kwa siku 4au zaidi hawawezi kurudi na kuwapoteza! Jaribuni kumweleza huyo muhusika ili abadilike!
 
Hivi voda ni kwann mnadanganya sana unakuta mnatuma sms umeshinda sms za bure tuma hiv upate dk zak gafla umejiunga na soka letu ndo nn sasa
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

  • Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
  • Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
  • Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
  • Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
  • Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Salama jamani.

Samahani, hiki suala LA kusajiri university offer limesitishwa ama??
Nimeunganisha Kwa muhudumuwenu wa hapa Nyamalango malimbe Saut Mwanza akanipa Sikh tatu kuwa mambo yatakuwa sawa.

Lakini mpaka sasa ni zaidi ya siku tano bila mafanikio. Naomba kujua kama hiki huduma imesitishwa ama ili niunganishe mitandao mingine.
Regards

Mtema wenu.
 
Vodacom..nasikitika kuwatangazia kuwa, mm mteja wenu wa muda mref sn NIMEAHAMA RASMI.

SITAWEKA VOCHA YYTE wala KUUNGA BUNDLE LA AINA YYTE!!

NB: mm ni wakala wa M-Pesa, wateja walalamika sn kuhusu ada za kutolea hela M-pesa, mtafirisika muda si mrefu!!

Mark my words
 
Vodacom nimeishindwa kutokana na ghrama zake kuongezeka kila mara.
Nimeshaachana nayo. Ni vizur mtu utumie hela kulingana na kipato chako.
 
Kweheri vodacom, bundle ya tzs 2,500 haikumaliza hata masaa 3. Shwain zenu mnafidia share za Rostam
 
Vodacom wasanii kweli kweli, nimesafiri kwenda Nairobi nikaweka airtime ya kutosha kwenye simu yangu ili niweze kuwa hewani. Cha ajabu nimefika hapa naweza kupiga simu tu ila mtu mwingine hawezi kunipigia.

Niliwapigia Vodacom huduma kwa wateja wananiambia lazima nijiunge kifurushi cha kupiga na kupokea ndipo nitaweza kupokea simu nikiwa Nairobi, kama nina balance kwenye account kwa nini wasikate huko huko?

Kivumbi sasa, nimeangalia vifurushi vyao vipo bei juu kweli zaidi ya ninavyopiga bila kifurushi. Hii si sawa hata kidogo.
IMG-20190925-WA0000.jpg
 
Vodacom tawi lenu la gongo la mboto badilisheni wahudumu yani wanafanya kaz kwa kuringa sana

Nilipeleka documents zangu ili niweze kua Wakala wa M-pesa toka mwezi wa 6 ajabu hadi Leo hii nimeenda Wananiambia bado Majibu hayajaludi
Wakati huo Tigo nimekaa wiki 3 tu nikapata na airtel wiki 3 nikapata Laini zangu ukizingatia nilipeleka siku moja kwnn nyie vodacom pale tawi la gongo la mboto wasumbufu na mnafanya kaz kwa kujisikia?

Au mpaka tutoe hongo ndo mfanye haraka haraka

Mnakera sana Kwa kweli
 
Gharama zenu za bundle
Natafuta maneno ya kistaarabu ya kuwaeleza nakosa ila nafikiri naeleweka maana nahisi nitatukana
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

  • Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
  • Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
  • Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
  • Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
  • Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania

Mimi nakereka sana ninapo kuwa nimenunua kifurushi cha saa24 kabla hakika Isha naambiwa kimeisha au nimenunua dakika 38 nimeongea dakika 15 naambiwa dakika zako zimeisha, nashauri , tengenezeni utaratibu wa kunipa taarifa kila baada ya maongezi kuwa nimetumia dakika ngapi, na kama zimeisha niwekeeni utaratibu wa taarifa utakao nijulisha Imeishaje ishaje, vinginevyo sina furaha na kampuni yenu tena.
 
Hivi nyny bado mpo vodfyomu... Mimi nisharudi nyumbani TTCL, na internet naiwait ramadhani ofa ya Halotel ya usiku full raha kasi ya ajabu had 3mb/s. Wanatoa Gb za kumwaga kwa buku tu na ndo wapo 3g...mchana na nufaika na airtel kwa buku nakula dk 110(10 mitandao yote) gb 1 kwa siku tatu... Sms nipo halotel kwa buku tu nakula text 5000 mwezi mzima...yan natongoza hadi huduma kwa wateja wa voda... Sijui mutuma pesa nawatumia Tigo...yani vodafyomu sina habar nao Hawa ni .matapeli kama Iphone...yan wanakuletea ushuz kwa kusingizio cha upremier huku wakijua wateja hawawez hama au kuacha kutumia mihuda yao yakifalailo...kuku hao..

Bora utumie Zantel kuliko hawa wez Vodafyomu...nawashaur wabadili .meneja
 
43 Reactions
Reply
Back
Top Bottom