Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
KWa mtazamo wangu na Experience niliyo nayo kwenye utumiaji wa Simu za Mkononi ninapata shaka inayoniaminisha kuwa wezi wa mtandaoni wanashirikiana na watu wa Simu, siamini kuwa hawa provider wanahitaji kufanya kazi kubwa kumpata mwizi wa mtandaoni hasa wakiashaambia number ya mtu aliye tapeli. Mfano mini ananitumia sms akitaka nimtumie pesa immeditely nilitakiwa niitume hiyo number VODA wao wamfuatilie huyo mtu na atakiwe kufika katika ofisi zao ili kuthibitisha kuwa yeye ni mteja halali na kwamba anatakikiwa kuendelea kupata hduma. sasa Polisi wanaishi kutuambia tusitume pesa kwa watu tusio wajua lakini hawa watu wapo very technical na ni rahisi kukudanganya. Unapopatwa na tatizo unalipeleka Polisi, mpelelezi anakuambia swala lako ni gumu sana kwani VODA au TIGO hawatoi Ushirikiano wa haraka kutoa taarifa ya huyo mwizi ili sisi tuweze ifuatilia na mimi nimethibitisha hilo baada ya kuibiwa kimtandao niliripoti na hadi sasa mwaka unaisha sijapata msaada wowote. HIvyo nime Coclude kuwa Polisi na hawa Watu wa phone provider wanashirikiana kuwaibia raia wa Tanzania.
 
Data datani siielewi mjali na thamani ya pesa ya mteja .nimejiunga kifurushi Cha 500 wakaongeza za kwa 75.nimewasha data hakuna download hakuna message iliyoingia napokea message kifurushi kimekwisha .data datani kwa Mimi hapana .haiko sawa
 
LEO MPESA WAMENIKATA ZAIDI YA ELFU 60.KULIKONI?NIMETUMIWA 250000 NIMELIPA MPOWER 77000 NIKANUNUA SALIO 5000 NIKATUMA 47000 NA 20000 JUMLA 149000/-BAKI 101,000/=NIKAINGIZIWA MPOWER 75000 WAKAKATA RIBA BAKI 101,000! SIELEWI NILALAMIKE WAPI?
 
  • Thanks
Reactions: VMD
Vodacom M-pesa mna shida gan mbona mnaongeza kila kukicha gharama za makato kwa anaetoa
 
Kimetokea nini mkafanya haya mabadiliko? Mmefanya tathimini kwanza? Hizo namba hazilingani na kipato cha watanzania wengi... Total disappointments...
IMG_20190608_200203.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: VMD
Sory, hiv naweza pata msaada wa kujitoa kwenye haka kamfumo ka kutumiwa sms kutwa kucha za kubet ..., maana nshaacha hiz mishe muda sasa
 
nyie ni wezi mnatuibia sana watz na naenda kuwachoma leo tcra ushahidi ninao mara kibao mnaiba izo senti ngapi ngapi sh ngapi zitawatoka puani subirini vya halali..kamtandao ka kike mnawaza tu kuchuna wateja wenu voda kweli mnadanga
 
Hili gawio mnalotulipa wateja linatokana na nini? Halafu pesa yenyewe haitoshi hata kununua jojo!

Heri mbaki nazo hizo pesa na siyo kutukebehi!
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania

Muwe wa kweli, tusilete shida hapa halafu iwe ni blablaa. 1. Nimetuma pesa kwa simbanking kutoka CRDB kuja account yangu ya Mpesa tangu asubuhi ya leo haijafika kwenye namba yangu ilihali benki imeshakatwa. 2 sijawahi kuona kitengo cha hovyo kama custormer care ya Vodacom. Hakuna mhudumu anayepokea simu. Mlikiweka cha nini?
 
  • Thanks
Reactions: VMD
Vipi mbona vifurushi vya chuo mmepandisha kimya kimya kutoka 2000 hadi 3000, haa vodacom mtauwa bendi. Fanyeni tayhimini, la siyo tutawahama mzima. Tunawapa muda, mbona wenzenu ni Safi tu, nyinyi mnashida gani?
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Nina laini zenu mbili, soon nazitupa maana hizi bundles zenu za internet ni zaidi ya wizi
 
43 Reactions
Reply
Back
Top Bottom