Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vifurushi vyenu sio rafiki kwa wateja, halafu nakerwa na msg mnazotuma pasipo ridhaa yangu mara za mpira mara za kubet mara nk, unaweka sh 500 kwenye simu lkn unatumiwa msg kibao, kwa nn isitumwe msg 1 yenye maelezo yote, huwa inanibore sana, mtu unaweka vocha lkn inakubidi usubiri kutumia mpaka mtakapomaluza kutuma msg zenu.
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

  • Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
  • Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
  • Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
  • Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
  • Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
naomba msaada kujua kuwa unapokuwa na akiba kwenye M-PAWA gawio linakuwaje? maana kwanza gawio lenu mnalitoa baada ya miezi mitatu.

Na je nikiwa na salio kwenye mpesa kuna gawio lolote lile? na tofauti kati ya gawio la m-pawa na m-pesa ni ipi?
 
Nimechoshwa sana na meseji za matangazo ya biashara zenu mara Tatu mzuka,Beti na upuuzi mwingi kama huo kama vipi muanze kutulipa maana matangazo sehemu zote yanalipiwa hata nashindwa kupumzika kila baada ya muda meseji au mtupe namna ya kuya block.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pumbavu zenu VIDACOM, kama deni la 6b ndio mnataka mlilipe hivi mbwa nyie, kila siku nikiweka vocha ya 2,000 nakwata hizo tsh 3,
Pumbavu zenu fala sana nyie, MNAKERA SANA

Screenshot_2019-04-17-18-45-19.png
 
Vodacom toeni maelezo juu ya zoezi la usjili mpya wa line utakao tumia alama za vidole.
utahasiri vipi account za M-PESA kwa watu ambao hawatakuwa na vitambulisho kipindi cha usajili,pia kuna njia mbadala kusajili line kwa mfumo mpya tofauti na kitambulisho cha taifa,mtakuwa na vituo vya kusajili tofauti na vodashops?.
 
Nawashauri msijaribu katu kuiga mfumo mpya wa tigo pesa. Nawatahadharisha kwa kuwa nafahamu huwa mnaigana mambo mengi kibiashara.

Kwa tigo pesa sasa hivi miamala yote ya pesa, iwe kulipa, kutuma ama kupokea hakuna taarifa (message) inayotumwa na mtandao kukutaarifu kiasi kwamba mpaka uingie kwenye main menu kuulizia salio ama token ulizotumiwa kwa mtandao.

Nanyi wanaJf changieni kwa uzoefu wenu, ila mie nimeachana nao kwa masuala ya pesa. Nimebaki na mawasiliano tu!
 
Mi hawa jamaa walishanishinda,bando za mwanachuo zinabadilika rangi kila kukicha.nmeona niwaweke pembeni hakuna namna
 
Kuongeza bei ya kifurushi cha sms kwa mwezi mzima wakati mitandao mingine bei iko simple no kufukuza wateja,nilijiunga sana kifurushi chenu ila kwa sasa hamnipati tena mpk mshushe bei ndio nitarud tena
 
M-pesa ina shida gani jamani? Nanunua vifurushi hela inakatwa siunganishwi
aseee,, nipo najuiliza hapa,,, hela nikituma inaenda na nnarudishiwa msg,, nmeshaunga kifurushi hadi salio limekata lakn hakuna muda wa maongezi nimepata nikiwapigia network bize,,, yaan jamaa wa ajabu hawa jakuna mfano
 
Vodacom naitaji ufafanuzi ktk hili swala langu:-

kipindi naitaji line ya uwakala nilifka ofisi za TRA nikapigwa picha za kielectonic na finger print pia, baada ya hapo nikalipia leseni ya biashara kwa ajiri ya kupata line ya uwakala..

Swali langu ni hili kwa nini mniambie nikaisajiri line hii ya uwakala tena kwa mara nyingine kwa mfumo huu wa vidole, wakati nilishapigwa mapicha na finger print pia, inamaana hizo finger print na picha hazitoshi ama zina tofautiana baina ya vidore nilivyoviacha huko ofisi za TRA na hizi za NIDA? hamuoni kuwa ni kama mnatupotezea mda wa kila mda kuchukuliwa finger print wakati mambo ni yale yale?!!
 
Back
Top Bottom