Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Hawa jamaa wa voda bure kabsaa...eti wanatoa vifurushi vyakuanzia kila mara wanapandisha gharama zake....1500,2500,leo wameweka kifurushi cha 5000,Dar supa Uni.....hivi hii bihashara yenu mnarenga Wateja watanzania wenye kipato cha chini au kwa wenye kipato cha Juu tu????
 
PAYPAL-VODACOM

Hili suala linaniumiza sana kichwa kwani nina kama $123 kwenye paypal lakini tatizo linakuja kuamisha kutoka paypal kuja hapa Tz mbona kenya wameweza kuunganisha hiyo ishu na wanatoa hela kutoka paypal kuja kwenye M-pesa.

Je Tanzania tunakwamia wapi yani hata hiyo M-pesa MasterCard nayo haitaki kupokea hela yenyewe ni kutoa tu kufanyia malipo ya mtandaoni ila mimi ninachoomba muiboleshe basi ili hata tuweze kuweka hela kupitia hiyo M-pesa MasterCard. Mi ni hayo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Ni lini mtatuletea vifurushi maalumi (special bundles) vya kustream sisi wateja tunaotumia Smart Devices haswa TV majumbani.
 
PAYPAL-VODACOM

Hili suala linaniumiza sana kichwa kwani nina kama $123 kwenye paypal lakini tatizo linakuja kuamisha kutoka paypal kuja hapa Tz mbona kenya wameweza kuunganisha hiyo ishu na wanatoa hela kutoka paypal kuja kwenye M-pesa. Je Tanzania tunakwamia wapi yani hata hiyo M-pesa MasterCard nayo haitaki kupokea hela yenyewe ni kutoa tu kufanyia malipo ya mtandaoni ila mimi ninachoomba muiboleshe basi ili hata tuweze kuweka hela kupitia hiyo M-pesa MasterCard. Mi ni hayo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo sio voda bob, ni BOT wao ndio hawajairuhusu paypal kufanya kaz tz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani tuwe macho na mtandao wa Voda nchini kuna wizi unaendelea na tukikaa kimya kweli wanatengeneza za wizi kwa watu wengi sana kwa njia hii.

Hata na mimi nakatwa pesa hata sielewi hii huduma ya kutumiwa za habari kwa njia ya Sms nimeiomba lini na sijawahi hata siku moja kuimba !! Kila nikiweka pesa ili ninunue muda wa maongezi naambiwa pesa niliyoweka haitoshi kwani imekatwa kwa ajili ya huduma hiyo.

Mhhh nimeamua kutoa line yao na kuweka mtandao mwingine, wahusika mtusaidie kuhusu mtandao huu kweli inawaibiwa wateja wake.

Sent from my HUAWEI VNS-L21 using Tapatalk
 
Number hii ya VODA 0742 780 349 imesajiliwa kwa jina la HUSNA KETI. Ni ya tapeli. Anakupigia simu akikueleza ni mtumishi wa Vodacom makao makuu, anakueleza umeshinda Mpesa bonance. Ukimshtukia tu matusi atakayokupa ni hatari. Take care. Imesajiliwa kwa jina la kike, anayeitumia ni wa kiume.
Uongozi wa Vodacom Tz. Mpo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna tabia naona inajirudia najiunga kifurush kwa M PESA mnakata mara mbili na salio la kifurushi linabaki lile lile la kimoja, nmeshatoa malalamiko sipatiwi suluhisho...mnakera sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna baadhi ya supervisor ambao ni wavivu na hawasaidi watoa huduma ambao wapo kweny hizi deskshops.. unakuta unawatumia atatue tatizo anachukua mpk miezi 3 hajatatua! Halafu kila siku visingizio ambavyo havina msingi! Kama wanashindwa kuwasaidia ni Bora watoke ofisini na wapewe supervisors ambao watakuwa na uwezo wakuwasaidia Hawa wahudumu wa hizi Vodacom service Desk..



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juzi Ijumaa nilinunua bundle ya 2GB ya wiki lakini nilpojaribu kutumia internet ilishindikana. Baada ya nusu saa nikaangalia salio. Chakushangaza ni kukuta sina salio! Sikufanya matumizi yoyote kwani Internet ilikuwa haipatikani. Bundle langu limeenda wapi?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
leo tarehe 24 march internet yenu ipo slow utazani haijui kama stars wameshinda leo mlipaswa muwe sharp
 
43 Reactions
Reply
Back
Top Bottom