Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Nimejiunga kifurushi cha 2000 nikapewa offer ya instagram bure mwezi mzm.
Cha kushangaza zilivyoisha haifunguki tena.
Why😞😣
 
Tatizo makato ya kutolea pesa n makubwa mnoo alaf mnajifany ofa hamzitoi na mkitoa kam vil watu tunafanya kaz serikalin ofa utasikia mb 250 kwa 10000/= nakuuliz ww voda kuna usawa hapo???
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Kuhusu m-pesa mastercard je,inauwezo wa kupokea pesa ? .kama ni dollars zitakuwa TSH?
 
Siku hizi voda ni kero kwa mbele! Internet haifai kabisa maeneo ya Madale. Kuiba salio usiseme
 
Huduma ya Weekly Auto-renew imewekwa upya kwa gharama ya TZS500.00. Makato mengine yatafanyika 2018-12-31 00:00:00. Bonyeza gemu.vodacom.co.tz kwa game zaidi. Kujiondoa SMS ONDOA kwenda 15430. Shinda simu janja hapa https://bit.ly/2rmYax


Voda wizi umezidi. Yaani msione kuna salio kwenye simu ya mteja. Acheni upumbavu huu.
Huduma mnalazimisha na hela mnakata.
 
Napenda kufahamu kuhusu suala la TUZO points, Nikiuliza salio naambiwa nina sh 3150 lakini nikitaka Kuvuna naambiwa salio langu halitoshi nina sh 21... ufafanuzi tafadhali!
 
Supa uni,siku ambayo niliweka buku mbili(2000) nikajiunga na bando la chuo ndani yake unapata muda wa maongezi ya voda to voda na dakika chache mitandao mingine shindani na gb 1(mb 1000) za my surf internet lkn kilichonikuta siku within a few hours nikapewa sms notification kuwa mb zimekwisha.Sikuamini lkn ndio hvyo ilikuwa zimekwisha.
From that day no long Vodacom member period!,ilikuwa ni ujuzi wa kiwango cha juu sana .
Nilijaribu kuwapigia customer care huwezi amini nilikutana na utaratibu mreefu hadi kumfikia muhudumu alikuwa zamu, maelezo hayakujitosheleza kuhusu matumizi yngu au ni nni kilitokea hadi kufilisiwa mb zangu.
Vodacom asanteni kwa huduma zenu lkn mmi tena basi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwani huko voda sijui mnapewa huduma bure? maana kila siku malalamiko na kuhama hamtaki
Tatizo vijijini tunakotoka wanatumia Voda sana sasa unajiuliza nikihama voda kule kijijini mzazi ataweza kujiunga bando la mitandao yote?
Kwa hiyo mitandao mingine iji supply kama voda then watapotea kidogo kidogo
 
kama magawiwo yenu yatakuwa cha mtoto kiasi hicho kwa mara ya tatu mfululizo basi hisa zitashuka hadi jero, DG and Chairman Mfuruki what have you to offer to the shareholders? hisa zinashuka from 900-720TZS why?

Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
 
TCRA/BOT komesheni dhulma hii:

Ipo hivi. Unamtumia mtu pesa kutoka mpesa kwenda namba ya mtandao mwingine. Lengo ni mlengwa wako apate fedha bila makato (inaenda kama meseji). Mlengwa wako hapati meseji wala voda hawakwambii kama pesa haijakwenda. Unapiga customer care wanakwambia kuna tatizo la kiufundi muamala hauwezi kwenda na hawajui tatizo litaisha baada ya muda gani....wanakushauri kuzuia muamala (reverse). Mpaka hapo hakuna tatizo. Lakini wanarudisha pesa uliyotuma tu, ile fee waliyokukata hawakurudishii. Hapa ndio kwenye dhulma ambayo BOT na TCRA ni lazima waifanyie kazi. Kama tatizo la kushindwa kukamilisha muamala ni la kwao (vodacom), iweje wamkate pesa mteja kwa kazi ambayo hawakuifanya? Actually, ki haki kabisa Vodacom ndio ilipaswa kumlipa mteja wake kwa kushindwa kukamilisha muamala kwa wakati.

Ingawa imenitokea binafsi kama mteja wa Vodacom, naamini hili linatokea kwa mitandao mingine pia. Nilijaribu kuwapigia na kulalamika lakini sikufanikiwa.Ni dhulma kubwa kwa kampuni kunufaika kwa kutoa huduma mbovu (si sawa wao kunufaika kwa kushindwa kukamilisha muamala). Nawomba BOT/TCRA kama wanapita humu waone tatizo hili na walifanyie uchunguzi suala ili kukomesha hiyo dhulma kwa wateja.
 
Kifurushi cha halichachi kwanini mmeondoa? Nimekitafuta kwenye menu ya *149*01# sijakiona kulikoni?

Sent from my Infinix-X551 using Tapatalk
 
Back
Top Bottom