Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

M-PESA WAKALA

Mimi nauliza mbona sipewi till yangu ambayo niliiomba tangu mwaka 2013 na wakati till tayari inaonekana inatumika?

Kila nikijaribu kuongea na wafanyakazi wa huku mitaani wananiambia watashughulikia lakini mwisho wa siku wananiomba tu hela hata tatizo hawajalisolve.

Naomba sana vodacom mnisaidie niipate till yangu maana TRA wanadai mapato tangu 2014 wakati kimsingi mimi sifanyi biashara ya M pesa kwa sasa na nilishindwa kwenda kustopisha kwa kuwa nilijua till yangu nitaipata wakati wowote

Till ina jina la Herbert Bathlomeo Nkuluzy
Nipo Tarime, niliiombea Mwanza na Tarime ila ya Mwanza ndiyo ilitoka na ndiyo hiyo sijaipata hadi sasa.
 
Vodacom Tanzania km mnavyojiita
Sijwahi kuacha salio kwny line yangu nikaikuta hata iwe sh 10/huduma kwa wateja wanasema sina huduma yyt ya makato toka kwao lkn kila siku nakwata salio/hvyo basi nimefanya mahamuzi magumu line nimeikata kwa ss niko TTCL
 
Vodacom mnashangaza kwa kweli kwa kuthamini line isiyokuwa active kuliko ile active. Line isiyonunua vifurushi wala kuweka salio mara kwa mara mnaithamini kwa kuipa ya kwako ofa nzuri kuliko ofa za mteja active mkiamini kuwa mteja active hawezi kuhama, mnajidanganya!.
 
Mm nilifatwa na na mhudumu wa mpesa mkoani shinyanga hapa.akaniomba kusajilia laini ya kazi kw ajiri ya biashara ya mpesa.nikatoa na hela elfu 20000.nikutoka mwezi wa 4 mpk leo hiyo laini cjapata.na kila nikiuliza naambiwa zitakuja tu.na ntatumiwa msg.mpk leo ni miezi 8.naona km hawa voda ni matapeli au majizi.nifanyaje?
 
Je vodacom mnajuwa kwamba Arusha mjini na maeneo mengi jirani signal za mtandao wenu ziko chini sana? Ni vigumu sana kutumia data. Yawezekana mnajua je mna mpango gani?
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

  • Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
  • Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
  • Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
  • Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
  • Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
1. Mnakata salio bila sababu za msingi..acheni kutuibia hela zetu

2. Vifurushi vya university offer vimepanda bei sana kiasi kwamba watu wanahamia mitandao mingine yenye vifurushi vya bei nafuu...liangalieni hili vizuri

3. Kule kwetu Rombo mpakani na Kenya simu zinaandika Safaricom na Orange badala ya kuandika Vodacom Tanzania.
 
Umepokea TUZO Pointi 100. Salio lako jipya la TUZO Pointi ni 2918. Piga *149*01# >TUZO kucheki na kuvuna TUZO pointi zako

Naomba Vodacom unisaidie hizi point nazitumiaje. Sielewi
 
Bando zinapanda kila siku nanyi mnajua... Hadi bando za chuo zimekua expensive yaani ile GB mliyokua mnatupa kipindi cha nyuma sio sawa na GB ya sasa.

Hii ya sasa unaweza ukawa unachart tuu whatsap ndani ya masaa 6 hamna kitu. Alafu tunaunga bando ya wiki 2000 ya chuo na ikiisha unaambiwa kifurushi chako cha 1500 kimeisha.
Rudisheni huduma za mwanzo acheni tamaa
 
Bando zinapanda kila siku nanyi mnajua... Hadi bando za chuo zimekua expensive yaani ile GB mliyokua mnatupa kipindi cha nyuma sio sawa na GB ya sasa. Hii ya sasa unaweza ukawa unachart tuu whatsap ndani ya masaa 6 hamna kitu. Alafu tunaunga bando ya wiki 2000 ya chuo na ikiisha unaambiwa kifurushi chako cha 1500 kimeisha. Rudisheni huduma za mwanzo acheni tamaa
Hii ndiyo ilinifanya nikahama taratiiibu...wizi sitaki
 
Vodacom nauliza mbona utaratibu wenu wa ajira ni mgumu na umejaa magumashi mengi sana. Mnazuga kuwa na Vodafone recruitment portal lakini kujiregister ni kazi, kila mara inakataa established passwords, mnablock watu bila sababu,

hivi ajira hapo kwenu zinakwenda kwa reference tuu ya huyu anamjua huyu lets say shemeji yangu alisoma na makwaia basi aniunganishe nipate kazi au? tunaomba mje na press release juu ya mnavyoajiri tafadhali
 
Niko Afrika Kusini kikazi napenda kuuliza kama kuna mtandao wowote wa simu huku ambao mmeunganisha nao kwa ajili ya kufanya miamala ya M-PESA kwa kutuma na kupokea baina ya Tanzania na Afrika Kusini ??
 
Naomba mnisaidie kufahamu namba za Tatu Mzuka au tcra, maana kuna namba imetuma ushindi lakini kila ukipiga haipokelewi.

Nahitaji niwasiliane nao au kama ni utapeli niwashitaki tcra.
 
43 Reactions
Reply
Back
Top Bottom