Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Write your reply... Mtandao wa VODACOM mnakoelekea mnaenda kufail kwa sababu vifurushi vyenu vimekuwa vya ngarama saaana.... na si tulivyo tunaangalia uliko wepesi wa maisha ndo huko tunahamia.. mjihudumie wenyew..
 
Toka jana tarehe 27/10/2018 hadi leo kuna shida kubwa internet maeneo ya chuo cha mipango dodoma miyuji.
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
 
VODACOM mlinifanya nijute kwann nilishawishika kutumia M PAWA.

Nililazmika kukopa pesa kwa mtu na kuingia kwenye madeni wakati nina pesa ya kutosha tu M Pawa kisa tu iligoma kutoka, siku tatu nzima.

Siku nimefanikiwa kutoa nilitoa yote na sitokuja kuweka tena pesa M PAWA, maana hii m pawa ishakuwa huduma ya ajabu
 
Mm nataka kuongea na customer care leo ni siku ya nne nikipiga namba 100 naona maelezo mengi
Ni kweli. Hata Mimi nina shida hiyo hiyo. Maelezo mengi na pamoja na kusikiliza, sijabahatika kukutana na hiyo ya kuongea na muhudumu. No vema watueleze huduma hiyo inapatikana menu gani, au wameifuta?
 
Hivi kweli kabisa Vodacom hamtaki tuongee na watoa huduma kwa wateja... Maana hatuwapi ama hatupati hicho kipengele cha kuongea na mtoa huduma kwa wateja... Ukipiga 100
 
Hivi kweli kabisa Vodacom hamtaki tuongee na watoa huduma kwa wateja... Maana hatuwapi ama hatupati hicho kipengele cha kuongea na mtoa huduma kwa wateja... Ukipiga 100
Kweli kabisa tunashindwa kuongea Na watoa huduma kwa wateja kulikonii??
 
Mnamo tarehe 12 Sept.2018 nilituma pesa kutoka ktk account yangu ya M-Pesa 500,000/= Tsh(Laki 5) kwenda bank ya DTB(Through CELLULANT Tanzania Ltd),sms ya malipo nikaipokea tarehe 13 sept.2018.Cha kushangaza kwenye account ya DTB pesa haikuingia.Nilipiga simu huduma kwa mteja bila mafanikio,kwa bahati mbaya siku hio hio nilitakiwa kusafiri nje ya nchi hivyo nikaondoka na kumwachia mdogo wangu afanye follow up.Alivyowasiliana na vodacom wakamwambia aende Bank ,kwenda bank wakamwambia hakuna pesa iliyoingia,akawapigia tena voda,ila cha ajabu voda hawajafanya chochote na mpaka sasa pesa haijaingia kwenye account.Tafadhali sana Vodacom ninaomba mshughulikie tatizo langu,nimeattach image ya muamala.
 
Ahsanteni Vodacom kwa kulifanyia kazi tatizo langu.Kuweka kumbukumbu sawa pesa zangu zilirudishwa kwenye no yangu ya simu.
 
Vodacom nimefanya malipo kwenye kampuni fulani, mlichelewa kunipa sms, niliipata kwesho yake, mmekiri kuwa ni kosa lenu, ila ni mwezi sasa mnanizungusha. Nashukuru.
 
Huu mtandao haufai kabisa ni wezi waliokubuhu,mimi sasa hivi nimeamua kutumia halotel kwa buku tano wananipa dakika mia mitandao yote 30 halotel to halotel, wakati voda wanakupa dakika 60 mitandao yote na wanaiba kishenzi
 
Vodacom nimefanya malipo kwenye kampuni fulani, mlichelewa kunipa sms, niliipata kwesho yake, mmekiri kuwa ni kosa lenu, ila ni mwezi sasa mnanizungusha. Nashukuru.
Mkuu hao ni wezi waliokubuhu,nashangaa serikali inawaangalia tu wanavyotuibia
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Voda mnaudhi mpk leo hii mwiko mm kuweka salio kweny simu yangu labda mpesa tu na nmeacha kununua bundle za data .mnabundle chache mno jamna ipeni thaman hela ya mtanzania mnponipa mb 1 hivi mm nnaifanyia nn hiyo mb moja ,usiweke vocha kweny simu yako ukaiacha hata kwa dk tano zinatosha kukata hata simu ikiwa imezimwa mnakata huu kama sio wizi ni nn nikapiga sim hudum kwa wateja three times wakasema imetumika kweny data chakushangaza cm yangu ilizima had nkaanza kujiuliza .mna majibu marahisi hamtoi maelezo mazuri huduma kwa wateja ipo ilimradi na nyie muwe nayo ila binafsi sion faida yake.
Muuache huo wizi kwan hela ikikaa kweny simu nyie inawakera nn
 
Vodacom huo mradi wenu sijui poromesheni ya Tuzo point ni janga la kitaifa, yaan mnatu danganya danganya na hizo tuzo point ambazo hazina faida yoyote kwetu, nimepiga huduma kwa wateja eti mnaniambia nyinyi wateja wa pre paid hamna menu ya tuzo point?

Maana yake mmetubagua? Mtuambie tuache kutumia huduma zenu sijui za mpesa, mpawa, airtime recharge nk!
 
Internet yenu kwa KIBAHA mkoa wa Pwani ni tatizo.

Fanyeni utaratibu wa kurekebisha hill ksma lipo nje ya uwezo wenu ni vyema mkatoa taarifa kwa wateja wenu.
 
Write your reply... kwa aliepata chuo cha ustawi wa jamii bamaga ngazi ya cheti na anahitaj chumba karibu na chuo cha ustawi wa jamii bamaga
 
Njie watu mmezidi na matangazo yenu ya hizo kamari zenu. Kwa siku napokea kama dozi, asbh,mchana na jioni hala sio sms moja mnazituma kama kukomoa mnatujazia inbox tu!

Haipiti masaa mawili sms sita mpaka kumi! Tumewachoka bnaaa
 
Kuna wizi mkubwa kwa fedha za salio za wateja unaoendelea sasa hivi katika mtandao wa Vodacom.
Kwa vile hili si jungu bali ukweli nimisha report wizi huo katika kitengo cha malalamiko TCRA kwa hatua zaidi.

Nimeweka salio la Tsha 10,000 mchana wa leo kwa Mpesa ref Y23SY687 na baada ya muda mfupi nikakuta salio langu la maongezi ni sifuri.

Nikanunua vocha na kutumiwa tshs 10,000 na hela yote imekatwa tena.

Wateja wa Vodacom jihadharini, kuna mwizi kaingia mtandaoni Vodacom

UPDATE
=====
VODACOM wamefanya ustaarabu wa kunipigia baada ya kuona detail ya transaction hapo juu, na kuiona kwenye mtandao wa Jamiiforums.
Kimsingi wameapologise kwa mtafaruku uliotokea lakini wamenieleza nifike ofisini kwao kuona aian ya simu ninyotumia isije ikawa data apps ziko wazi.
Na kweli baada ya maongezi ya kuchunguza, mobile data setting ilikuwa ON, na mimeizima sasa.

Hata hivyo ni vema nitaenda kupata maelezo ya kuyeyuka kwa salio langu , karibu 20,000, kwa siku moja.
Wanabodi mtajulishwa inawezekana kuna wenye tatizo kama langu.

UPDATE
=====
Nimeonana na waheshimiwa sana wa Customer Care pale Block 4 Mlimani City.
Cha kusikitisha ni wao kushindwa kuchukua malalamiko yangu na kuyafanyia kazi, na hii ni licha ya kuwaelewesha kuwa hili tukio nalijawahi kunitokea na hii kuwa ni mara ya kwanza.

Hawa jamaa wa Customer Care ni kama mabalozi waliopewa jukumu la kusafisha kampuni ya VODACOM hata kama inanuka kwa wizi uliodhahiri.
Kitu ambacho hawajui ni kuwa nilifanya due diligence kupitia wafanyakazi ndani ya VODACOM walionidhihirishia kuwa kuna wafanyakazi wasio waaminifu ambao wana access na personal security settings za wateja.

Na wafanyakazi hao huwa "wapiga kishenzi" fedha za wateja.

Kwa kifupi mtu wa Customer Care ameshindwa kuniconvince na maelezo yake ya upotevu wa Tshs 20,000 katika mtandao wa VODACOM.


Vodacom sijui tuseme ni wizi au namna gani swala la kupotea masalio ya watu limekua jambo la kawaida sana

Mimi leo na jana nimenunua salio ili nijiunge wananiambia salio langu halitoshi kujiunga na kifurushi cha ajabu nikiangalia salio lipo vilevile na kama mnavyojua mtu ukikaa na salio bila kujiunga litaisha bila taarifa

Vodacom you have to change maana hata baada ya kutatuliwa hizi shida hturudishiwi masalio yetu

Muda mwingine tunanua vocha tukiwa hna hali ngumu yaani ikitokea tumepoteza pesa kijinga tunaumia sana
 
43 Reactions
Reply
Back
Top Bottom