Vodacom Tanzania ndio mtandao wenye gharama kubwa Tanzania

Attachments

  • 1466943803838.jpg
    1466943803838.jpg
    40.6 KB · Views: 37
Najua kuwa naibiwa. Ndio maana nikasema sio voda peke yao wanaotoa mb 500. Hata tigo ni hivyo hivyo. Huenda wapo wa voda wanaopewa gb 1 ila wewe unapewa mb 500. Au bado hujapata point
Aiseee wote MAJIPU
 
Hivi zantel bado ipo??
Zantel ipo kinadharia kuliko kiuhalisia.. Zantel ni Tigo.... Kuanzia mwezi wa 12 wateja wa zantel watafaidi network ya tigo kama wanavyofaidi tigo wenyewe...

Kwa kifupi MIC ni mmiliki halali wa zantel waliuziwa na ETISALAT.
 
si tetei Vodacom lakini kama unataka kusema wao ni ghali kuliko wengine walau ungepitia huduma zote wanazozitoa mathalani mobile money, voice, etc kama kote huko wapo ghali ndio uje na conclussion hiyo hapo vinginevyo hujawatendea haki Voda na wala hujaitendea haki taaluma yako kama Great thinker
ucjilazmishe kutokukubali.... voda wako juu sana. acha ubish kwenye seriuz ishu
 
Ni ukweli Voda wapo juu sana gharama zao,ila Makato yao kwenye miamala ni nafuu kuliko mitandao mingine na pia Internet yao ipo kasi sana kuliko mitandao mingine!!,Hapo huwa wananipoza na machungu ya gharama zao kua juu!!!
 
Watanzania wenzangu ninachoandika hapa ni ukweli kabisa, Vodacom gharama zao ni Jipu ,maana si kwenye vifurushi vya data,kupiga simu ,sms au makato ya miamala ya huduma za kifedha, hawa jamaa ni hatari,
Mfano mzuri ni huu,
Airtel kwa Tsh 1000 =GB1
Zantel kwa 1000=GB 1
Tigo kwa Tsh 999=GB 1
Ila Voda Tsh 1000=MB 500
huu MTANDAO una GHARAMA za juu sana hapa nchini na sielewi kwanini !! Mpaka najiuliza
(i)Wanalipa KODI KUBWA kuliko wenzao?
(ii)Wametumwa Pesa?
(iii)Wanajua watanzania wote matajiri ?
(iv)Wanafanya makusudi ?

Kama kuna mtu anangangana na hawa WEZI mim namdharau sana
 
Ni ukweli Voda wapo juu sana gharama zao,ila Makato yao kwenye miamala ni nafuu kuliko mitandao mingine na pia Internet yao ipo kasi sana kuliko mitandao mingine!!,Hapo huwa wananipoza na machungu ya gharama zao kua juu!!!
Hko kwenye miamala ndyo balaa xx
 
Wapo ghali ila pia quality ya huduma zao pia ni nzuri.. Internet iko stable zaidi tofauti na mitandao mingine.. Dabo bando kwa mfani napata 2 gb of very fast internet..
 
Back
Top Bottom