Vodacom sasa hii imezidi, tunaomba msitishe huu ujumbe wenu ambao unachukua zaidi ya sekunde kumi kuhusu uhakiki wa namba

Mromboo

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,497
2,000
Wanajukwaa jumapili njema,

Hivi hii kitu vodacoma wameleta wakati mtu unapiga simu kwenda voda mnaionaje? Wameshindwa kutuma ujumbe mmoja kwa kila mteja waache kutupigia kelele kila tunapotaka kupiga simu?

Inafikia kiwango mpaka sasa mtu unaona tabu kupiga simu. Muda mwingine unapiga unaweka chini usubirie sekunde kumi ziishe ndo uweke simu sikioni.

Kiukweli kwangu mm hiki kitu ni kero sana kiasi kwamba natamani hata niwe natuma tu ujumbe badala ya kupiga simu. Vodacom tuoneeni huruma wateja wenu msitishe hiki kitu.
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
3,885
2,000
Vodacom walishajikokea ile kitambo kutoa huduma, wanatafuta akselereta ya spidi ya kufukuzwa waende huko SA & London
 

Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
43,870
2,000
Uhakiki wa namba for what na mimi nimeshasajili kila kitu, wanakera sana
 

mic69

Member
Dec 23, 2016
95
150
Hili Jambo ukweli Lina udhi sana ,sijui wanakwama wapi? Tulishapewa miongozo ya kusajili laini na kuzihakiki Sasa sijui wanawashwa na Nini na hii mi kelele
 

reyzzap

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,500
2,000
Mimi kero yangu ipo kwenye msg.
Asubuhii naamshwa na
M-Pawa, sijatulia
Songesha,
Jimixie,
Vodacom Ofa,
Polisi,
Utapeli,
Double Data,

Vodacom wanaweza wazidi hata mchepuko kwa msg zao.
 

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
4,608
2,000
Kila nilipiga Simu yule mdada anaanza kusema nibadili namba kwenda 4g sijui nitapata ofa ya GB ngapi anakera Sana aiseee
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom