Vodacom Premier League: Yanga SC 0 Vs 1 Azam FC

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
ILEE, Patashika ya ligi kuu Tanzania kuendelea kupigwa leo January 18, 2020, ambapo Azam FC Wanalamba lamba, wakiwa na alama 29 kwa michezo 14, wanawakaribisha Yanga SC Wanajangwani, wenye alama 25 kwa michezo 13, kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na ushindani mkubwa kwa muda wote wa dakika 90' hasa ukizingatia timu hizi muda sasa zimekuwa wakipokezana katika kushinda na vilevile kupokezana katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania.

Katika michezo mitano ya mwisho ambayo wamekutana, Yanga imeshinda michezo mitatu huku Azam FC ikishinda michezo miwili.

Na katika michezo ya mwisho ya ligi hii ya VPL, Azam FC walishinda mchezo wao wa mwisho mabao 2-0 dhidi ya Lipuli huku Yanga wakifungwa mchezo wao wa mwisho kwa kalamu ya mabao 3-0 dhidi Kagera Sugar.

Kazi Ipo Leo..Nani kuibuka na ushindi hii leo Azam FC au Yanga SC? Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1:00 usiku, Usikose Ukaambiwa.

••Kikosi cha Azam FC Kinachoanza:
Razak, Wadada, Kangwa, Amoah, Masai Raphael, Mahundi, Abubakar (c), Chilunda, Chirwa, Suleiman.

••Kikosi cha Yanga SC kinachoanza:
Shikalo, Abdul, Jaffar, Lamine, Mtoni, Tshishimbi (c), Kaseke, Niyonzima, Balama, Molinga, Sibomana.

••••••================••••

Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara VPL' kati ya Azam FC dhidi ya Yanga African umemalizika Uwanja wa Taifa ambapo Yanga wamepokea kichapo cha pili mfululizo kwa kufungwa bao moja bila, likiwa ni bao la kujifunga kwa beki Ally Mtoni katika dakika ya 25 za mchezo.

FT: Azam FC 1-0 Yanga African

FB_IMG_1579343420941.jpeg
 
Back
Top Bottom