Vodacom Premier League VPL | Uwanja wa Taifa: Yanga SC 0 - 0 Azam FC

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,228
Mechi hii itarushwa moja kwa moja na Azam Sport 2 mida ya saa kumi jioni,Ni mechi muhimu sana kwa timu zote mbili,Azam akitaka kubaki nafasi ya pili na Yanga pia akipigania kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu.

Utabiri wako unasemaje
20200621_120855.jpeg
 
Naaaam patashika ya Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League (VPL ), kuendelea kuvurumishwa leo Juni 21, 2020 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo Yanga SC watapapatuana na Azam FC.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa mkali na kusisimua kwa muda wote wa mchezo huku kila timu ikijinasibu kuibuka na ushindi, ambapo Yanga SC ipo nafasi ya tatu kwa alama 55 ikiwa imecheza michezo 29 huku Azam FC ikishika nafasi ya pili kwa alama 57 kwa michezo 29.

Timu hizi zimekutana mara 26, Yanga SC wameshinda mara 10 huku Azam FC wakishinda mara 8 na kutoka sare mara 8, ambapo katika michezo hiyo Yanga wamefunga magoli 33 huku Azam FC wakiwa wamekifunga magoli 30.

Je nani kuibuka na ushindi na kukusanya alama 3 leo ili kuweza kumsogelea kinara wa VPL, Simba SC mwenye alama 75?

Shughuli yote pevu ni kuanzia saa 10: 00 jioni..Usikose Ukaambiwa.

=================

Update;

Katika mchezo wa VPL, Yanga SC na Azam FC uliochezwa uwanja wa Taifa, leo Juni 21, 2020 timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana

FT, VPL Yanga SC 0-0 Azam FC

FB_IMG_1592729554788.jpg
 
Naaaam patashika ya Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League (VPL ), kuendelea kuvurumishwa leo Juni 21, 2020 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo Yanga SC watapapatuana na Azam FC.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa mkali na kusisimua kwa muda wote wa mchezo huku kila timu ikijinasibu kuibuka na ushindi, ambapo Yanga SC ipo nafasi ya tatu kwa alama 55 ikiwa imecheza michezo 29 huku Azam FC ikishika alama 57 kwa michezo 29.

Timu hizi zimekutana mara 26, Yanga SC wameshinda mara 10 huku Azam FC wakishinda mara 8 na kutoka sare mara 8, ambapo katika michezo hiyo Yanga wamefunga magoli 33 huku Azam FC wakiwa wamekifunga magoli 30.

Je nani kuibuka na ushindi na kukusanya alama 3 leo ili kuweza kumsogelea kinara wa VPL, Simba SC mwenye alama 75?

Shughuli yote pevu ni kuanzia saa 10: 00 jioni..Usikose Ukaambiwa.View attachment 1485009
Tuko kwenye kampeni ya:
NO UTOPOLO FC KTK CAF COMPETITONS...
 
Back
Top Bottom