Vodacom Premier League 'VPL' Simba SC dhidi ya Namungo FC, Kazi Ipo Uwanja wa Taifa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Hello Hello...!
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania kuendelea kutimua vumbi leo Jumatano ya January 29, 2020 ambapo Mabingwa wa Nchi Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, vinara wa VPL wakiwa na alama 41 kwa michezo 16, wanawakaribisha Namungo FC, wenye alama 28 kwa michezo 15, mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani na mgumu kwa pande zote kutokana na kuwa mara ya kwanza kukutana kwenye mashindano ya Ligi Kuu tangu Namungo FC kupanda daraja msimu huu wa mwaka 2019/2020.

Kocha wa Simba SC Sven Vanderbroeck, amesema kikosi chake kina maandalizi ya kutosha ya kuweza kupata matokeo ya ushindi wa kuweza kukusanya alama tatu muhimu ili kujikita zaidi kwenye msimamo wa VPL

Kocha wa Namungo FC, Hitamana Thierry, amesema wamejiandaa vizuri kwa lengo la kupata ushindi ili kusogea juu kwenye msimamo wa VPL huku akiongeza kuwa Simba ni timu kubwa na wanaiheshimu lakini amewapa maelekezo wachezaji wake mbinu ya kuidhibiti Simba ili kupata ushindi bila wasiwasi wowote.

Kazi Ipo..Nani kuibuka mbabe? Dakika 90 zitaamua hii patashika..Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1: 00 usiku, Usikose Ukaambiwa.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana


Vikosi vinavyoanza leo, angalia post # 31 Simba SC dhidi ya Namungo FC...

•••••============••••

Timu ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya Namungo FC kwenye mfululizo wa Ligi Kuu

Mabao ya Simba yamewekwa kimiani na Kahata 21' Dilunga 39' Kagere 89' huku yale ya Namungo yakifungwa na Birigimana na Kikoti

Kwa matokeo hayo Simba imezidi kujiimarisha kileleni kwa alama 44 kwa michezo 17.

VPL, FT; Simba SC 3-2 Namungo FC

FB_IMG_1580292361062.jpeg
IMG_20200129_125546_043.jpeg
 
Kwani nimesema nina timu Ses. Mi sina timu leo hapo mana hata hao Namungo anayewapa kiburi si 5imba mwenzenu? #PM

Sina timu leo hapo.
Hapo sawa, bora ukawa huna timu kuliko kua Namungo. Yes PM ni Lunyasi mwenzetu japo Namungo ni vijana wake leo itabidi atusamehe tu, tunatoroka na point tatu safi
 
Back
Top Bottom