Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Vodacom Premier League VPL kuendelea kutimua vumbi leo February 1, 2020 kusaka alama tatu muhimu, ambapo Vinara wa Ligi Wekundu wa Msimbazi, Mnyama Mkali, Simba SC, kuwakaribisha Wagosi wa Kaya, Coastal Union kutoka Tanga, ambao wapo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi, mchezo utakaopigwa kunako Uwanja wa Taifa.
Patashika ya leo inatarajiwa kuwa ya aina yake huku Wekundu wa Msimbazi wakijivunia rekodi bora dhidi ya Wagosi wa Kaya hasa kumbukumbu ya msimu uliopita, ambapo Simba SC walitembeza kichapo kikali cha bakora 8-1 dhidi ya Coastal Union.
Kocha wa Simba, Sven Vanderbroeck amesema wachezaji wake wamejiandaa vya kutosha kuelekea mchezo huo, huku akikiri mapungufu yanayojitokeza siku za hivi karibuni hasa sehemu ya ulinzi kutokana na kuruhusu mabao mfululizo na kwa kauli hiyo wadau wanasema huenda kukawa na mabadiliko kwenye eneo la ulinzi.
Naye Kocha wa Coastal Juma Mgunda amesema kuwa kwa upande wao wamejiandaa kushinda mchezo wa leo licha ya kwamba mchezo utakuwa mgumu huku akitanabaisha kuwa wao kama Coastal hawaangalii yaliyopita, wanaangalia yaliyo mbele yao.
Je? Mnyama ataendelea kukusanya vitambulisho vya ushindi? Au Mgosi atakataa? dakika 90 kuamua..Soka Kabambe Uwanja wa Taifa kuanzia saa 10: 00 jioni, USIKOSE UKAAMBIWA.
Line Up Itakujia Hivi Punde.....!