Vodacom Premier League (VPL) Ruvu Shooting vs Simba SC Uwanja wa Uhuru, show ya hatari

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,415
2,000
Salaam Tanzania na duniani kote!

Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayojulikana kama Vodacom Premier League (VPL), Kuendelea kushika kasi katika viwanja tofauti ambapo kwenye dimba la CCM Kirumba Mbao FC wanawakaribisha Azam FC huku gumzo kubwa likiwa katika uwanja wa Uhuru kwa Ruvu Shooting kupepetana na Simba SC, Mnyama Mkali Mwituni.

Mchezo huo utarajiwa kuwa mkali na wakusisimua kwa muda wote wa dakika tishini ambapo Ruvu Shooting wakitaka kuendeleza rekodi ya kuzifunga timu zote nne za VPL ambazo ziliwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kimataifa, yaani Simba SC, Yanga SC, Azam FC na KMC FC, huku kwa upande wao Simba SC wakizisaka alama tatu muhimu ili kuweza kuweka matumaini ya kutetea tena Ubingwa.

Kulitaka mwana, kulipewa mwana

Wanasimba na mdau wa kabumbu popote ulipo shuhudia hii Show ya Hatari kuanzia saa 10: 00 jioni kutoka kwa Simba SC, ya nguvu moja yenye viwango vilivyowekwa bayana na CAF. Usikose Ukaambiwa!

FB_IMG_1574507745881.jpeg
IMG_20191123_141823_878.jpeg

Kutoka Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, mpambano wa VPL umemalizika kwa Simba SC, kuchomoza na ushindi wa mabao matatu bila majibu dhidi ya Ruvu Shooting.

Mabao ya Simba yamewekwa kimiani na Miraji Athumani akifunga mawili 40' 74' na mlinzi wa kati Tairone Santos 46

FT: Ruvu Shooting 0-3 Simba SC

Ghazwattttttttttttt
 

mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
3,150
2,000
Mmiliki wa Uwanja wa Uhuru aone AIBU inakuwaje gemu inaruka Kimataifa kupitia TV halafu uwanja mweusiiiiii kwenye majukwaaa yamejaa Fungus kama stoo ya mkaa. Vitu vingine havihitaji kutumbuliwa au kuambiwa na Mhe.Rais ndio tuvifanye
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom