Vodacom Premier League 'VPL' Mwadui FC yaituliza Simba SC kwa kuichapa kwa goli 1 - 0

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League VPL inatarajia kurindima leo kunako dimba la Kambarage Shinyanga ambapo wenyeji Mwadui FC, wanawakaribisha Mabingwa wa Nchi Simba SC, Mnyama Mkali Mwituni.

Mchezo unakuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika tisini hasa ukizingatia Simba SC wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa na lengo moja tu la kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo katika VPL

Simba ndo timu pekee ambayo haizapoteza mchezo wowote huku safu ya ushambuliaji ikiongozwa na MK 14 Maddie Kagere ikiwa ni moto wa kuotea mbali kwa timu nyingine. Je Mwadui ataweza kumzuia Mnyama au Mnyama ataendelea kujikita mawinguni?

Usikose Ukaambiwa soka hili la Mwana Kulitaka Kulipewa ...kuanzia saa 10:00 jioni.View attachment 1248980
IMG_20191030_143938_787.jpeg
 
Naaaaaaaaaaaaaaam mpira umeanza uwanja wa Kambarage VPL

Mwadui FC 0-0 Simba SC
 
10' Timu zimeanza kwa mashambulizi kwa pande zote mbili huku Mwadui wakipata kona 2 ambazo hazikuzaa matunda

Mwadui FC 0-0 Simba SC
 
15' bado milango ni migumu, mpira sasa ukiwa ni kurusha kuelekea Simba SC lakini mabeki wanaokoa kwa Shiboub...Mpira Unatoka nje..!
 
27' Kuanzia dakika ya 25 mpaka 27 Simba wamepeleka mashambulizi makali lango la Mwadui FC, sifa kwao mabeki wa Mwadui kwa kutibua plani ya Simba..Hata hivyo bado lango ni gumu

Mwadui FC 0-0 Simba SC
 
32' Goooal goooooal Mwadui FC wanapata bao la kuongoza likifungwa na Gerard Mathis

Mwadui FC 1-0 Simba SC
 
Back
Top Bottom