Vodacom pia walipanda kizimbani kutoa ushahidi dhidi ya Sabaya katika kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili

Kwa nini unalazimisha wengine wa kubaliane na wewe?? Simama mwenyewe. Usitufokee
 
Shida ni kwamba kesi ya Mbowe ipo wazi kabisa kwamba ni ya kutengenezwa kulingana lakini ya Sabaya 100% bila hata ushahidi you can tell kwamba the guy alikua muuaji na muhujumu uchumi na gaidiai

Shida ni kwamba kesi ya Mbowe ipo wazi kabisa kwamba ni ya kutengenezwa kulingana lakini ya Sabaya 100% bila hata ushahidi you can tell kwamba the guy alikua muuaji na muhujumu uchumi na gaidi
Akili zile zile za chadema..wewe umeshasikia Sabaya kamuuwa na nani...hakuna sheria inaelekeza eti kwasababu yule anachukiwa na nyumbu ndio taarifa zake ziwekwe wazi na mitandao..ndio unachojaribu kuaminisha watu ila kwa maneno tofauti.Sheria inatoa haki sawa kwa mtu yeyote anayepelelezwa taarifa apewe officer wa police anayechunguzwa mtuhumiwa.

Na mbowe bora afungwe tu maana ushahidi wa jamhuru umeenyooka sana Kuliko hata ule wa Sabaya wa kuunga unga naa gundi. Kama hii kesi ni ya uwongo niamini kesi ya namna gani. Technologia aidanganyi bhana

Mnasumbua tu mahakana
 
Akili zile zile za chadema..wewe umeshasikia Sabaya kamuuwa na nani...hakuna sheria inaelekeza eti kwasababu yule anachukiwa na nyumbu ndio taarifa zake ziwekwe wazi na mitandao..ndio unachojaribu kuaminisha watu ila kwa maneno tofauti.Sheria inatoa haki sawa kwa mtu yeyote anayepelelezwa taarifa apewe officer wa police anayechunguzwa mtuhumiwa.

Na mbowe bora afungwe tu maana ushahidi wa jamhuru umeenyooka sana Kuliko hata ule wa Sabaya wa kuunga unga naa gundi. Kama hii kesi ni ya uwongo niamini kesi ya namna gani. Technologia aidanganyi bhana

Mnasumbua tu mahakana
Umeandika kwa hisia sana mkuu, naheshimu maoni yako na naamini yapo sahihi kulingana na perceptions zako, kwenye nyuzi kama hizi ni vizuri tu ukajifunza kuheshimu mawazo ya wengine hata kama yanapingana na kile unachokimini mwisho wa siku mahakama ndio mwamuzi wa mwisho kwenye hili suala, kwa hiyo tujipe muda 🤝
 
Tuletee mahojiano kamili wakati anaongozwa kutoa ushahidi wake...
Ulichoambatanisha hakitoi taarifa za kina. Unazidi kuifanya Vodacom ionekane ni bora kuliko tiGo.
 
Hapo vip!

Katika kesi ya Sabaya vodocom walipanda kizimbani kutoa ushahidi dhidi ya Sabaya ila huu upande ambao kwa sasa hivi wanailalamikia TIGO kutoa ushahidi dhidi ya kesi ya Mbowe waliona sawa na walikaaa kimya.

Ninachokiona kuna ushabiki mkubwa wa kisiasa katika hizi kesi..nakuna vikundi vya watu unajaribu kupeleka pressure kwenye chombo cha kutoa haki ili iyamue shauri kulingana na matakwa yao.

Kuna upande wao wanajiona wapo sawa na nimalaika wakamilifu wasio kosea ila wao wanahaki ya kumtuhumu mtu mwingine hata kwa hila.

Nchi ikifikia hapa yakwamba kunawatu wanaweza kushinikiza vyombo mbalimbali ndani ya nchi hii ifanye maamuzi kwa maslahi yao ni hatari sana.

----
Meneja wa ulinzi na mshirika katika vyombo vya ulinzi na usalama Vodacom PLC makao makuu, James Wawenje emepanda kizimbani leo kutoa ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Hai, Lengai ole Sabaya na wenzake sita.

Shahidi huyo wa sita wa Jamuhuri akitoa ushahi wake mbele ya hakimu mkazi wa Mahakama ya Arusha, Patricia Kisinda amesema idara yake ndiyo inahusika na mfumo wa kunakili kumbukumbu za kupiga na kupokea simu na kunakili ujumbe wa simu.

Akiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Ofmed Mtenga amesema idara yake pia ndiyo inahusika na kunakili kumbukumbu za kutuma na kupokea miamala.

Amesema amekuwa mwajiriwa wa Vodacom tangu Agosti 25, 2015 ma ana shahada uzamili masuala ya utawala katika ulinzi aliyoipata nchini Uingereza.

Amesema katika majukumu yake wateja wake wakubwa ni Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), mahakama na taasisi zingine kama Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mamlaka ya Mapato (TRA) na tume za ushindani.

Wawenje ameileza mahakama kuwa amekuwa akishirikiana kutoa taarifa za uchunguzi kwa mujibu wa sheria.

Kusimamia ulinzi na mali za kampuni na kishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kutoa nyaraka zinapohitajika kwa mujibu wa sheria.

Katika shauri hilo la uhujumu uchumi namba 27, 2021 washitakiwa wengine ni Enock Mnkeni, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na makosa matano la kwanza ambalo ni kuongoza genge la uhalifu na kosa la tano ambalo ni utakatishaji fedha linawakabili washitakiwa wote saba wanadaiwa kupata Sh90 milioni huku wakijua kupokea fedha hizo ni zao la kosa la vitendo vya rushwa.

Kosa la pili, tatu na nne Sabaya peke yake ameshitakiwa kwa makosa ya kujihusisha na rushwa ambapo anadaiwa kuchukua Sh90 milioni matumizi mabaya ya ofisi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.

Watuhumiwa hao wanatetewa na mawakili Moses Mahuna, Fauzia Mustapha, Edmund Ngemela na Fridolin Gwemelo.

Katika shauri hilo Jamuhuri inawakilishwa na wakili mwandamizi Ofmed mtenga na Felix Kwitukia na Wakili Neema Mbwana.
Shahidi huyo anaendelea kutoa ushahidi wake.

Soma gazeti la Mwananchi na mitandao yake kwa habari zaidi kujua amesema nini kuhusu Sabaya.

Chanzo: Mwananchi
Unawezaje kumlinganisha jambazi aliye tumia vibaya madaraka yake na kiongozi wa upinzani ambaye anabambikiwa kesi kisiasa!? Kwenye kesi ya Mbowe, kuna uhalifu gani ambao walalamikaji wameuonesha zaidi ya kusema alituma laki 5 kupitia Tigo? Hata Mimi nilituma milioni na laki 5 kwa mtu kupitia M Pesa jana, na siyo kosa!
 
Back
Top Bottom