Vodacom pia walipanda kizimbani kutoa ushahidi dhidi ya Sabaya katika kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Oct 23, 2016
2,050
3,658
Hapo vip!

Katika kesi ya Sabaya vodocom walipanda kizimbani kutoa ushahidi dhidi ya Sabaya ila huu upande ambao kwa sasa hivi wanailalamikia TIGO kutoa ushahidi dhidi ya kesi ya Mbowe waliona sawa na walikaaa kimya.

Ninachokiona kuna ushabiki mkubwa wa kisiasa katika hizi kesi..nakuna vikundi vya watu unajaribu kupeleka pressure kwenye chombo cha kutoa haki ili iyamue shauri kulingana na matakwa yao.

Kuna upande wao wanajiona wapo sawa na nimalaika wakamilifu wasio kosea ila wao wanahaki ya kumtuhumu mtu mwingine hata kwa hila.

Nchi ikifikia hapa yakwamba kunawatu wanaweza kushinikiza vyombo mbalimbali ndani ya nchi hii ifanye maamuzi kwa maslahi yao ni hatari sana.

----
Meneja wa ulinzi na mshirika katika vyombo vya ulinzi na usalama Vodacom PLC makao makuu, James Wawenje emepanda kizimbani leo kutoa ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Hai, Lengai ole Sabaya na wenzake sita.

Shahidi huyo wa sita wa Jamuhuri akitoa ushahi wake mbele ya hakimu mkazi wa Mahakama ya Arusha, Patricia Kisinda amesema idara yake ndiyo inahusika na mfumo wa kunakili kumbukumbu za kupiga na kupokea simu na kunakili ujumbe wa simu.

Akiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Ofmed Mtenga amesema idara yake pia ndiyo inahusika na kunakili kumbukumbu za kutuma na kupokea miamala.

Amesema amekuwa mwajiriwa wa Vodacom tangu Agosti 25, 2015 ma ana shahada uzamili masuala ya utawala katika ulinzi aliyoipata nchini Uingereza.

Amesema katika majukumu yake wateja wake wakubwa ni Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), mahakama na taasisi zingine kama Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mamlaka ya Mapato (TRA) na tume za ushindani.

Wawenje ameileza mahakama kuwa amekuwa akishirikiana kutoa taarifa za uchunguzi kwa mujibu wa sheria.

Kusimamia ulinzi na mali za kampuni na kishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kutoa nyaraka zinapohitajika kwa mujibu wa sheria.

Katika shauri hilo la uhujumu uchumi namba 27, 2021 washitakiwa wengine ni Enock Mnkeni, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na makosa matano la kwanza ambalo ni kuongoza genge la uhalifu na kosa la tano ambalo ni utakatishaji fedha linawakabili washitakiwa wote saba wanadaiwa kupata Sh90 milioni huku wakijua kupokea fedha hizo ni zao la kosa la vitendo vya rushwa.

Kosa la pili, tatu na nne Sabaya peke yake ameshitakiwa kwa makosa ya kujihusisha na rushwa ambapo anadaiwa kuchukua Sh90 milioni matumizi mabaya ya ofisi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.

Watuhumiwa hao wanatetewa na mawakili Moses Mahuna, Fauzia Mustapha, Edmund Ngemela na Fridolin Gwemelo.

Katika shauri hilo Jamuhuri inawakilishwa na wakili mwandamizi Ofmed mtenga na Felix Kwitukia na Wakili Neema Mbwana.
Shahidi huyo anaendelea kutoa ushahidi wake.

Soma gazeti la Mwananchi na mitandao yake kwa habari zaidi kujua amesema nini kuhusu Sabaya.

Chanzo: Mwananchi
 
Labda umesahau watu walivyoishutumu hiyo kampuninkiasi cha kuwa na kampeni ya kususia bidhaa zao. Jambo hilo halikubaliki bila kujali ni kampuni gani inasaidia kuvunja katiba na haki za faragha ya watu.
 
Mkuu usiwaze sana. Hilo ni genge la watu 60 tu hapa mtandaoni, kati ya watu milioni 60 hapa nchini. Ndio maana kelele unazoziona hapa mtandaoni, huku mtaani hazipo kabisa, kila mtu anaendelea na shughuli zake kuitafutia mahitaji familia yake.

Inajulikana wazi kuwa kati ya hao watu 60, 40 wanalipwa kutetea uovu dhidi ya mahakama, na 20 ni bendera fuata upepo ambao hawajui kuwa kuna wenzao wanalipwa kwa kazi hiyo.

Hata hivyo zote ni kelele za vyura ambazo haziwezi kumzuia ng'ombe kunywa maji.

Mahakama itafanya kazi yake kwa mujibu wa sheria na sio kwa mujibu wa kelele zao. Japo wengi wao wana ID tano tano mpaka kumi kumi lkn hiyo haiwezi kuwa sababu ya kuzuia sheria kufanya kazi yake.
 
Mkuu usiwaze sana. Hilo ni genge la watu 60 tu hapa mtandaoni, kati ya watu milioni 60 hapa nchini. Inajulikana wazi kuwa kati ya hao watu 60, 40 wanalipwa kutetea uovu dhidi ya mahakama, na 20 ni bendera fuata upepo ambao hawajui kuwa kuna wenzao wanalipwa kwa kazi hiyo. Hata hivyo zote ni kelele za vyura ambazo haziwezi kumzuia ng'ombe kunywa maji. Mahakama itafanya kazi yake kwa mujibu wa sheria na sio kwa mujibu wa kelele zao. Japo wengi wao wana ID tano tano mpaka kumi kumi lkn hiyo haiwezi kuwa sababu ya kuzuia sheria kufanya kazi yake.
Well noted!
 
Hapo vip!!
Katika kesi ya Sabaya vodocom walipanda kizimbani kutoa ushahidi dhidi ya Sabaya ila huu upande ambao kwa sasa hivi wanailalamikia TIGO kutoa ushahidi dhidi ya kesi ya Mbowe waliona sawa na walikaaa kimya.

Ninachokiona kuna ushabiki mkubwa wa kisiasa katika hizi kesi..nakuna vikundi vya watu unajaribu kupeleka pressure kwenye chombo cha kutoa haki ili iyamue shauri kulingana na matakwa yao.

Kuna upande wao wanajiona wapo sawa na nimalaika wakamilifu wasio kosea ila wao wanahaki ya kumtuhumu mtu mwingine hata kwa hila.

Nchi ikifikia hapa yakwamba kunawatu wanaweza kushinikiza vyombo mbalimbali ndani ya nchi hii ifanye maamuzi kwa maslahi yao ni hatari sana.

----
Meneja wa ulinzi na mshirika katika vyombo vya ulinzi na usalama Vodacom PLC makao makuu, James Wawenje emepanda kizimbani leo kutoa ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Hai, Lengai ole Sabaya na wenzake sita.

Shahidi huyo wa sita wa Jamuhuri akitoa ushahi wake mbele ya hakimu mkazi wa Mahakama ya Arusha, Patricia Kisinda amesema idara yake ndiyo inahusika na mfumo wa kunakili kumbukumbu za kupiga na kupokea simu na kunakili ujumbe wa simu.

Akiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Ofmed Mtenga amesema idara yake pia ndiyo inahusika na kunakili kumbukumbu za kutuma na kupokea miamala.

Amesema amekuwa mwajiriwa wa Vodacom tangu Agosti 25, 2015 ma ana shahada uzamili masuala ya utawala katika ulinzi aliyoipata nchini Uingereza.

Amesema katika majukumu yake wateja wake wakubwa ni Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), mahakama na taasisi zingine kama Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mamlaka ya Mapato (TRA) na tume za ushindani.

Wawenje ameileza mahakama kuwa amekuwa akishirikiana kutoa taarifa za uchunguzi kwa mujibu wa sheria.

Kusimamia ulinzi na mali za kampuni na kishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kutoa nyaraka zinapohitajika kwa mujibu wa sheria.

Katika shauri hilo la uhujumu uchumi namba 27, 2021 washitakiwa wengine ni Enock Mnkeni, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na makosa matano la kwanza ambalo ni kuongoza genge la uhalifu na kosa la tano ambalo ni utakatishaji fedha linawakabili washitakiwa wote saba wanadaiwa kupata Sh90 milioni huku wakijua kupokea fedha hizo ni zao la kosa la vitendo vya rushwa.

Kosa la pili, tatu na nne Sabaya peke yake ameshitakiwa kwa makosa ya kujihusisha na rushwa ambapo anadaiwa kuchukua Sh90 milioni matumizi mabaya ya ofisi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.

Watuhumiwa hao wanatetewa na mawakili Moses Mahuna, Fauzia Mustapha, Edmund Ngemela na Fridolin Gwemelo.

Katika shauri hilo Jamuhuri inawakilishwa na wakili mwandamizi Ofmed mtenga na Felix Kwitukia na Wakili Neema Mbwana.
Shahidi huyo anaendelea kutoa ushahidi wake.

Soma gazeti la Mwananchi na mitandao yake kwa habari zaidi kujua amesema nini kuhusu Sabaya.

Chanzo: Mwananchi
Wewe hujakatazwa kuwasema hao voda wala hujalazimishwa kuilamu tigo.

Hivyo hivyo huna mamlaka ya kuwalaumu wanaotoa mawazo yao maana hili ni jukwaa huru.
 
Mkuu usiwaze sana. Hilo ni genge la watu 60 tu hapa mtandaoni, kati ya watu milioni 60 hapa nchini. Ndio maana kelele unazoziona hapa mtandaoni, huku mtaani hazipo kabisa, kila mtu anaendelea na shughuli zake kuitafutia mahitaji familia yake.

Inajulikana wazi kuwa kati ya hao watu 60, 40 wanalipwa kutetea uovu dhidi ya mahakama, na 20 ni bendera fuata upepo ambao hawajui kuwa kuna wenzao wanalipwa kwa kazi hiyo.

Hata hivyo zote ni kelele za vyura ambazo haziwezi kumzuia ng'ombe kunywa maji.

Mahakama itafanya kazi yake kwa mujibu wa sheria na sio kwa mujibu wa kelele zao. Japo wengi wao wana ID tano tano mpaka kumi kumi lkn hiyo haiwezi kuwa sababu ya kuzuia sheria kufanya kazi yake.
Endelea kujidanganya kisa shemeji yako anaye kulisha anafanya kazi tigo
 
Labda umesahau watu walivyoishutumu hiyo kampuninkiasi cha kuwa na kampeni ya kususia bidhaa zao. Jambo hilo halikubaliki bila kujali ni kampuni gani inasaidia kuvunja katiba na haki za faragha ya watu.
Nani na nani waliendesha hiyo kampeni mkuu?maana ushahidi umetolewa just two weeks ago na sijaona hiyo kampeni ya kususia vodacom.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom