Vodacom njooni hapa mnipe msaada wa haraka

iCode

JF-Expert Member
Oct 16, 2013
757
438
Wakuu nina imani kuwa mu wazima kiafya..

Katika safari zangu za hapa na pale nimekutana na hali ngumu sana.. Nimekuja Mwanza kumleta mdogo wangu shule...

Fedha zangu nilihamishia M-Pesa for easy access. Baada ya kumaliza issues ziluzonileta jioni hii nilienda kutoa pesa M-Pesa ili nikate tiketi ya kurudi Arusha.... Nilipofika kwa Wakala nikatajiwa namba ambayo baadae jina lililokuja alisema sio lake... Maana yake nilikosea namba ya wakala.. Nilipiga simu Vd wakaniambia nisubiri siku 7...
(alisisitiza mno)

Hapo nilichanganyikiwa kabisa....
Naombeni staff wa vodacom waliopo humu wanisaidie kwa sababu sina namna ya kuendelea kuishi Mwanza.. Nipo maeneo ya nyegezi tu hapa nimejawa na stress...

Msaada tafadhali..
 
Kaka hao voda hata hizo 7 wamekudanganya! Ukizipata labda baada ya mwez hapo mpk mahakaman! me mpk sasa nishapotezea laki na nusu! Nimezunguka kila ofs yao nimegiveup
 
Kaka hao voda hata hizo 7 wamekudanganya! Ukizipata labda baada ya mwez hapo mpk mahakaman! me mpk sasa nishapotezea laki na nusu! Nimezunguka kila ofs yao nimegiveup
Mkuu kwa kweli ni mistake ndogo na wameniambia hela ipo hewani ila watairuhusu irudi ndani ya siku 7.... I never expected that
 
Mkuu kwa kweli ni mistake ndogo na wameniambia hela ipo hewani ila watairuhusu irudi ndani ya siku 7.... I never expected that
Kaka bora wewe umekosea! Mimi sikukosea nilituma sehem sahihi ila pesa haikufika na kwangu haokurudi
 
Haya yameshakuwa majambazi bila silaha nililipia faini za makosa barabarani nilikamatiwa tazara nikarudi mwanza nilipe nikakosea kumb No sijarudishiwa pesa yangu mpaka leo naambiwa iko hewani siku saba zimekatika hola kesho nina mpango niende ofisini kwao pale vodashop wanipe pesa yangu la sivyo nitakinukisha pesa imeshakuwa ngumu namna hii halafu wanaleta ujanja ujanja
 
Mkuu kawaida inakuwa masaa 72, kuna siku wakala alikosea kutuma wakanirudishia ndani ya saa 1. Hiyo ya kwako sijajua ni kwanini wamekuambia siku 7.
 
Kaka hao voda hata hizo 7 wamekudanganya! Ukizipata labda baada ya mwez hapo mpk mahakaman! me mpk sasa nishapotezea laki na nusu! Nimezunguka kila ofs yao nimegiveup

Mkuu unazungumzia mwezi! Hahaa anaweza asizipate kabisa, unawajua voda au unawasikia!
 
Mkuu kawaida inakuwa masaa 72, kuna siku wakala alikosea kutuma wakanirudishia ndani ya saa 1. Hiyo ya kwako sijajua ni kwanini wamekuambia siku 7.
Hapa ninajiandaa kupumzika nikiwa na imani kubwa kuwa itakuwa umerudi asubuhi. Aliniambia utaratibu umebadilika na yeye yupo makao makuu na pia aliniambia hata nikienda vodashop sitasaidika.. Kwa sababu yeye yupo hq
 
Hiyo hairudi mkuu! Utatupa mrejesho hapa! Hao ni matapeli! Cha msingi anza mdogo mdogo kwa mguu, au kama una mtu azima tu
 
Nimevunjika moyo sana.. Nina ratiba za kiofisi Arusha hivyo nikichelewa kurudi ni maumivu makubwa kwangu
 
Mkuu wana jukwaa lao humu kama liko active ni bora issue yako ipeleke kule unaweza pata msaada.
 
Hawa jamaa kwa sasa wamekua tatizo mimi tarehe 12/7 nilihamisha pesa kutoka mpesa kwenda ac ya bank uhamisho ukakamilika na pesa wakanikata tarehe 16/7 wakazichukua tena hizo pesa kiasi cha sh.330000 kwangu hazikurudi na bank hazipo
 
Hamia airtel mkuu. Mm voda nilishahama kitambo tangu mwaka jana mwez wa 12. Walinizingua sana, tangua siku nikauchukia sana. Hawa siku hiz wamekuwa matapeli kbsa mkuu. Mm sina hamu nao kbsa hawa jamaa. Hapo andika maumivu. Ingia kweny page ya vodacom uone watu wanavyolalamika
Kwa hali hii watapoteza wateja sana.
 
Mimi wamenila 240000
tokea tarehe 10/7 hadi leo,
awali waliniambia nisubiri ndani ya masaa72,
ila mpaka sasa ni hewa tu, yaani inauma sana bora ningejua nimeifanyia jambo gani hyo pesa.. kulikokuipoteza kama ilivyotokea
 
Mrejesho....

Nimerudishiwa pesa zangu muda huu.. Baada ya kufanya nao mawasiliano kwa kupitia Twitter.. Huyo staff kunisaidia haraka na kwa busara.. Just by chatting..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom