Vodacom nirudishieni pesa yangu haraka, acheni wizi na uhuni mnaofanya

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,104
7,857
Kutokana na uhuni ambao VODACOM wamekuwa wananifanyia, mfano bando zangu zinaisha haraka sana katika mazingira ya wazi ya wizi na udanganyifu, nimepunguza sana kutumia vifurushi vyenu. Sasa bado nahifadhi hela yangu kwenye M-PESA na nikiwa na mahitaji nayo ya kununua bando najitumia kwenye namba nyingine.

Hivi karibuni nimegundua kumbe unaweza kununua airtime moja kwa moja kutoka M-PESA kwenda mtandao mwingine bila kuingia gharama za kutuma hela kwanza, nikasema, this is even better! Sidhani kama utaratibu huo mnaupenda.

Sasa jana nilinunua airtime kwenye namba yangu nyingine kutoka M-PESA, nikakaa kidogo kimya, sioni message imeingia wala nini. Nikakumbuka last time ilitokea hivi hivi na nilipoamua kucheki balance ya M-PESA, haikupita dakika 3 message ikaingia kuwa hela niliyotumia imekwenda.

Akili ikanijia kuwa kumbe mnanitegea mpaka nicheki balance yangu ndiyo mnakamilisha muamala (ukicheki balance utaratibu unajulikana kuwa mnakata hela kwenye M-PESA). Nikasema sitafanya hivyo, badala yake nikajitumia kiasi kidogo cha pesa kutoka M-PESA kwenda M-PAWA, nikajua ukifanya hivyo message itakuja ikionyesha balance ya M-PAWA na M-PESA. Na kweli, message imekuja hapo hapo na inaonyesha hela niliyotuma imekwenda na hata ile niliyotuma kununua airtime mtandao mwingine pia inaonyesha ilishatoka ila kule kwingine haijafika.

Customer service nimewapigia jana wananiambia nisubiri masaa 24 kama itashindikana nitarudishiwa. Nimesubiri sasa ni masaa zaidi ya 28 yamepita, hela yangu haijarudi M-PESA na huko nilikotuma haijafika.

Najua mnanitega mpaka nicheki balance yangu ya M-PESA ili mnikate hela ndiyo mkamilishe muamala na nimeamua sifanyi hivyo.

Msiponirudishia hela yangu nitachukua hatua zaidi.
 
Screenshot_20200516-181824.jpg

Ni mwezi wa pili sasa nimehamia Halotel special line.
Voda na Tigo Huko sirudi tena, zinakaa hewani tuu sababu ndio zimezoeleka.

Elf 10,
GB 12, dk 100000 mitandao yote, SMS 500 siku 30.
 
Pole sana na kuwa makini ,sasa wanaongeza namna ya kujipatia mapato zaidi

Na wameanzisha kamari ya mnada poa ili kuchukua jero jero za wanyonge
 
Kutokana na uhuni ambao VODACOM wamekuwa wananifanyia, mfano bando zangu zinaisha haraka sana katika mazingira ya wazi ya wizi na udanganyifu, nimepunguza sana kutumia vifurushi vyenu. Sasa bado nahifadhi hela yangu kwenye M-PESA na nikiwa na mahitaji nayo ya kununua bando najitumia kwenye namba nyingine.

Hivi karibuni nimegundua kumbe unaweza kununua airtime moja kwa moja kutoka M-PESA kwenda mtandao mwingine bila kuingia gharama za kutuma hela kwanza, nikasema, this is even better! Sidhani kama utaratibu huo mnaupenda.

Sasa jana nilinunua airtime kwenye namba yangu nyingine kutoka M-PESA, nikakaa kidogo kimya, sioni message imeingia wala nini. Nikakumbuka last time ilitokea hivi hivi na nilipoamua kucheki balance ya M-PESA, haikupita dakika 3 message ikaingia kuwa hela niliyotumia imekwenda.

Akili ikanijia kuwa kumbe mnanitegea mpaka nicheki balance yangu ndiyo mnakamilisha muamala (ukicheki balance utaratibu unajulikana kuwa mnakata hela kwenye M-PESA). Nikasema sitafanya hivyo, badala yake nikajitumia kiasi kidogo cha pesa kutoka M-PESA kwenda M-PAWA, nikajua ukifanya hivyo message itakuja ikionyesha balance ya M-PAWA na M-PESA. Na kweli, message imekuja hapo hapo na inaonyesha hela niliyotuma imekwenda na hata ile niliyotuma kununua airtime mtandao mwingine pia inaonyesha ilishatoka ila kule kwingine haijafika.

Customer service nimewapigia jana wananiambia nisubiri masaa 24 kama itashindikana nitarudishiwa. Nimesubiri sasa ni masaa zaidi ya 28 yamepita, hela yangu haijarudi M-PESA na huko nilikotuma haijafika.

Najua mnanitega mpaka nicheki balance yangu ya M-PESA ili mnikate hela ndiyo mkamilishe muamala na nimeamua sifanyi hivyo.

Msiponirudishia hela yangu nitachukua hatua zaidi.
VODACOM ni wezi sana tena sana. Mi nilinunua bundle la 50,000, ndani ya siku mbili kwisha. Nikanunua bundle ya 20,000 ndaki ya siku moja ikaisha. Sasa nimeamua kurudi kwenye university, maana huko wanajua hao ni maskini hakuna haja ya kuwaibia
 
Voda wana university offer
 
Voda muninyoooshee hizi kenge, endeleeni kukaza!
Mahali pekee voda wanaponipiga spana ni kwenye MPESA tu. Si vinginevyo.
 
Ila hawa wajinga nina hasira nao sana. Juzi nimetoka kuwawakia mno.
 
Back
Top Bottom