Vodacom ni kero, wananiambia wana hitilafu ya kimtandao hela niliyotuma ipo hewani

mezanane

Senior Member
Apr 11, 2011
116
185
Vodacom mnahuduma mbovu sana. Nimetuma Pesa kwenda mtandao wa Tigo nimekatwa hela lakini baadaye wanatuma message hii,
"Samahani, muamala wako haukukamilika kwasababu za kiufundi. Tafadhali wasiliana na huduma kwa wateja."

Nawapigia customer care wananiambia wana hitilafu ya kimtandao hela niliyotuma ipo hewani.

Kwamba watatua tatizo ndani ya saa 24 nawaambia huo ni muda mrefu hela ni ya mgonjwa hawezi kuwasubiri wanasema hawana njia yeyote ya kutakua.

Nawaza kwa sauti vyombo vinavyowasimamia hawa jamaa TCRA na BOT wako wapi?

Kama wana tatizo na wameona muamula upo sijui hewani si wanirudishie pesa yangu nitume kwa njia nyingine?

Ni wakati muafaka kukomesha huu ubabe wa kibiashara ni kinyume na haki za mteja.
 
Kweli haiwezekani kwani ni mpaka Tigo wagundue shida ndipo hela irudi tafuta another alternative.
 
Ila tigo walitoa taarifa hii mapema tu saa tisa

Ndugu Mteja, Kutakua na maboresho ya huduma za Tigo Pesa leo kuanzia saa 5 usiku mpaka 12 asubuhi. Tafadhali fanya miamala yako kabla na baada ya muda huo
 
Mkuu matatizo ya kimtandao hasa hela utatuz wake unahusisha high command ya kampuni , huenda ni mtu mmoja Tu anayeweza kutatua hii ni kuepusha flaud ...usiwaforce hao customer care ndo wameishia hapo , na lazima uwe mpole tuu mkuu...
 
Vitu nilivyojofunza vya KUTOFANYA ninapotumia hizo Mobile Money:

1. Kutotuma pesa kupitia mitandao miwili tofauti.

2. KUTOTUMA hela kutoka Bank au kwenda Bank.

Aisee niitwe mshamba tu.
 
Vitu nilivyojofunza vya KUTOFANYA ninapotumia hizo Mobile Money:

1. Kutotuma pesa kupitia mitandao miwili tofauti.

2. KUTOTUMA hela kutoka Bank au kwenda Bank.

Aisee niitwe mshamba tu.

Na pia Kutuma hela kutoka Bank kwenda Mobile Money (M- Pesa, TigoPesa ...you name it ) Gharama au charges ni kubwa balaa
 
Me. Iliwahi kubaki hewani adi Leo sijuwi Sana hivi itakuwa sayari gani
 
Me. Iliwahi kubaki hewani adi Leo sijuwi Sana hivi itakuwa sayari gani
Sijawahi kukutwa na tatizo la kiufundi na Voda haswa maswala ya helahela ndio mtandao naouamini ktk hiyo sekta unafuata halotel.. mkuu pesa yako itakuwa ilikwapuliwa na alien alishaga inywea balimi huko..🤣
 
😂 Me pia ninatumia voda Ila ndio hao hao wamliniambia pesa ipo hewani sijuwi hewani ya umbali gani
 
Back
Top Bottom