VodaCom Miss Tanzania 2009

Mbogela

JF-Expert Member
Jan 28, 2008
1,384
257
Umewadia wakati mwingine tena wa mpambano wa kumsaka mrembo atakayeipeperusha bendera ya nchi katika mashindano ya 60 ya dunia (Miss World) yanayotarajiwa kufanyika huko Afrika Kusini 12 Desemba 2009.

Warembo wapatao 30 tayari wameshaingia kambini wakijiandaa na mchuano huo. shindano la Vodacom Miss Tanzania linaratibiwa na kamati ya Vodacom Miss Tanzania chini ya mkurugenzi Hashimu Lundenga.

Mpaka sasa Tanzania haijafanya vizuri katika mashindano ya kimataifa ingawa ndani ya nchi shindano limezidi kupata msisimko mkubwa. Hali ya hivi karibuni imeonyesha kumekuwa na mchuano mkali kati ya washindani wanaotoka mikoani na wale wanaotokea mikoa ya Dar.

Katika mshindano ya ngazi za mikoa tuliona washindani walioshindwa wakianguka majukwani na kupoteza fahamu, na pia shindano hili limekuwa likipata umaarufu kadri siku zinavyosogea mbele.


CONTESTANTS:


11.JPG

STELLA CHIDODO-SINGIDA

30.JPG

MARY JOSEPH- MARA

29.JPG

TORRY OSCAR-MOROGORO

28.JPG

CATHERINE LETARA-NYANDA ZA JUU KUSINI

27.JPG

GLORY WILLIAM-ILALA

25.JPG

EVELYN LUJAMASA-ILALA

24.JPG

BEATRICE LUKINDO-VYUO VYA ELIMU YA JUU

23.JPG

LULU IBRAHIM-KINONDONI

22.JPG

GLORIA MAYOWA-LINDI


21.JPG

MARIA DANIEL-ARUSHA


21a.JPG

PRECIOUS DONALD-PWANI

20.JPG

GLADIES SHAO-ILALA


19.JPG


ALOYCIA INNOCENT-KINONDONI

18.JPG

SUZAN EMMANUEL-ARUSHA




17.JPG

MARY LUCAS-NYANDA ZA JUU KUSINI


16.JPG

STELA SOMONI-TEMEKE

15.JPG

SIA NDASKOI-TEMEKE

14.JPG

SANDRA MALEBEKA-KINONDONI

13.JPG

DORIS DEODATUS-VYUO VYA ELIMU YA JUU

12.JPG

ESTER GAO- VYUO VYA ELIMU YA JUU

10.JPG

SABINA BUDODI-MARA

9.JPG

JULIETH WILLIAM -ILALA

8.JPG

IVONY BIGIRWA-KINONDONI

7.JPG

WAGALA SHUNGU-VYUO VYA ELIMU YA JUU

6.JPG

SHANY ANTONY-TEMEKE

5.JPG

JACQUELINE NITWA-DODOMA

3.JPG

MIRIAM GERALD-MWANZA

2.JPG

SLYVIA SHALLY-ILALA

1.JPG

GLORY CHUWA-TANGA

26.JPG


WITNESS NESPHORY-NYANDA ZA JUU KUZINI (AMETOLEWA KWA KUBAINIKA NI MJAMZITO).



Miss Tanzania 2009 Finals, October 2

Vodacom Miss Tanzania 2009 pageant final is to be held on Friday 2 October 2009 at Mlimani City, Dar es Salaam. That was said in Dar es Salaam yesterday by Miss Tanzania Director, Hashimu Lundenga.

Lundenga said that the preparation is in progress after the process of completing competition for almost six months starting from first stages, municipals, regions and zones. "We are aimed at holding this pageant for high quality ever in the history of this country especially those ones held in in-door halls" said Lundenga.

He said that they have decided to hold it in-door halls because of the weather change which is expected to start anytime. He added that various and prominent musicians in the Tanzanian market and outside are expected to entertain on the show.

Vodacom Miss Tanzania 2009 is sponsored by Vodacom Tanzania Limited, Samsung Electronic Company Limited, Tanzania Broadcasting Corporation (TBC) ,New Habari (2006) LTD, Tanzanite One Group and Giraffe Oceanic View Hotel.

30 contestants from different zones are expected to contest this year on Miss Tanzania 2009. The contestants are expected to start camping on September 7 at Giraffe View Oceanic Hotel.

The current Miss Tanzania title holder is Nasreem Karim Ndiye.
 
Last edited:
Bwana taji Liundi pamoja na Nancy Sumari wametajwa kuwa watakuwa washerehekeshaji wa sikuu hiyo kwa mujibu wa mtandao wa JIACHIE
 
Wanaume bwana, hivi ni kweli, akili zao huwa zinawaza kitu kimoja tu when it comes to warembo?
 
Miss Tanzania hapatoshi
Imeandikwa na Betram Lengama;
1st October 2009

Habari Leo

HOMA ya shindano la kumsaka Miss Tanzania mwaka huu inazidi kupanda katika kambi ya warembo, Dar es Salaam.

Wasichana hao, kila mmoja anatamba kwamba atatwaa taji hilo Ijumaa kumrithi Nasreem Karim. Warembo wanaotoka nje ya Dar es Salaam wamewatambia wenyeji wao kuwa wasahau taji la mwaka huu.

Mlimbwende kutoka Dodoma, ambaye pia anaiwakilisha Kanda ya Kati, Jacqueline Nitwa, amepania kufuata nyayo za Emil Adolf. Emil alitwaa taji la Miss Tanzania mwaka 1995 alipouwakilisha mkoa wa Dodoma.

Jacqueline amesema, amejiandaa vizuri hasa baada ya kubaini mapungufu waliyokuwanayo katika mashindano yaliyopita.

“Waandaaji wa mikoa hivi sasa wana uzoefu mkubwa baada ya kubaini mapungufu waliyokuwa wakiyafanya katika maandalizi warembo hapo kabla na safari hii na kuendelea utawala wa Dar es Salaam umekwisha,” amesema mrembo huyo kwa kujiamini.

Mrembo kutoka mkoani Morogoro,Tolly Oscar, amewataka walimbwende wa Dar es Salaam wasahau taji la mwaka huu kwa maelezo kwamba, Miss Tanzania mwaka huu lazima atoke mikoani.

Wiki iliyopita msichana huyo alitia fora kwenye shindano la vipaji ambalo ni sehemu ya shindano la Miss Tanzania mwaka huu.

Tolly amesema, kwa kuwa taji hilo lilikwenda Mwanza mwaka jana halirudi tena Dar es Salaam kwa sababu warembo wa mikoani wamepania 'kufanya kweli'.

Hata hivyo, mrembo, Sylvia Shally, kutoka kanda ya Ilala, Dar es Salaam, amejigamba kwamba, mwaka lazima mmoja wa warembo kutoka huko awe Miss Tanzania.

Walimbwende watano wanaiwakilisha Kanda ya Ilala katika shindano la mwaka huu litakaloshirikisha warembo 29.

“Ilala tumejiandaa vilivyo na safari hii tunahakika miongoni mwetu sisi watano atalichukua taji na kulirejesha nyumbani baada ya kulikosa kwa miaka kadhaa sasa” amesema Sylvia.

Jopo la majaji tisa wa shindano la kumsaka mlimbwende wa Tanzania ‘Miss Vodacom Tanzania 2009’ litajulikana leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya majaji hao walifahamika tangu jana akiwemo Susan Mungy Kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), na Doris Malulu, wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

Majaji hao jana walikuwa na semina katika hoteli ya Giraffe nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
 
Hivi ni saa ngapi hiyo miss tanzania ?


....duuuuh, mashindani haya safari hii hayana mvuto kabiiiisa JF mwaka huu,...tofauti na miaka ile ya kina Richa Adhia, mkuu MegaPayne alipokuwa anatumwagia mapicha humu,... :D
 
....duuuuh, mashindani haya safari hii hayana mvuto kabiiiisa JF mwaka huu,...tofauti na miaka ile ya kina Richa Adhia, mkuu MegaPayne alipokuwa anatumwagia mapicha humu,... :D


Naona mkuu Mbogela hana access tu, inaonyesha mdau sana wa fani hizo, yeye anatoa data tu, bila visual aids!!
 
yani hata siangaliii.sijui mwaka huu vipi.yaani natazama tbc lakini hata interest sina.
 
Back
Top Bottom