VodaCom MasterCard rekebisheni hii kasoro ya kiusalama

Kaudunde Kautwange

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
1,243
2,000
Kwanza kabisa niwape pongezi VodaCom kwa kutuletea huduma ya MasterCard. Kwa kweli mmetukomboa.

Lakini mbali na yote, suala la usalama hamjalizingatia kabisa!

Ukiingia kwenye menu ya M PESA, chukulia tayari umesha create MasterCard yako, sasa ili kupata taarifa za card yako, baada ya kungia kwenye menu ya M PESA, utachagua Lipa kwa M PESA.. hapa utaenda kwenye kitufe cha MasterCard. ukiingia tu, utakutana na kitufe cha View MasterCard info... sasa hapa ndo penye kasoro ya kiusalama.

Kwa kufanya hivyo, utaweza pata infos zote za kadi, ambazo utazitumia kufanya muamala online, na ukiweke tu, hakuna cha kuuliza namba ya siri wala nini, muamala unafanyika automatically.

Sasa hii, maana yake ni kuwa, mimi kama najua jamaa yangu anatumia M PESA MasterCard, namuibia kwa urahisi zaidi, maana kwa kufuata hizo steps hapo juu, nitaweza kupata taarifa za Card yake.

Tofauti na bank, bank hata ukiweka hizo infos za Card, bado utahitajika kuwe na namba ya siri ili kuruhusu muamala kufanyika. Lakini tofauti kabisa na nyinyi, yaani kwa kupata hizo infos nakuwa nimemaliza kila kitu.

SULUHISHO
Weke kizuizi hapo, kabla mtu ajauliza kupata infos za Card yake, kuwe na ulazima wa kuweka namba ya siri ya M PESA, hii itasaidia sana!

Mniwie radhi kwa uandishi wangu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Michael Mtitu

Verified Member
Oct 6, 2012
633
500
Kwanza wangeweka tu password hapa nje kabisa kama wanavyofanya bank. Yaani ukibonyeza tu *150*00# utakiwe kuingiza password kwanza kabla ya kufanya chochote.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom