Vodacom M-pesa yapandisha tozo la kutoa na kutuma pesa

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,898
11,745
Nimeenda kutoa pesa kupitia huduma ya M-pesa nimeshangaa kukuta vodacom kupitia huduma yao hiyo wamepandisha gharama za kutuma na kupokea pesa mathalani zamani kutoa 40000-49000 ilikuwa unakatwa Tsh 1800 lakini sasa hivi ni 2200, tozo hili ni kubwa sana kwa wananchi wa kipato chini wanaotumia huduma hiyo ya kutuma na kupokea pesa.
Tunaomba serikali isimamie kupanga viwango vya kutuma na kutoa pesa ili makampuni ya simu yasituibie watanzania.
 
Tulia uisome namba wewe,ala!?
 
Hawa walikuwa wakwepa kodi wakubwa. Baada ya issue ya TCRA, wamehamishia kodi kwa wananchi.
 
Wakuu sio voda pekee waliopandisha makato hadi Tigo wamepandisha jana nilitoa 50,000 nikakatwa 2250 naona
Tunaomba haya makampuni yatupe ufafanuzi kuhusu haya makato na serikali iliangalie tena kwa jicho la tatu
 
Alafu sasa uliza mawakala wanapata sh ngapi kwenye iyo 2,200.
Kwa muamala huo wakala anapata 350 ambayo mwisho wa mwezi inakatwa 100%...
Magufuli sema neno mawakala na mitaji yao ipone
 
Kabla ya hapo mimi nilishtuka miezi miwili iliyopita, ni afadhali bank kwenye ATM wanakata shs 500 kwa kiasi chochote chini ya 400,000/- ukitoa.

Tokea hapo sina stress through mitandao ya simu, ninachofanya kwenye line nnazotumia naweka salio la kununulia credit tu!.
 
Haitosaidia kitu hata mukilia tulieni dawa iwaingie
HAPA KAZI TU.! nyie mulitakaje hacha tuisome namba
 
Back
Top Bottom