Vodacom kukubali ombi la Yanga ni zaidi ya udhaifu ktk biashara

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
5,159
5,399
Msimamo wa yanga kwa sasa ni kutoitambua nembo ya mdhamini kampuni ya Vodacom Tanzania kutokana na rangi zake nyeupe na nyekundu.

Ni wazi hii imeleta mtafaruku tangu msimu uliopita.Nembo ya vodacom nyekundu na nyeupe ndiyo nembo yao ya biashara inayotambulisha kampuni hiyo siyo maneno.
Ikiwa vodacom watakubali kuibadili nembo hiyo kwa matakwa ya wanayanga ni wazi mdhamini atakuwa hawakilishwi wala kutangazwa na yanga bali yanga watakuwa wanatangaza kitu kingine tofauti kinachoshabihiana na nembo ya vodacom ila hakika hakitakuwa nembo ya vodacom.

Ifike hatua TFF waheshimu mikataba wanayoingia na wadhamini na timu pia ziheshimu nembo za kibiashara za wadhamini wao.
Kitu kinachotaka kufanyika kwa yanga ni cha kipekee duniani hakipo mahali popote ktk ulimwengu wa soka duniani na ktk biashara na sheria za mikataba.
FB_IMG_1567927955994.jpeg
 
John na Yohana ni sawa na kusema Soccer na Kandanda.
BRELA pia wanajua nembo ya vodacom siyo hiyo ambayo yanga wanataka kuitumia na ikiwa yanga wataitumia hiyo tofauti na vodacom bado BRELA wanauwezo wa kuwashitaki vodacom kutumia nembo ambayo hawajaisajiri hivyo wakaonekana ni wafanyabiashara haramu watakatishaji pesa tu.
Otherwise waende BRELA washughulikie hilo ili wawe na nembo mbili tofauti na hapo ni kinyume na sheria.
 
Umejuaje kama hawajasajili?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom