VODACOM HUU WIZI AU KUREKEBISHA MTANDAO.

mcmzungu

Member
Jul 11, 2015
48
65
Mimi ni wakala wa Max malipo,kawaida huwa Tunatumia mpesa kutuma miamala ya fedha kwenda katika mashine za maxlipo ili kuweza kuuza luku, vocha nk mnamo tarehe 22/6/2016 saa 2:54:33am Nilituma fedha 50,000 kwenda 302726 (Max malipo no) ya kulipia ajabu fedha iliingia kisha ikatolewa ghafla yote wakalamba, kwenda kufuatilia maxcom wakanipa kumbukumbu no 3FK3503HF kwamba Nifuatilie vodacom ndo wamechukua Niliporudi vodacom wakafuatilia wakasema fedha itarudi lakini mpaka leo haijarudi Ukiuliza oh Tunashughulikia lakini kimya hata majibu ya customer care hayaridhishi ni Kama Umetoa sadaka na hali ya kiuchumi kwa sasa ilivyo rahisi 50,000 ni nyingi sana Naomba vodacom Tafadhali rudisheni fedha yangu na Mimi ni mmoja wapo huwezi jua Watu wangapi fedha zao hazijarudi kupitia miamala ya simu. Ushauri wangu kuwe na center maalum katika kushughulikia miamala ya muda mrefu.Mteja wenu.
 
Back
Top Bottom