VODACOM: Huu ni Wizi wa Mchana Kweupe!

Jitume

Senior Member
Dec 13, 2008
142
23
Nilijiunga na shindano la promotion ya BURE linaloendeshwa na VODACOM. Kwenye maelezo yao wameelekeza namna ya kujitoa kwenye shindano hilo la kila siku. Baada ya kujiunga kwa muda wa siku tatu ambapo unakatwa sh. 550/= kila siku, niliamua kujihengua. Nimefuata utaratibu wa kujihengua na wao wakanitumia sms ya kuondolewa kwenye promotion vinginevyo nijiunge tena.

Hajabu wanaendelea kukata shs 550/= kila ninapoongeza salio bila idhini yangu . Huu si uhuni na wizi? Na hawaweki namba ya mawasiliano kwenye sms za promotion hiyo incase mteja ana tatizo kuhusiana na jambo hilo. Ninakusudia kusitisha matumizi ya line yaho mpaka promotion imalizike.
 
Hii ni kampuni isiyojali wateja hata utu wa watu.Kama wao waliweza kuendelea na Miss Tz huku watanzania tunamajonzi wewe unategemea nini.!
 
Unajitoaje kwenye huu utapeli??
Mi wananiboa sana na limeseji lao eti "sishikiki",
Sishikiki kivipi?
Na nishikike ili iweje?
 
Kawashitaki TCRA Ipo next to Mlimani city kama unatokea mwenge kwenda Ubungo. Watapewa adhabu na watakulipa kiasi chochote utakachotaja kulingana na usumbufu ulioupata. TCRA ni kiboko yao kamwone Jamaa mmoja Anaitwa Innocent Mungi au Semu Mwakyanjala ni watu wa Information.
 
Nilijiunga na shindano la promotion ya BURE linaloendeshwa na VODACOM. Kwenye maelezo yao wameelekeza namna ya kujitoa kwenye shindano hilo la kila siku. Baada ya kujiunga kwa muda wa siku tatu ambapo unakatwa sh. 550/= kila siku, niliamua kujihengua. Nimefuata utaratibu wa kujihengua na wao wakanitumia sms ya kuondolewa kwenye promotion vinginevyo nijiunge tena.

Hajabu wanaendelea kukata shs 550/= kila ninapoongeza salio bila idhini yangu . Huu si uhuni na wizi?Na hawaweki namba ya mawasiliano kwenye sms za promotion hiyo incase mteja ana tatizo kuhusiana na jambo hilo. Ninakusudia kusitisha matumizi ya line yaho mpaka promotion imalizike.
mzee ilikuaje ukajiunga, watanzania kwa vya bure. ila ingekuwa bure si wangeliangalia wateja wao wazuri wakawapatia tu hizo tv kwani lazima wachezeshe bahati nasibu.
 
nijuzen jinsi ya kujitoa bana otherwise hali itakuwa ngumu

Ushalikoroga hilo best, ni lazima ulinywe!!! Kama halinyweki, basi ongeza japo pilipili na ndimu kidogo ili upate stimu na bila shaka next time utakuwa makini katika kukurupukia vya bure! Ulisikia wapi mtu akupe 11m hivi hivi tu?! Vodaaaaaaaaa, kula visenti vyao watu kama hawa hadi gharama za gari lenu mulilotoa kwa Vodacom Miss Tanzia zitakapokuwa recovered!!!
 
Kawashitaki TCRA Ipo next to Mlimani city kama unatokea mwenge kwenda Ubungo. Watapewa adhabu na watakulipa kiasi chochote utakachotaja kulingana na usumbufu ulioupata. TCRA ni kiboko yao kamwone Jamaa mmoja Anaitwa Innocent Mungi au Semu Mwakyanjala ni watu wa Information.
<br />
<br />
Hivi hii habari ya "kamwone kamwone" itaisha lini? Huwa najiuliza hawa watumishi wa TCRA wanatumia line za mitandao gani kiasi hawaoni wala kujua kinachoendelea mpaka wanasisitiza wote tupeleke malalamiko yetu huko? Nchi hii sasa imekuwa kama choo cha umma kwa mia 2 yako tu unaingia kufanya utakalo!
 
Kwanini mwanzoni ulijiunga?. Nyie ndio mnaoish kwa ndoto. Unatoa 550 unapata million.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom