Vodacom hiki mnachokifanya kwa wateja wenu ni uhuni wa hali ya juu sana. Jirekebisheni haraka iwezekanavyo

Kwa wiki nzima Sasa Voda wamekuwa wakinifanyia Huu uhuni.

Sina Deni songesha Wala nipige tafu.

Nimeweka Bando la sh elfu 2 Na Mia tano ili nijiunge Na kifurushi cha internet cha siku.

By the time namaliza kujiunga naambiwa salio halitoshi. Natazama salio nakuta lipon2400 au 2300 ikiwa Na maana kwamba hizo sekunde wakati natumia kujiunga wamenikata sh Mia mbili au sh Mia.

Nikijaribu kupiga huduma Kwa wateja nakuta wame incapacitate Ile segment ya kuongea Na mhudumu. Yani utapiga simu halafu katika zile option za kubonyeza kunakuwa Hakuna option ya kuongea Na mhudumu.

Nashindwa kuamini kama Voda wanaweza kuwa wababaishaji kiasi hiki.

Najiuliza Ni kwamba Voda wanajua kuhusu uhuni Huu au Kuna watu wachache WA kitengo cha IT Voda ndio wanacheza Huu mchezo? Wanakata hizo Mia mbili Mia mbili for unsuspecting victims?

Vodacom Vodacom Vodacom Huu ni uhuni ambao hauwezi kukubalika.
Dah! Mkuu umenikumbusha miaka imepita, kuna wizi tulifanyiwa watumishi wa Wizara flani bila ya sisi wadau kuhisi ama kugundua kuibiwa, yaani mpaka leo huwa sihisi wala kuamini kama nami ni mmoja wapo kati ya walioporwa!

Kijana wa It makao makuu aliprogram makato ya sh.500 toka katika mishahara ya kila mwezi ya kila mmoja wetu.

Embu fikiria loss ya sh.500 utaigunduaje katika mshahara wako?

Na wizara ilikuwa na watumishi zaidi ya 40000, hapo piga hesabu, jibu utakalolipata, ndiyo hela alikuwa akitia kibindoni mwake kila mwezi!

Kijana akatajirika hadi akavimbewa kwa kufuru.

Sijui pesa za bure huwaga zina laana gani tu, maana life style yake ndiyo iliyofanya watu waanze kujiuliza: "huu utajiri wa kutisha kaupata wapi huyu kinda.

Kwani walimkawiza.
 
Voda naitumia sababu nilipo ndio mtandao pekee unaosababisha niwe mtandaoni bila kusumbuka 4G
Nikiwa mjini tiGO na Halotel
 
Voda ni kwa wateja wenye matumizi ya utopolo na utopolo wenyewe. Voda ni vibaka watupu
 
Mnaosema ni data ime kata sh100 au 200 sio kweli maaana data ina kata haswaaa within seconds una weza kuta sh 0.

Hapo mteja ume unganishwa na vihuduma vyao kama SOKALETU tazama kama huna hizo text kila zikiingia tu wana kata tshs 200 una letewa habari Ligikuu bara hapo mzee wame kuunga makusudi kama wanavo tuunga wateja wengine ili watule masalio yetu
 
Back
Top Bottom