Vodacom CHEKA TIME ni utapeli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vodacom CHEKA TIME ni utapeli?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lucchese DeCavalcante, Sep 9, 2009.

 1. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kuna hii huduma ya VodaCom CHEKA TIME ambayo imeanzishwa hivi karibuni, kujisajili unatakiwa kuwa na salio la angalau TZS 5,000 na unapiga *147*01# kujisajili.

  Sasa leo nimejaribu kujisajili na inakupa ujumbe ufuatao

  "Umenunua dakika 300 za CHEKA TIME kwa Tsh 5000 kwa muda wa siku 5 kuanzia leo,zitumie upige simu bure Voda kwenda Voda kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 10 jioni"

  Kwa kweli huu ni utapeli na udanganyifu wa hali ya juu sana kwani mtu unalipia TZS 5,000 lakini wenyewe wanadai eti ni huduma ya bure kwa vipi? Wadanganyika tutadanganyika na kunyonywa mpaka lini au ndio mambo ya eti ukiwekeza Bongo hata kwa mtaji kiduchu lazima upate faida ya kufa mtu kwa kipindi kifupi???
  Huzuma kama hizi pia zinatolewa na makapmuni mengine ya simu ya Zantel, Zain na TIGO wakidai ni za bure kumbe unazilipia, wadau hii imekaaje??
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  wametuibia kimya kimya wamechoka wanataka mpaka tujue jinsi wanavyotuibia......poa komputer wanajua wao sisi ni kubali yaishe,ila mkiwa tayari wadau tuandamane.......
   
 3. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Ni wizi wa aina hii utaendela mpaka lini?
   
 4. GP

  GP JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  WAKUU,
  kuna maswali mengi ambayo mtanzania wa kawaida anaweza kujiuliza hapa.
  mfano wake ni kama hivi:
  [FONT=&quot]
  [/FONT] [FONT=&quot]1. yaani ukitoa Tsh 5000 utakua unaweza kupiga simu bure kwa dakika 300 kila siku ndani ya siku tano ama vipi??
  2. je, hawa Vodacom, suppose nimeongea hizo dakika 300 ambazo ni masaa 5 tu
  inamaana Tsh 5000 yangu itakua kwishney ama??.
  (mfano wa Zain na Tigo wao unalipa 1900/1800 lakini unaongea BURE tangu 12 asubuhi hadi 12 jioni, hii ni sawa kwa kua inaeleweka wazi ni masaa 12 kwa siku moja)[/FONT]


  Mimi nadhani hawa Vodacom watakua wametumia lugha ya 'kisanii', nionavyo hapa ni kwamba kama wangetumia lugha takatifu na fasaha ya kiswahili ilitakiwa waseme ifuatavyo:
  "kati ya Jumatatu hadi Ijumaa (ambazo ni siku 5) mteja wa Vodacom ataweza kupiga simu kwa Tsh 5000 vodacom kwenda vodacom"
  AMBAYO KWA SIE WAKALI WA MAHESABU TUNAWEZA KUSEMA KWAMBA KWA SIKU MOJA(kati ya jumatatu hadi Ijumaa) MTEJA ATAONGEA NA SIMU KWA MASAA 5 (dk 300) KWA Tsh 5000, KWA LUGHA NYEPESI NI Tsh 1000 KWA SAA.
   
  Last edited: Sep 9, 2009
 5. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Na kama ni TZS 1000 kwa saa kwa nini wanasema ni BURE hapa ndio kuna issue??
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Mimi naona labda ni kiswahili kupindana kidogo. Wanaamanisha kuwa ukiingia tu kwenye huduma hiyo kuna fee ambayo itakatwa kutoka kwenye salio lako. sasa ukishakatwa tu basi wewe utakuwa huru kupiga simu bila salio lako kukatwa ka kipindi kile walichokuwekea na ee kukubali.

  Kisheria huwezi kusema huu ni wizi.Bali ni makubaliano.
   
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  sio makubaliano.........ukipiga hesabu ina kuwa Tsh17/minute,sasa si bora ninunue tigo naweka vocha na kuchonga tu bila kujiunga?
   
 8. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Wewe barubaru unafahamu sheria au unakurupuka tu? Makubaliano lazima yawe yanaeleweka na wazi vinginevyo ni utapeli
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Sasa hapa unachanganya madawa. Mada yako inahusu huduma za Voda. mara unarukia huduma za Tigo. Sielewi una maana gani?

  .

  Sasa kama unahisi umetapeliwa sheria za Tz zipo wazi, fungua kesi mahakamani utajilike.
   
 10. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,420
  Likes Received: 3,768
  Trophy Points: 280
  Unakatwa hiyo hela kwa kujiunga na siyo kuongea. What happens if hizo siku tano zikapita na hujaongea??? Si wanakata hiyo hela??
   
 11. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Ni tactics za biashara tu (bundling!) na unayo haki ya kuchagua vinginevyo. Elfu tano kwa dakika mia tatu (sekunde 18,000) ni kama senti 28 kwa sekunde. Kwa jinsi voda walivyo expensive nadhani hii ni bure kwao!

  Kimsingi unapojisajiri unakuwa umenunua 'haki ya kupiga simu bure' (voda kwa voda) kwa dakika 300 ndani ya siku tano. Usipopiga simu/au ukipiga pungufu ya dakika 300 ndani ya muda huo wa siku tano unapoteza haki hiyo. Hii maana yake ni kuwa unachonunua siyo 'kiasi cha hizo dakika' bali 'haki ya kupiga simu bure'.

  Naweza kufananisha na mtindo wa buffet (soma ‘bufei’) unaotumiwa na mahoteli ambapo unanunua haki ya kula upendachacho kati ya vilivyopo mezani katika muda maalumu. Umenunua 'haki ya kula bure', sasa usipokula au ukila kidogo hiyo ni juu yako.

  Nitapeleka invoice voda kwa kuwatetea:D!
   
 12. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  But I am still not conviced that improper cummunication on the service they offer is business tactical approach???
   
 13. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Sasa hapaaaaaaaa, ujambazi si ujambazi, wizi si wizi, utapeli si utapeli.
  Unajua huu ni wizi wa kisomi. Hapo ni chaguo lako kuibiwa au kutoibiwa ndio maana wameeleza namna ya mteja anavyoibiwa. Sasa ukiendelea kulalamika si umesaini we mwemyewe mkataba wa kuibiwa sh. 5000 kwa dakika 300. Poleni sana mnaoibiwa kwa mtindo huo.

  Halafu ukishaibiwa hiyo 5000 yako hapo ujue hakuna cha VODAJAMAA. Heri yangu mimi na baadhi ya wengine tuliogharamia line ya sh.30000 halafu tunalonga kwa sh.1 tu kwa sekunde kwenda voda.
   
 14. l

  lageneral Member

  #14
  Sep 9, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau nani anamiliki jk school iliyokuwa ikimilikiwa na akina Jenerali enzi hizo za Habari corp?
   
 15. Keen

  Keen JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 620
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mfunyukuzi na wengine: Mimi nakubaliana na nanyi asilimia mia kwa mia!!! Si makampuni ya simu tu. Kuna wengine wamekuja wanasema tuma neno "MAFUTA" kwenda namba (?), du! nimeisahau upate tank la mafuta. Wizi wanaoufanya ni pale wanapoacha kwa makusudi kusema kila sms utakayotuma utachajiwa sh.ngapi. Huu si wizi jamani. Wengine wanajiita "KWANJA" nao hawasemi charge ya kila sms. Michezo kama hii ya kubahatisha nadhani kama walivyochangia wengine, sheria za mchezo lazima ziwe wazi. Mimi nadhani makapuni mengi yanayofanya michezo hii including makampuni ya simu yamegundua kuwa wabongo ni mbumbumbu wa sheria na si watu wa kujali sana. Kuna umuhimu wa kuwahoji. Unaposema huduma ya bure bila kufafanua ubure huo ukoje ni wizi mtupu!!
   
 16. O

  Omumura JF-Expert Member

  #16
  Sep 10, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Jamani hakuna haja ya kubishana, hawa jamaa ni wezi wa kutupwa.sasa hivi wamegundua kuwa mitandao yote imewapiga bao, sasa wanachofanya ni wizi wa mchana kweupeeee!bora tuachane nao tu, mie nilishatupa line ya voda haikuwa na msaada kwangu katika suala zima la mawasiliano.
   
 17. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #17
  Sep 10, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,029
  Trophy Points: 280
  Mkuu we ni mkali. Express yourself!
   
 18. GP

  GP JF-Expert Member

  #18
  Sep 10, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  stay tuned guyz,
  ule mtandao wetu wa kujiexpress unakuja na bonge moja la promosheniiiiiiiiii!. hapo lazima upoteze mitandao mingine ya ovyo ovyo. jamaa wa kujiexpress nawakubali they are so creative.
   
 19. JAYJAY

  JAYJAY JF-Expert Member

  #19
  Sep 10, 2009
  Joined: Oct 31, 2008
  Messages: 2,495
  Likes Received: 824
  Trophy Points: 280
  kweli kuna haja ya mamlaka husika kufuatilia suala hili.hizi huduma hasa za kutuma sms ni lazima viwango vyake vya gharama viwekwe wazi.tigo naona wao wameanza kurekebisha,sijui mitandao mingine.
   
Loading...