Vodacom tutendeeni haki wateja wenu. Mnapandishaje Cost 25% kimya kimya bila kutujulisha? Huu sio wizi wa mchana Kweupe? TCRA mnalijua hili?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,548
Wanabodi,

Kwa kawaida mimi huwa nanunua bando za voda weekly kwa 15,000 unapata GB 10.

Kwanza sometimes hiyo bando huwa inakata kabla hata wiki haifika na nikifanya assessment ya matumizi yangu, GB 10 huwa haijafika, lakini kwa sababu huwa nawasha tethering silalamikii kuibiwa.

Monday nimenunua bando yangu ya 10 GB, sijashare, sija download, nime upload few clips hazifiki hata 2 GB, japo kuna siku nilipitiwa usingizi simu ilikaa jf 24/7, leo naamka na sms ya bando imekata!

Ni katika ku recharge bando ya 15,000 leo inauzwa 20,000!. Nikacheki bando nyingine zote zimepandishwa kwa 25% increase! Mbona hatukuambiwa?

Hivi makampuni ya simu yanajipandishia tuu bei kiholela na regulator yupo, hii imekuaje?

Kumetokea changes gani kwenye shilingi ya Tanzania against US. $ kusababisha such increase ya 25%?!

TCRA tusaidieni jamani haya makampuni mengine ya simu, sio yanatunyonya, yanatunyonga!

NB. Kwa vile media ni nyingi kama walitangaza nyongeza hii mimi ndio sikuiona, mtanisamehe bure.

P.
 
Kaka hata mimi naunga la week kwa elfu 15 sasa naona ni 20 pakubwa hapa nimeamua kwa sasa naunga social pack ya tigo kwa mwezi halafu hiz download kubwa nasubiri night na halotel au ttcl maisha yanaenda nishaacha kununua bando voda.
 
VODA wameingia ubia wa utunzaji wa mazingira na WWF, wametoa mahela mengi sana huko na kama ilivyo kawaida ya mfanya biashara hakuna kukubali hasara sasa wateja ndio watafidia huo udhamini na sio kufidia tu pia kujinyakulia faida ya kutosha, kazi ni kwetu kama wanavyo jinasibu.
 
Rudi nyumbani mkuu.

Screenshot_20190821-105020.jpeg
 
TCRA wamelala sana, kuna masuala mengi sisi kama watumiaji tunaonewa na hii mitandao, lakini wao wapo kimya, sijui kazi zao ni nini hasa. Kiuhalisia hata haya mabando, wanaweza kukuambia ni GB 10 kumbe ni GB 8, mamlaka hata hazijali kwa wizi huu
Na speed pia!
 
Back
Top Bottom