VoA: Lissu aomba Rais Magufuli kufanya maridhiano na wapinzani wake

Securelens

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
316
541
Katika mahojiano aliyofanya leo na VOA, Lissu amekiri kuwa Watanzania wamempuuza kwa kutokuandamana pamoja na yeye kutoa wito huo kwa nguvu zote.

Amesema hata kabla ya uchaguzi aliwahimiza watanzania kuwa tayari kuingia barabarani lakini bado haikusaidia, Watanzania walimgomea. Ametulaumu watanzania kuwa hatujawa tayari kwa mabadiliko.

Alipouulizwa akikutana na Rais Magufuli kwa sasa atamwambia ujumbe gani. Kwa unyenyekevu huku akimwita 'Mheshimiwa Rais Magufuli' na siyo tu kumwita casually Magufuli alivyozoea kumwita, Lissu amemwomba akubali kusamehe akitumia neno 'arudi nyuma' na akubali maridhiano na kusema hapendi kutumbukia kwenye shimo. Unaweza kusikiliza mahojiano hayo kupitia VOA ya tarehe ya leo.




===========

MTANGAZAJI: Safari yako ya kwenda hapo Ubelgiji imeibua hisia mseto, hebu tueleze umefikaje na kwanini?

LISSU: Nimefika Ubelgiji jana asubuhi nikitokea Tanzania ambako niliondoka juzi mchana na nimeondoka kwa sababu usalama wangu ulikuwa mashakani. Tangu baada ya uchaguzi nilianza kupata vitisho kwenye simu kwamba kuna amri imetolewa ya kunimaliza na kwa mtu ambae nimepitia niliyoyapitia mie ya kushambuliwa kwa risasi na karibu kuuliwa miaka mitatu iliyopita, hivi vitisho nilivipa uzito mkubwa sana na kwahiyo nilifanya jitihada ya kwanza kujificha na baadae nilikimbia ubalozi wa Ujerumani ambako nilikamatiwa nje na polisi lakini baadae maafisa wa kibalozi waliingilia kati na nikaachiliwa a baadae nikakaa kwa balozi wa Ujerumani nchini Tanzania kwa siku nane mpaka nlipoondoka kuja huku.

MTANGAZAJI: Kuna swali limeulizwa kwenye mitandao ya kijamii hivi leo kwamba mheshimiwa Lissu atahutubia Bunge la Jumuiya ya umoja wa Ulaya, zungumzia hilo, ni kweli si kweli!

LISSU: Mimi napenda sana kukaribishwa kuhutubia vikao kama hivyo lakini hili linalozungumzwa mitandaoni ni porojo tu za mitandaoni, mimi sijaomba wala kuombwa kuhutubia kikao chochote cha Bunge la Ulaya kwa hiyo hayo ni mambo ya kutunga ya mitandaoni tu na wanayoyatunga wana sababu zao.

MTANGAZAJI: Kwa wale wanaosema Tundu Lissu amteroka Tanzania, ameachiwa wengine kufanya kazi, labda arejee tena kuwania Urais, ungewaambia nini? Wanaona kama ni kusaliti labda ungekaa nao mpambane pamoja. Msukumo uliokuwa umetangaza wewe na viongozi wengine wa kisiasa kwamba watanzania watokee kwa wingi kwenye barabara za Tanzania kupinga matokeo ya uchaguzi, msukumo huo bado upo? Kama upo i nini hasa kwa mawazo yako iwe hatma yake.

LISSU: Sijatoroka kama nilivyosema nimeondoka Tanzania mchana kweupe, nimepitia uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, nimepita kwa passport ya Tanzania niliyopewa na serikali siku ya Jumatatu, kwa hiyo sijatoroka lakini nilichofanya nimeondoka ili kuokoa maisha yangu. Sasakwa watanzania wenzangu sharti wafahamu kwamba ni muhimu kuendelea kuishi ili niweze kupambana kesho na keshokutwa, nikikaa nikauawa basi safari ya mapambano yakwangu angalau itakuwa imeishia hapo na mimi nataka niendelee na mapambano ya kudai demokrasia, ya kudai nchi ambayo tunastahili na inabidi ili niendeleze mapambano inabidi niwe hai, inabidi kukimbia kujiokoa ili kuishi na kupigana siku nyingine, ndicho nilichofanya.

Hatma ya siasa za Tanzania, ni wazi wito wa kupinga matokeo ya uchafuzi uliofanyika tarehe 28 Oktoba haukuitikiwa na watanzania, nilisema wakati wote wa kampeni endapo uchaguzi na watawala wa sasa, wananchi wachukue hatua ya kulinda demokrasia yao wao wenyewe na ndichi nilichofanya niliitisha watu wajitokeze kuchukua hatma ya nchi yao kwenye mikono yao, hawakufanya hivyo sio kwa sababu mimi sikutoa wito, inaelekea kwasababu wananchi hawako tayari kupambania haki zao kwa hiyo tuendelee siku zijazo. Kwa tafsiri yangu tu, kwa hii miaka mitano iliyopita, miaka mitano ijayo itakuwa migumi sana kwa nchi yetu kwa kuzingatia aina ya mtawala ambae tunae, Rais Magufuli amedhihirisha wazi jinsi ambavyo ni mtawala katili, asiyejali demokrasia, haki za binadamu, uchumi wa nchi yetu na kwahiyo miaka mitano inayokuja itakuwa miguma sana kwa watanzania wa kila aina.

MTANGAZAJI: Kuna wito mliotoa kwa jumuiya ya kimataifa iafanye juu chini mnapata haki na uchaguzi haukufanyika ambavyo mlitarajia ungefanyika, swali langi ni hasa katika jumuiya ya Afrika Mashariki katika ujirani huo wa Tanzania, unaweza kusema wamefanya vya kutosha kushinikiza ama kuwasaidia kwamba mnapata haki kama ambavyo mliuliza.

LISSU: Jumuiya ya Afrika Mashariki haijafanya kile ambacho ilitakiwa ikifanye kwa maana ya kwamba mimi nafahamu na nafahamu kwa sababu nilizungumza na waangalizi wa umoja wa Afrika ulioongozwa na Goodluck Jonathana na waliniambia wao pamoja na waangalizi wa EAC walishuhudia matukio mengi ya ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi kwa namna ambayo wasingeweza kusema uchaguzi huu ulikuwa huru wala wa haki kwa yale ambayo wao wenyewe waliyashuhudia a kuyapiga picha masanduku ambayo yalikuwa yameshajazwa kura na kuwekwa kwenye vituo vya kupigia kura kabla zoezi la kupiga kura halijaanza. Sasa ripoti waliyotoa EAC inasema kwamba uchaguzi ulikuwa huru na haki ni ripoti ya uongo, hatukutegemea kwamba waangalizi hawa wangeweza kuzungumza hivyo baada ya kushuhudia hayo ambayo tunaambiwa waliyashuhudia lakini tusistaajabu sana, Jumuiya ya Afrika Mashariki inaundwa na nchi gani na zinaongozwa na watawala wa aina gani ukiachia Kenya ambayo demokrasia yake iko mbele zaidi katika hiyo Jumuiya, nchi nyingine zote zilizobaki ndio hizo za kina Museveni, Rais wa maisha, Generali Kagame, Rais wa maisha, Burundi ndio hivyo tena na Magufuli anaelekea kuwa Rais wa maisha. Wengine tunasubiri ripoti ya AU.

MTANGAZAJI: Mwisho, kama ungepata nafasi ya kukutana na Rais John Magufuli hivi leo, ungemwambia nini?

LISSU: Ningemwambia mheshimiwa Rais itisha mkutano wa kitaifa wa maridhiano tutengeneze nchi ambayo makundi mbalimbali ya kisiasa yataridhiana, tuwe na nchi ambayo itakuwa na umoja wa kitaifa, huko unakoelekea unaenda kututumbukiza sisi wote katika shimo kubwa na nchi yetu inaweza kuangamia, rudi nyuma, fanya maridhiano tujenge nchi kwa pamoja, tujenge nchi ya kidemokrasia na nchi ambayo itakuwa sehemu ya Jumuiya ya kimataifa, sisi tunahitaji dunia zaidi kuliko dunia inavyotuhitaji, usifikiri kwamba unaweza kuishi peke yako katika dunia hii ambayo kila mtu anahusiana na mwingine.

MTANGAZAJI: Nikushukuru sana Tundu Lissu kwa kuzungumza na sauti ya Amerika

LUSSU: Asante sana kaka BMJ kwa kunipa nafasi hii

----MWISHO----



My take:
Lissu ameshaelewa kuwa Watanzania wamemshtukia na wanampuuza.

Amesalimu amri na ameanza kulegea na sasa anaanza kulialia na kuomba maridhiano. Kwa mara ya kwanza anaanza kuimba wimbo wa maridhiano.

Tuombe uzima, tutaona upande mwingine wa shilingi kwa huyu Tundu Lissu. Wana CHADEMA bakini na maneo ya akiba, muda si mrefu mtabadilisha majina yenu ya JF na kukimbia jukwaa.
 
Swaga za Lumumba!

Acha kupotosha! Kaulizwa nini angemshauri Magufuli na ndio akajibu angemshauri yafanyike maridhiano na hili la maridhiano haliajaanza kuzungumziwa leo. Au wewe mtu kutoa ushauri kama alivyotakiwa ndio kulegea?

Alafu mbona hujaongelea aliposema utawala huu kuwa ni wa kikatili na akaonya miaka mitano ijayo itakuwa migumu zaidi?

Mbona hujaongelea aliposema kakimbia kuokoa maisha yake ili aendeleeze mapambano?

Kasema wazi ni bora aendelee kuwa hai ili aendeleze mapambano kwani akifa hatoweza kuendeleza mapambano na ndio maana aliona ni bora kwanza awoke maisha yake ili apate nafasi ya kuendelea mapambano.
 
Lissu kachezea za uso Hana hamu na watz , kweli wananchi ni wajumbe waliochangamka , wanamwambia tupo pamoja kwenye sanduku wakamchinja na bado kwenye maandamano wakamkick,-out , mwamba akaona aamshe mamtoni....
 
Matokeo ya kusomea chini ya miti viti vikiwa mawe na matofali. Ni ngumu sana kuelewa hata unachosikia.
 
51 Reactions
Reply
Back
Top Bottom