Vladimir Putin: Niliendesha magari na teksi ili kujikimu kimaisha miaka ya 1990

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,037
20,333
Rais wa Urusi Vladimir Putin amezungumzia majuto yake kuhusu kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti mwaka 1991, akifichua kwamba alilazimika kufanya kazi ya udereva wa teksi ili kujiongezea kipato.

Matatizo ya kiuchumi yaliyosababishwa na kuanguka kwa muungano huo yaliwalazimisha Warusi wengi kutafuta njia mpya za kupata pesa.

Bw Putin alielezea kuvunjika kwa nchi hiyo kama kuporomoka kwa Urusi ya kihistoria.

Matamshi hayo yanaweza kuchochea uvumi kuhusu nia yake kuelekea Ukraine, jamhuri ya zamani ya Usovieti.

Urusi imekusanya zaidi ya wanajeshi 90,000 kwenye mpaka wake na Ukraine na kuna hofu kwamba inapanga kuivamia.

Urusi inakanusha hili, ikiishutumu Ukraine kwa uchochezi na kutafuta hakikisho dhidi ya upanuzi wa Nato kuelekea mashariki.

Matamshi ya Bw Putin yanatoka katika filamu ya hali halisi iitwayo Russia, Latest History, iliyopeperushwa Jumapili.

"Ilikuwa ni mgawanyiko wa Urusi ya kihistoria chini ya jina la Umoja wa Kisovieti," alisema, akiongeza kuwa katika nchi za Magharibi iliaminika kuwa kusambaratika zaidi kwa Urusi ni suala la wakati tu.

Inajulikana kuwa Bw Putin anaona kuanguka huko kuwa janga lakini matamshi yake kuhusu matatizo yake ya kibinafsi wakati huo ni mapya.

"Wakati mwingine nililazimika kupata pesa za ziada," alisema. "Namaanisha, kupata pesa za ziada kwa gari, kama dereva wa kibinafsi. Haipendezi kuzungumzia haya kwa kweli, lakini kwa bahati mbaya ndivyo ilivyokuwa."

Wakati huo, teksi zilikuwa adimu nchini Urusi, na watu wengi katika magari ya kibinafsi walikuwa wakiwabeba watu wasiowajua kwenye magari yao ili kuwasaidia kujikimu. Wengine wangetumia hata magari ya kazini kama vile ambulensi kama teksi.

Bw Putin anajulikana kuwa ajenti wa zamani wa idara ya usalama ya Soviet, KGB.

Walakini, mwanzoni mwa miaka ya 1990 alifanya kazi katika ofisi ya Meya wa St Petersburg Anatoly Sobchak. Anashikilia kuwa alijiuzulu kutoka kwa KGB baada ya mapinduzi ya Agosti 1991 dhidi ya Rais wa Soviet Mikhail Gorbachev ambayo yalisababisha kuvunjika kwa USSR.

Kuyasimamisha magari ya teksi yaliyojulikana kama 'bombila'

Nilichukua basi likirejea kwenye depo yake usiku mmoja lakini niligundua jambo kwenye ambulensi hiyo... Haya yalikuwa baadhi tu ya magari ambayo nilipata yakifanya kazi ya ziada kama teksi katika Urusi ya miaka ya 1990 .

Kila kijana wa Kirusi niliyemjua huko Moscow wakati huo alionekana kuzitumia na, hatimaye, kila mwanamume wa familia ya Kirusi aliye na gari alionekana kufanya kazi kama kama bombila (mshambuliaji), jina la utani la madereva wa teksi zisizo rasmi.

Nilipofika Urusi kama mwanafunzi mwaka wa 1989 kulikuwa na sheria mbili tu ambazo hazijaandikwa: usiingie kwenye gari lenye zaidi ya mtu mmoja ndani yake na ukubali nauli kabla ya kuanza safari. Hakukuwa na teksi rasmi za kutosha. Kwa kawaida hatari kubwa uliyokimbia ilikuwa kumkera dereva kwa kujaribu kufunga mkanda wa usalama.

Wakati USSR ilipoanguka mwaka 1991 na sarafu yake ikapoteza thamani yake, soko lisilo rasmi liliongezeka na unaweza kujikuta unabebwa na watu kutoka kila aina ya maisha.

Mara kwa mara nilikuwa na mazungumzo ya kuelimisha na madereva lakini mara nyingi kimya cha aibu kilikuwa kikishuka, labda kwa sababu dereva aligundua kuwa anaweza kunilipisha zaidi baada ya kuchelewa kugundua kuwa mimi ni mtu kutoka Magharibi, lakini labda pia kwa sababu wanaweza kuwa na aibu kwa kutumia wakati bora wa maisha yao "kupiga kazi ya teksi " badala ya kutafuta kazi na maisha waliyokuwa wamepanga.
 
Hata hapa KWETU hali ilikuwa hivyohivyo tu tena ilikuwa mbaya zaidi..

Tena sisi tuna bahati mbaya zaidi maana 2015 - 2020 ilijirudia Tena.
Kwamba mmoja alitaka tuishi kama mashetani.
Mkuu Covid kwa hivyo ulivyobambiwa sisi utamwambukiza mwenzio,na pia mwacheni mzee wa watu apumzike kwa amani maana kila lawama anatupiwa yeye, tuambie sasa ni nani aliyeishi kama shetani ,?😁
 
Hata hapa KWETU hali ilikuwa hivyohivyo tu tena ilikuwa mbaya zaidi..

Tena sisi tuna bahati mbaya zaidi maana 2015 - 2020 ilijirudia Tena.
Kwamba mmoja alitaka tuishi kama mashetani.
Unamsema nani huyo?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom