Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,875
Taarifa nilizozipata haraka sasa hivi ni kuwa watu wengi sana wanahisiwa kufa maji baada ya kivuko kubinuka juu chini, chini juu katika kisiwa cha UKARA wilayani Ukerewe.


Capture.PNG

Dnjvqu3X0AAoBIC.jpg large.jpg

Wakazi wa Ukerewe wakiwa mita chache kutoka kivuko kilipozama​

====
Taarifa Kwa Umma Kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme-TEMESA Kuhusu Kuzama Kwa Kivuko Cha MV.Nyerere

Dnip_wvX0AADKuS.jpg

Kivuko cha MV Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorara na kisiwa cha Ukala katika ziwa Victoria kimezama huku taarifa za idadi ya watu waliokuwemo ndani ya kivuko hazijajulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana amesema kivuko hicho kimezama wakati kikielekea katika Kisiwa cha Ukara. Kiliondoka saa 6 mchana na ilipofika saa nane kamili mchana kilipinduka.

Amesema bado hawajapata idadi kamili ya waliokuwemo kwenye kivuko hicho.

Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Hassan Karonda amekiri kuzama kwa kivuko hicho na yuko njiani kulekea huko na watatoa taarifa baadaye.

Kivuko cha MV. NYERERE kilinunuliwa na kuanza kutoa huduma mwaka 2004. Kilifungwa injini mbili mpya zenye thamani ya shilingi milioni 191 JULY 2018. Kivuko cha MV. Nyerere kina uwezo wa kubeba tani 25 sawa na abiria 100 na magari 3 kwa wakati mmoja.



DnitYLXWwAEDLUS.jpg

UPDATES: 1900HRS

=> Watu watano wamekufa na wengine 32 wameokolewa mpaka sasa ila hali zao ni mbaya kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere.

=> "Mtu Hajalipwa Mshahara Halafu Anasikia Trilion 1 Imepotea Inauma" -Joseph Mkundi

Mbunge Joseph Mkundi akitahadharisha kuhusu kivuko cha MV Nyerere Apr 24, 2018

Alikuwa akichangia hoja ya bajeti ya Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano iliyopo chini ya Waziri wake, Profesa Makame Mbarawa.

UPDATES:

Rais Magufuli atuma salamu za Rambirambi

"Nimeshtushwa na kusikitishwa sana na ajali ya MV Nyerere, nawapa pole wote waliopoteza jamaa zao na nawaombea wote walionusurika kupona haraka, kwa wakati huu nawaomba tutulie wakati juhudi za uokoaji zinaendelea"


AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE: WATU 44 WAMEFARIKI, ZOEZI LA UOKOAJI LASITISHWA HADI KESHO

Mbali na idadi hiyo ya waliofariki, Watu 37 wameokolewa katika ajali huku hali zao zikiwa mbaya

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema zoezi la uokoaji limesitishwa kutokana na giza kuingia


10:40 - MIILI 86 IMESHAOPOLEWA MPAKA SASA
Idadi ya vifo katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere, Mwanza imefika watu 86 huku uokoaji ukiendelea, RC John Mongella amethibitisha

11:41 - IDADI YA WALIOOPOLEWA YAFIKA 94
Idadi ya vifo katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere, Mwanza imefika watu 94 huku uokoaji ukiendelea, RC John Mongella amethibitisha

11: 43 Chanzo cha kuzama kwa mujibu wa DC wa Ukerewe
DC Ukerewe amesema kivuko kilikuwa kimebeba zaidi ya abiria 400, kilivyokaribia kufika mwaloni(kutia nanga) nahodha akapunguza spidi hivyo abiria wakakimbilia upande wa kushukia ili wawahi kutoka, kivuko kikazidiwa uzito na kupinduka.

12:40 - MIILI ILIYOOPOLEWA YAFIKA 100
Miili ya waliokufa na kuopolewa mpaka sasa yafika 100.

12:49 - IGP SIRRO: UTAMBUZI WA MAREHEMU UNAENDELEA
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simoni Sirro amesema utambuzi wa marehemu katika ajali ya MV Nyerere mkoani Mwanza unaendelea kwa miili iliyoopolewa.
Litafunguliwa Jalada maalum la kuchunguza tukio la kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere

13:03 - Idadi ya miili iliyoopolewa yafika 125
Idadi ya miili iliyoopolewa kwenye kivuko cha Mv Nyerere imefikia 125 mpaka sasa

13:20 - WAZIRI ISACK KAMWELWE: ZOEZI LA KUOPOA MIILI ILIYOKWAMA LITAKAMILIKA SAA 12 JIONI LEO
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema shughuli ya uokoaji wa watu walionasa kwenye kivuko cha MV Nyerere inatarajiwa kukamilika leo saa 12 jioni

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema mazishi ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya Mv.Nyerere iliyotokea Septamba 20 huko kisiwani Ukara, Ukerewe mkoani Mwanza yatakuwa ya kitaifa ambapo viongozi wakuu wa kitaifa wanatarajia kushiriki mazishi hayo.

17:21 - MIILI ILIYOOPOLEWA YAFIKA 126
Waliofariki dunia ajali ya kivuko wafikia 126, miili 36 imeshatambuliwa na ndugu zao

17:46 - MIILI ILIYOOPOLEWA YAFIKA 131
Kwa mujibu wa Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Isack Kamwelwe idadi rasmi ya vifo mpaka jioni hii kutokana na ajali ya MV Nyerere ni watu 131.

18:10 - IDADI YAFIKA 136
Afisa mkuu wa Polisi Tanzania, Simon Sirro anasema kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na mkasa huo imefikia 136

18:15 - TAMKO LA SERIKALI (Katibu Mkuu Kiongozi)
Rais Magufuli ameagiza kuwa kufuatia ajali ya MV Nyerere Bendera ya Taifa itapepea nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia kesho Septemba 22, 2018.

Rais Magufuli ameagiza viongozi wa taasisi na mamlaka zinazosimamia usafiri wa majini wahojiwe na watakaobainika kuhusika kwa uzembe wachukuliwe hatua kali.

18:30 - Waziri Mkuu Majaliwa, CDF Mabeyo wawasili Ukerewe
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na CDF Mabeyo wamewasili Ukerewe na wamepokelewa na RC Mongella na IGP Sirro.

20:00 - NAHODHA WA KIVUKO ANASHIKILIWA KWA UCHUNGUZI
Nahodha wa MV Nyerere anashikiliwa na vyombo vya ulinzi kwa kosa la kumuachia mtu asiye na uwezo(Deiwaka) kuendesha kivuko na yeye kutosafiri.

Taarifa ya Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza siku 4 za maombolezo kuanzia leo tarehe 21 Septemba, 2018 kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere katika ziwa Victoria na kusababisha vifo vya watu 131 waliothibitika mpaka sasa.

Kivuko hicho kilipinduka na kisha kuzama majini jana mchana meta chache kabla ya kufika katika kisiwa cha Ukara kikitokea kisiwa cha Bugolora ambapo mpaka sasa watu 40 wameokolewa wakiwa hai, miili 131 imeopolewa na zoezi la uokoaji linaendelea.

Pamoja na kutangaza siku 4 za maombolezo Mhe. Rais Magufuli amewapa pole wote waliopoteza jamaa zao katika ajali hiyo, amewaombea majeruhi wapone haraka na amewapongeza viongozi wa Mkoa wa Mwanza, vyombo vya ulinzi na usalama na wananchi wote wanaoendelea kushiriki katika uokoaji.

“Kwa masikitiko makubwa nawapa pole wote waliopoteza jamaa zao katika ajali hii, huu ni msiba mkubwa uliolikumba Taifa letu, nawaomba Watanzania wote kwa wakati huu ambapo vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na wananchi wanaendelea na uokoaji tuwe watulivu na tuendelee na kushikamana kama ilivyo desturi yetu, huu sio wakati wa kulumbana na kukatishana tamaa” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania kuwapuuza wanaotaka kutumia ajali hii kujipatia umaarufu wa kisiasa, na amebainisha kuwa ni vema Watanzania wote tuungane kuwaombea Marehemu wapumzike mahali pema, majeruhi wapone haraka na kuwatia moyo wote wanaoendelea na zoezi la uokoaji.

Mhe. Rais Magufuli amemtuma Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kwenda eneo la tukio, ameagiza kuundwa tume ya uchunguzi wa chanzo cha ajali hii na ameagiza wote waliohusika kusababisha ajali hii wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

“Taarifa za awali zimeonesha dhahiri kuwa kivuko cha MV Nyerere kilikuwa na idadi kubwa ya watu na mizigo kupita uwezo wake, kama kuna mtu yeyote mwenye ushahidi wa chanzo chochote cha ajali hii, tunatarajia kuwa ataupeleka mahakamani” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

21 Septemba, 2018

UPDATES: 22 SEP 2018

0845hrs: Miili 15 yaopolewa

Miili mingine 15 imeepolewa leo asubuhi na kufanya idadi ya vifo katika ajali ya MV. Nyerere kufika 151.

0820HRS: Nahodha na Mkuu wa Kivuko cha MV Nyerere ni miongoni mwa watu waliofariki

Nahodha na Mkuu wa Kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi kikiwa safarini kutoka kisiwa cha Bugorora kwenda Ukara wilayani Ukerewe, Mwanza, ni miongoni mwa watu waliofariki dunia katika ajali hiyo.

1100hrs: Idadi ya miili iliyoopolewa yaongezeka

Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi mchana Septemba 20, 2018 imefikia 157 huku uokoaji ukiendelea.

1115hrs: MHANDISI WA KIVUKO APATIKANA AKIWA HAI

Mhandishi wa kivuko #MVNyerere, Alphonce Charahani ameokolewa akiwa hai siku 2 baada ya kivuko kuzama, amekutwa akiwa amejipaka oili mwilini. Sasa majeruhi wafikia idadi ya 41.

1117hrs: Serikali kugharamia kusafirisha maiti hadi hospitali ili zitambuliwe na kutoa TSH 500,000 kwa kila familia iliyofiwa

11:26 - Mbunge wa Ukerewe: CHANGAMOTO NILIZOWASILISHA BUNGENI ZILITATULIWA
Mbunge wa ukerewe amesema changamoto za kivuko alizowasilisha bunge zilitatuliwa miezi miwili iliyopita, kilikuwa sawa na kilikuwa mbioni kubadilishiwa ratiba ikiwemo kuongeza idadi ya safari ili kukidhi mahitaji ya wananchi wa eneo hilo.

12:00 - MIILI 163 IMEOPOLEWA
Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya kivuko cha Nyerere imefikia 163 baada ya miili mingine 27 kuopolewa leo.

12:16 - WAZIRI UMMY MWALIMU: TUACHE KUSAMBAZA PICHA ZA MAREHEMU
"Ndugu zangu Watanzania, ninawaomba sana TUACHE KUSAMBAZA NA KUPOSTI PICHA ZA MAREHEMU WA AJALI YA MV NYERERE. Tuheshimu Utu na Ubinadamu wao"

12:19 - MIILI 116 YA WALIOFARIKI YATAMBULIWA

1250hrs: Wananchiwa Ukerewe wakosa Usafiri wa kwenda Ukara

Zaidi ya wananchi 500 wamekwama katika eneo la Bugolora baada ya kukosa usafiri wa kuelekea kisiwa cha Ukara kulikotokea ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere juzi Septemba 20, 2018.

1330hrs: Idadi ya waliopoteza maisha yaongezeka.

Miili mingine 33 imeepolewa na kufanya idadi ya vifo katikia ajali ya kivuko cha MV Nyerere kufika 196. Uokoaji unaendelea.

1600hrs: Meli yenye Vifaa Maalum yaelekea kwenye tukio

Meli ya MV Nyehunge kutoka Mwanza inaelekea kisiwa cha Ukara ikiwa na vifaa maalum vitakavyotumika kukinyanyua kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi.

17:30 - Miili iliyoopolewa yafika 209
Kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali, Idadi ya miili iliyoopolewa katika ajali ya Kivuko cha MV Nyerere mpaka sasa imefikia 209. Katika idadi hiyo miili iliyotambuliwa na ndugu na jamaa ni 172

17:45 - SERIKALI YATANGAZA KAMATA KAMATA YA WANAOTOA TAKWIMU ZA UONGO
Kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola imesema kuwa itatumia #SheriaYaTakwimu kuwakamata na kuwafikisha Mahakamani wote watakao fanya kosa hilo

20:25 - Miili iliyoopolewa yafika 218
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amesema miili 218 imeopolewa katika ajali ya MV Nyerere huku 171 kati ya hiyo ikitambuliwa. Kazi ya uopoaji itaendelea kesho

UPDATES: 23 SEP 2018

0800hrs: Siku ya tatu baada ya ajali, Miili mingine yapatikana.

Miili mingine 7 imeepolewa leo asubuhi na kufanya idadi ya vifo katikia ajali ya kivuko cha MV Nyerere kufikia 224, RC wa Mwanza

1220hrs: Ibada ya mazishi ya marehemu ambao hawajatambuliwa na wale waliombwa na ndugu kuzikwa na Serikali
IMG_20180923_125907.jpg

Miili 9 imewasili katika makaburi ya viwanja vya shule ya sekondari Bwisya kwaajili ya maziko ya Kitaifa yatakayoongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, makaburi zaidi ya 80 yamechimbwa kwa sababu mpaka sasa kuna miili ambayo inaibuka kutoka majini.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isaac Kamwele anasema; Waliofariki 223 wanawake 126, wanaume 71 watoto wa kike 17,watoto wa kiume 10.

4 Hawajatambuliwa. Wamachukuliwa DNA. Watano waliotambuliwa watazikwa na ndugu hapa. Jumla watazikwa tisa.

Wananchi wa Ukara waliokoa 40 wakiwa hai. Kivuko kilibeba watu 265,uwezo wake ni kubeba abiria 101.

Milioni 190 zimechangwa na wananchi

Serikali imeweka utaratibu mzuri wa kujenga mialo na kununua vivuko vilivyo salama

1320hrs: Waziri Mkuu Majaliwa anasema;

Rais Magufuli amepokea habari ya ajali hii kwa mshituko.

Ajali ya kivuko hiki imesababishwa na kivuko kubeba abiria wengi na mizigo mingi.

Taarifa za awali zinaonyesha abiria zaidi ya 260 walikuwa ndani ya kivuko hiki.

219 imetambuliwa na miili 214 imetambuliwa na kuchukuliwa na ndugu. Minne tutaizika hapa ikiwemo mitano iliyotambuliwa ila ndugu wameamuwa wazikwe hapa.

Serikali itachukua hatua ya kuunda tume ya wachunguzi wakiwemo wataalam ili kubaini chanzo na wote waliohusika watachukuliwa hatua.

Meli ya MV Nyahunge imeletwa kuendelea kutoa huduma.

Tayari tumewakamata maafisa wote walikuwa wanahusika na usalama wa majini.

Kuanzia tarehe 21-24 imetangazwa kama siku ya maombolezo na bendeza zitapepea nusu mlingoti.

Tumefungua account ya MV Nyerere namba 3111005726. Itakumika kujenga wigo na mnara wenye majina ya wote waliofariki.

Tutaivuta meli kuileta mwaloni. Tutaendelea na mazishi pale tutakapopata mwili mwingine, nami ntaendelea kubaki Ukara kusimamia zoezi hili.
Kwa niaba ya rais natoa pongezo kwa John Mongera Mkuu wa mkoa wa Mwanza kwa jinsi mlivyoshughulikia kazi hii. Kamwele, Muhagama nawashukuru kwa uratibu. Namshukuru Kigoma Malima, Venance Mabeyo, Vikosi vya uokoaji JWTZ na Zanzibar, Jeshi la wanamaji, Msalaba mwekundu, Jeshi la akiba la Mgambo na wananchi wa kisiwa cha Ukara. Tunashukuru Madaktari wauguzi na manesi, nashukuru Vyombo vya habari. Nawashukuru Viongozi wa dini. Tunawashukuru Wasanii kwa kutunga nyimbo za kufariji na kuwatuliza watanzania. Nawashukuru Viongozi wa Nchi mbalimbali kwa kutufikishia salamu za pole. Nawashukuru wote kwa niaba ya mheshimiwa rais.

Katika kuimalisha usafiri majini, Serikali imeendelea kuongeza vyombo. Ziwa Victoria serikali imeanza kujenga meli ya kwenda Kagera, na Vivuko vipya vya Ukara na Bugolora.

Serikali itaendelea kuimalisha usafiri mwingine sehemu nyingine.

Taifa lipata msiba mkubwa sana, wito wetu ni tushikamane. Ni majonzi makubwa sana,wafiwa wanahitaji faraja. Tujipe moyo kiwa ni mapenzi ya Mungu.

Tuendelee kumuomba mwenyezi Mungu aendelea kuwaponya majeruhi wote na awalaze marehemu wote mahali pema peponi Amina.

1344hrs: Namba ya Michango yatangazwa

Jenista Muhagama anatangaza namba ya tigo pesa ya kutoa mchango. Namba imesajiliwa kwa jina la RAS Mwanza. 0677030000

1347hrs: Inaendelea dua ya kuwaombea waliotangulia mbele ya haki

1400hrs: Majeneza yanaanza kuingizwa kwenye Makaburi. Haya ni mazishi ya pamoja ya miili 9, shughuli hii inaongozwa na Waziri Mkuu Majaliwa.

10:00 (24/09/2018) - Mwili mmoja wa mtoto umeopolewa na kufanya idadi kufikia 225
Mwili mmoja umeopolewa leo katika Ziwa Victoria na kufanya idadi ya waliokufa kwenye ajali ya MV Nyerere kufikia 225

10:54 (24/09/2018) - Miili miwili yaonekana ikiwa inaelea
Waziri wa Ujenzi Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kuna miili mingine miwili imeonekana muda huu ikielea juu ya maji

10:40 (25/09/2018) - Mwili mmoja wa mtoto umeopolewa na kufanya idadi kufikia 227
Mwili wa mtoto mmoja umeopolewa leo katika Ziwa Victoria na idadi ya waliokufa kwenye ajali ya MV Nyerere kufikia 227

10:30 (26/09/2018) - Mwili mwingine umeopolewa eneo la ajali
Mwili mwingine umeopolewa asubuhi hii kwenye eneo palipotokea ajali na kufanya jumla ya miili 228 mpaka sasa.

1212hrs (27/092018) - Mwili wa mtoto wa kike waopolewa
Mwili wa mtoto wa kike waopolewa wakati zoezi la kukinasua kivuko cha MV.Nyerere likiendelea katika eneo la Bwisya Ukara, nakufanya idadi ya waliopoteza maisha kufikia 229.

1212hrs:

Hatimaye kivuko cha Mv Nyerere kilichopinduka Septemba 20 kimenyanyuliwa
 
Kagame Mourns Victims of Tanzania Ferry Disaster

President Paul Kagame has sent a condolence message to the families of the victims of Thursday disaster in which a ferry capsized in Lake Victoria and claimed lives.

“Our deepest condolences to the families and loved ones of the victims of the Lake Victoria ferry accident. Our thoughts are with you. We cannot thank the rescuers enough,” President Kagame posted on his Twitter handle.

Kagame.PNG

Source: Kagame Mourns Victims of Tanzania Ferry Disaster

---
The death toll in a ferry capsize in Lake Victoria climbed to 126 on Friday, as Tanzanian rescue workers pressed on with the search to find scores more people feared drowned.

The MV Nyerere may have been carrying as many as 200 passengers -- double the ferry's capacity -- when it capsized close to the pier on Ukara Island on Thursday, according to reports on state media.

Death toll from Tanzania ferry tragedy hits 126:

-----
President of The Republic of Kenya - Uhuru Kenyatta
On behalf of the people of Kenya and on my own behalf, I express our most sincere condolences to my brother President @MagufuliJP and our dear neighbour of the United Republic of Tanzaniafollowing the tragic capsizing of MV Nyerere in the Lake Victoria Waters.

-----
Raila Amolo Odinga
I send sincere and heartfelt condolences to families who lost loved ones in the MV Nyerere tragedy in Tanzania. I mourn with the people of Tanzania at this very difficult moment. May God grant peace and strength to the families, the care givers and the Tanzanian nation.

-----
President of the Republic of Uganda - Yoweri Museveni
I have heard of the tragic accident on Lake Victoria where the MV Nyerere ferry capsized, drowning over 100 people. On behalf of the people of Uganda and on my own behalf, I express our condolences to H.E J. Pombe Magufuli & the people of the Republic of Tanzania upon this loss.

-----
Tanzanian ferry sinks in Lake Victoria, rescue underway


Scores of people are feared dead after a Tanzanian passenger ferry in sunk in Lake Victoria Thursday afternoon.

The MV Nyerere capsized at around 2pm local time on its way to Ukora Island, two hours after departing from Bugolora, Ukerewe Island, Mwanza Regional Police Commander, Mr Jonathan Shana said.

The ferry is believed to have had hundreds of people on board, though officials are yet to confirm the number of passengers.

No casualty numbers have been given but a local media had reported that five people died and 102 rescued.

Locals joined emergency teams in rescue efforts.

The Tanzania Electrical, Mechanical and Electronics Services Agency (Temesa), which operates ferry services, said the MV Nyerere did not have any mechanical problems because heavy maintenance had been carried on it in recent months including overhauling two engines.

Officials records show the ferry was purchased in 2004 for Tsh191 million and renovated in July this year.

It has a capacity of 100 passengers and about 25 tonnes of cargo.

Source: Tanzanian ferry sinks in L.Victoria, rescue underway

Papa Francisco atuma salamu za rambirambi kufuatia ajali ya MV Nyerere

DnorZccXoAAgrI1.jpg
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Papa Fransisco ametuma salamu za rambirambi kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere.

Katika salamu hizo kupitia kwa Balozi wake nchini Baba Mtakatifu amewapa pole wote walioko kwenye majonzi na kuwapa moyo wanaotafuta ndugu ambao hawajapatikana.

Amemuomba Mungu awajalie baraka,nguvu na faraja wote walioguswa na msiba huo.

Vladimir Putin sent a message of condolences to President of the United Republic of Tanzania

Vladimir Putin sent a message of condolences to President of the United Republic of Tanzania John Pombe Joseph Magufuli over the tragic consequences of a passenger ferry capsizing on Lake Victoria.

September 21, 2018 14:00

The President of Russia asked to convey words of sympathy and support to the families of the victims and wishes for a speedy recovery to the injured.


Tanzania ferry disaster: 136 bodies are pulled from Lake Victoria

At least 136 bodies have been retrieved from Lake Victoria in east Africa after a ferry sank on Thursday, Tanzanian officials have said.

Scores more were reported missing as rescuers searched for survivors.

The MV Nyerere, with a capacity to hold 101 people, had been dangerously overloaded, the government’s chief secretary John Kijazi told reporters. He ordered an investigation and said those responsible will face charges.

Initial estimates suggested that the ferry was carrying as many as 300 people when it capsized near the dock in Ukerewe, Lake Victoria’s largest island. The precise number was unknown, however, because the ticket-seller had drowned and the machine recording sales had not been found.

At least 37 people were brought to safety on Thursday, some in “a very bad condition”, said John Mongella, the commissioner for the Mwanza region in northern Tanzania. It was unclear whether any new survivors have been found since rescue operations resumed on Friday morning. Dozens of security forces and volunteers wearing gloves and face masks spent the day hauling bodies into wooden boats.

Tanzanian ferries often carry hundreds of passengers and are overcrowded, and there are shifts in weight as passengers move to disembark. The Nyerere was crowded because it was a market day.

Domina Maua, who was among those at the dockside seeking information about survivors, said: “I have not heard from either my father or my younger brother who were on the ferry. They had gone to the market in Bugolora to buy a school uniform and other supplies for the new school term.”

Davita Ngenda, an elderly woman in Ukara, wept as she said. “My son is among the bodies recovered,. He had gone with his wife but she has not been found yet. My God, what did I do to deserve this?”

Sebastian John, a teacher, said such tragedies had become part of life for those who live near the lake. “Since my birth, people have gone to their deaths on this lake, but what are we to do? We did not choose to be born here, we have nowhere to go,” he said.

Source: Tanzania ferry disaster: 136 bodies are pulled from Lake Victoria

--------
Tanzania: Magufuli Orders Arrest of Ferry Operators, Sumatra Officials

President John Magufuli yesterday ordered the arrest and questioning of all officials involved in supervision and operation of the capsized ferry, including Sumatra officers in order to establish their role in the accident.

The government's decision was announced in Dodoma by Chief Secretary John Kijazi on Friday, September 21.

The President also ordered national flag to fly at half-mast for three consecutive days starting tomorrow to mourn the victims, according to Mr Kijazi.

Source: Tanzania: Magufuli Orders Arrest of Ferry Operators, Sumatra Officials

----
Bobi Wine Sends Strong Message to Tanzanian President Upon Nyerere MV ferry disaster
--

This morning I read that the death toll in the Nyerere MV ferry disaster on Lake Victoria in Tanzania has risen to 209 or so. We continue to mourn with our Tanzanian brothers & sisters who lost countrymen and countrywomen in this tragedy of unimaginable proportions.

I send sympathies to fellow leaders & artistes in Tanzania. My prayers are with every family that has lost a loved one. May you find solace & peace in the Lord who promises never to leave us nor forsake us even in such trouble.

This tragedy brings to mind the perils on our lakes and rivers- with many people senselessly losing lives daily. May we all reflect and work towards eradicating such carnage on our waters because it is possible! May the souls of the departed rest in peace.
 
Habari za Hivi tulizopata kutokea huko Ukerewe kimezama mpaka sasa hivi Hatujaweza kupata idadi ya Majeruhi wala vifo tutawajuza mda si mrefu

Mwanahabari Huru

=====

Kivuko cha MV Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorara na kisiwa cha Ukala katika ziwa Victoria kimezama huku taarifa za idadi ya watu waliokuwemo ndani ya kivuko hazijajulikana.
 
55 Reactions
Reply
Back
Top Bottom