Viwanja vyetu vya ndege vina mfumo wa ulinzi uliopitwa na wakati

VIKWAZO

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
1,899
580
Salamu,
Nimesoma maelezo ya mwakyembe kuhusu polisi waliohusika na tukio la upitishaji wa madawa hapo JNIA, kwa kweli inasikitisha sana jinsi tulivyo nyuma ya wakati katika mifumo yetu ya ulinzi hasa idara za serikali.
[h=2]Mwakyembe aagiza wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wakamatwe![/h]Ni Koplo Ernest, Yusuph, Jackson, Juliana Tadei na Mohamed.
Aidha, amesema wafukuzwe mara moja ni baada ya kupitia CCTV na kuona namna walivyohusika siku hiyo kwani walionekana wakipiga simu mara watoke nje kinyume na sheria za chumba cha ukaguzi

Malezo ya waziri hapo juu yako bayana kwamba CCTV zinachofanya ni ku-record matukio yote mpaka mkanda/hard drive inaja na kuweka nyingine na kuanza record nyingine, kwa maana nyingine kinachofanyika ni kurecord matukio yanavyotokea hapo Airport kisha kuyatunza [ sijua kwa misingi gani]

Viwanja vya ndege ni sehemu muhimu sana, CCTV zake zinatakuwa live monitored, na sio tu za ndani ya uwanja lakini eneo zima la uwanja, hii ni pamoja na kusimamia mienendo ya wafanyakazi hapo uwanjani jinsi yanavyo fanya kazi zao,
Kinachofanyika kwa sasa ni mzaha yaani kurecord matukio na sio kuzuia matukio, bila viwanja kuwa na CCTV ROOM ambayo itakuwa na vijana wa kazi tena wanaosimamiwa na maafisa basi tutaendelea kuwa uchochoro, pia watumiaji wa viwanja vyetu wataendelea kupata huduma mbaya kila siku,
Waziri wa uchukuzi na Mambo ya ndani walitakiwa kuwa na TASK FORCE hizo kwenye hivi viwanja na bandari zetu na wawe wanachukuwa report kila week, kwa kadri tunakavyotumia Technologia tunapunguza sana matukio ya kijinga kama haya yanayotokea sasa [ yaani wafanyakazi kushiriki kwenye uovu kirahisi]
Salamu zangu kwa Mwakyembe
Madawa yataendelea kupita hapo kwenye uwanja mpaka viongozi mtakapokubali mabadiliko, mifumo yetu ya viwanja ni dhaifa sana na inaruhusu uharifu kufanyika kwa kiwango cha kutisha, niliwahi kusikia Gari la serikali limeibiwa hapo Airport ana liyeliiba akujulikana, sasa hapo tutapona kwenye siku ndugu zetu wale waaoteka meli wakitutaka?
Je tukio la Moto Nairobi limetufunza chochote juu ya mifumo salama katika viwanja vyetu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom