Viwanja vya wazi vyaanikwa-CCM yaongoza kwa ukwapuraji! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viwanja vya wazi vyaanikwa-CCM yaongoza kwa ukwapuraji!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Scolari, Jul 1, 2011.

1. Scolari

Scolari JF-Expert Member

#1
Jul 1, 2011
Joined: Aug 4, 2008
Messages: 273
Likes Received: 2
Trophy Points: 0
Mara kwa mara tumesikia watu wakikwapura viwanja vya wazi na kuvifanya chini ya himaya yao. Leo, 01.07.2011 Katika kikao cha Bunge, Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Mhe. John Mnyika amehoji juu ya nini hatma ya ripoti ya Kamati ya Lukuvi ambayo mpaka sasa imefanywa kuwa siri. Majibu ya Waziri, Anna Tibaijuka alikwepesha kusema lini ripoti hiyo itawekwa hadharani.

Kwanini lakini ripoti kama hiyo haipo hadharani? Mhe. Mnyika ameliambia bunge kwa mbinu zake yeye anayoripoti ambayo inaonyesha ukwapuraji wa viwanja na nani kaufanya.

Pita pita yangu, nikuta makala inayozungumzia rushwa kuwa chanzo cha ukwapuraji wa viwanja vya wazi katika Mtandao wa ufatiliaji wa rushwa. Mtandao bila kuuma umma umeainisha viwanja vilivyoporwa, vilipo, nani kapora, na anakifanyia nini;

Soma hapa makala nzima ujionee hamna ambavyo CCM inaongoza katika uporaji huo:Rushwa yatafuna viwanja vya wazi Dar

2. TIMING

TIMING JF-Expert Member

#2
Jul 1, 2011
Joined: Apr 12, 2008
Messages: 21,837
Likes Received: 125
Trophy Points: 160
3. VoiceOfReason

VoiceOfReason JF-Expert Member

#3
Jul 1, 2011
Joined: Nov 4, 2010
Messages: 5,234
Likes Received: 43
Trophy Points: 0
4. Scolari

Scolari JF-Expert Member

#4
Jul 1, 2011
Joined: Aug 4, 2008
Messages: 273
Likes Received: 2
Trophy Points: 0
5. Quinine

Quinine JF-Expert Member

#5
Jul 1, 2011
Joined: Jul 26, 2010
Messages: 10,924
Likes Received: 12,122
Trophy Points: 280
Bila kufata mtiririko, Mfumo wa ufatiliaji wa rushwa Tanzania (CTS) uliona maeneo ya wazi yaliyo katika hatua mbalimbali za uendelezwaji batili kwa matumizi ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo:
• Kiwanja Na. 1022 Kitalu E Sinza ambacho kuna ofisi ya afisa mtendaji na banda lenye vyumba vitano vya biashara na msingi wa jengo ambalo halijakamilika.
• Eneo karibu na kiwanja Na. 636 Kitalu E Sinza. Eneo lilibainika kuwa wazi ila limemegwa pande zote mbili na kuna matofali machache yamewekwa. Kamati ilielekeza kuwa Halmashauri irudishe mipaka ya kiwanja hiki na hatua ya kulitangaza kama eneo la wazi kwa mujibu wa sheria.
• Eneo karibu na viwanja Na. 281, 282, 283 na 287 Sinza B. Eneo hili limejengwa ofisi ya Mtendaji kata Sinza D. Kamati ilishauri kuwa eneo lililobaki litangazwe kama eneo la wazi kwa mujibu wa sheria na sehemu ilipojengwa ofisi ya kata eneo hilo lipimwe.
• Eneo karibu na viwanja Na. 411, 413,414 na upande mwingine kinapakana na 698 na 609 Sinza Block D, sehemu kubwa ya eneo hili ipo wazi na pia kimechimbwa kisima cha umma na kuna jiwe la msingi lenye shina la wakereketwa wa chama cha mapinduzi (CCM). Kamati ilishauri eneo lipimwe na kutumika kama eneo la wazi kama ilivyotakiwa kwa mujibu wa sheria.
• Kiwanja Na. 814, 818 Sinza Block D. eneo hili hutumika kama makazi ya watu na ndiyo waliondeleza eneo hilo. Kamati ilishauri Halmashauri kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini uhalali wa umiliki wa wananchi hao.
• Eneo jirani na viwanja Na. 480 na 481 Sinza Block D. Eneo hili lipo wazi na kamati imeshauri Halmashauri eneo hili lipimwe ili libaki kuwa wazi kwa matumizi yaliyokusudiwa. Bado haijafahamika kama halmashauri imepima eneo hili na kulitangaza kuwa wazi ili kuepuka wavamizi.
• Eneo jirani na kiwanja Na. 37 Sinza Block D ambalo kumejengwa msikiti na mmiliki wake hajulikani. Kamati ilishauri kuwa Halmashauri wafanye uchunguzi wa kina kubaini uhalali wa umiliki huu na hatua stahiki zichukuliwe. Bado haijafahamika endapo uchunguzi huo umeshafanyika au lah.
• Eneo jirani na viwanja Na. 75 na 77 Sinza Block D. Eneo hili limezungushiwa ukuta na mtu binafsi. Halmashauri ilishauriwa kufanya uchunguzi ili kubaini uhalali wa umiliki wa eneo hili na hatua stahiki zichukuliwe. Bado haijafahamika endapo uchunguzi umefanyika na ni hatua gani zilizochukuliwa.
• Eneo linalopakana na viwanja Na. 63, 99 Sinza Block D ambalo limejengwa Kanisa la Assemblies of God, Shule ya chekechea, ofisi ya CCM, gereji na pia kuna jengo la ghorofa limejengwa hapo. Halmashauri pia ilishauriwa kufanya uchunguzi wa kina na hatua stahiki zichukuliwe ili kubaini uhalali wa umiliki wa taasisi hizo (kanisa na CCM) na watu binafsi. Bado haikuweza kufahamika kuwa uchunguzi huo ulishafanyika na hatua gani zilizochukuliwa.
• Eneo lililopo mkabala na kiwanja Na. 475 Sinza B ambapo kumejengwa shina la wakereketwa wa CCM, mama lishe na pia kuna biashara ya pool inaendelea. Halmashauri ilishauriwa ifanye uchunguzi wa kina na hatua stahiki zichukuliwe. Bado haijafahamika endapo ushauri huo wa kamati ulizingatiwa na halmashauri.
• Eneo karibu na kiwanja Na. 23 Sinza C. Eneo hili hutumika limejengwa ofisi ya Afisa Mtendaji wa mtaa na pia kuna vibanda vya biashara. Kamati ilipendekeza kuwa sehemu ya ofisi imegwe na eneo lililobaki lipimwe na kutangazwa kama eneo la wazi. Haikuweza kufahamika kama ushauri huo ulikuwa umetekelezwa na halmashauri
• Eneo karibu na kiwanja Na. 24 Sinza C, ambalo limengwa makazi ya watu. Halmashauri pia ilishauriwa ifanye uchunguzi wa uhalali wa umiliki na hatua stahiki zichukuliwe. Bado haikufahamika kama halmashauri imezingatia ushauri huu na ni hatua gani walizochukua.
• Eneo karibu Na. 765, 789, 790, na 797 Sinza C. Hapa kuna sehemu hutumika kama maegesho ya magari na pia kuna kibanda cha kukaangia chipsi. Kamati ilishauri kuwa Halmashauri itoe amri kuwa wamiliki wa magari kuondoa magari yao na pia upimaji ufanyike na kulitangaza eneo hilo kuwa wazi.
• Eneo la wazi lililozungukwa na viwanja Na. 21, 23, 25, 27, 29 Sinza B. Eneo hili kuna shina la wakereketwa wa CCM ,vibanda vya mama lishe, sehemu za kutengenezea mageti, magenge na kontena la kuuzia vinywaji vikali na baridi. Halmashauri ilishauriwa kuwaondoa wavamizi hawa ili eneo libaki kuwa wazi. Bado haijafahamika lini halmashauri itatekeleza ushauri huo.
• Eneo la wazi lililozungukwa na viwanja Na.72-74. Eneo limewekwa shina la wakereketwa wa CCM Kawawa kuna mama lishe na vioski. Kamati ilibaini kuwa eneo hili kwa mujibu wa mipango miji ni la wazi na kuishauri Halmashauri iwapeleke mama lishe kwenye maeneo yanayostahili na kupima eneo husika na kulitangaza kuwa wazi. Bado haijafahamika nini kimeshafanyika mpaka sasa juu ya maeneo hayo.
• Eneo la wazi linalozungukwa na viwanja Na. 1, 2, 89, 90, 141 na 142 Sinza E. Katika eneo hili kumejengwa nyumba za makazi, Baa na asilimia ndogo ya eneo lipo wazi (baadhi ya namba ya viwanja hivyo ni 655 na 690). Kamati ilishauri kuwa Halmashauri iendelee na uchunguzi na hatua stahiki zichukuliwe. Matokeo ya uchunguzi endapo kama ulifanywa hayajajulikana bado.
• Eneo la kiwanja cha michezo na Shule ya Msingi Sinza E. Kiwanja kimemilikishwa kwa CCM na kuna vibanda vimejengwa kuzunguka eneo lote na ndani linatumika kama maegesho ya magari. Kamati ilishauri kuwa eneo litumike kwa matumizi yaliyopangwa na shughuli ambazo hazihusiani ziondolewe. Bado haijafahamika kama halmashauri imeshawapa taarifa CCM kuhusu hili na kutangaza eneo husika kutumika kwa matumizi yaliyopangwa.
• Eneo la wazi jirani na viwanja Na. 77, 79, 81, 151-154, eneo hili limejengwa makazi ya watu na sehemu za biashara. Kamati imeshauri kuwa Halmashauri ifanye uchunguzi wa kina na kuchukua hatua zinazostahiki. Bado haijaweza kufahamika hatua ambazo halmashauri imechukua mpaka sasa.
• Viwanja Na. 9 na 10 Sinza A. Wamiliki wa viwanja hivi viwili wamefunga barabara ya kuingia eneo la wazi. Kamati ilishauri kuwa Halmashauri ichukue hatua ya kufungua barabara husika ili eneo la wazi litumike kwa matumizi yaliyopangwa. Bado haijafahamika nini kinachelewesha utekelezaji huo.
• Kiwanja Na. 846 Sinza A. Eneo hili limejengwa nyumba ya makazi na biashara. Katika eneo hili taratibu za kubadili matumizi inasemekana zilifuatwa, bado haijafahamika kuwa ni ukweli au uongo.
• Jirani na viwanja Na. 38, 40, 44, 46 na 48 Mtaa wa Kibesa Makurumla. Eneo hili limejengwa ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Makurumla. Kamati ilishauri kuwa eneo la ofisi limegwe na taratibu ya kubadilisha matumizi zifuatwe na eneo lililobaki litangazwe kuwa wazi na litumike kama sehemu ya starehe na michezo kwa mujibu wa sheria. Bado haijafahamika hatua ambazo Halmashauri imefikia kutekeleza ushauri huo.
• Jirani na viwanja Na. 18 na 19 Mtaa wa Malala Makurumla. Kuna wavamizi wasio rasmi wanalitumia eneo hili kama gereji. Kamati ilishauri kuwa wavamizi waondolewe na kutokana na uhaba wa maeneo ya wazi katika maeneo hayo, eneo hilo litumike kama kiwanja cha wazi. Bado haijafahamika utaratibu mbadala ambao halmashauri imeshaweka kwa ajili ya gereji husika.
• Jirani na viwanja Na. 73, 78, 80, 82, 84 na 86 Mtaa wa Mengo Makurumla, eneo hili limevamiwa na wavamizi wasio rasmi. Kamati ilishauri kuwa wavamizi waondolewe na kutokana na uhaba wa maeneo ya wazi katika maeneo hayo, eneo hilo litumike kama kiwanja cha wazi. Bado haijafahamika utaratibu mbadala ambao wajasiriamali wamewekewa na halmashauri.
• Eneo la wazi lililopo Mtaa wa Kagera Makurumla limevamiwa na na kuna ofisi ya CCM Tawi la Karume Kata ya Makurumla na pia kuna banda linalotumika kama sehemu ya biashara. Kamati ilibaini kuwa wahusika walishapewa notisi ya kuondoka na hivyo Halmashauri ichukue hatua ya kuwaondoa wavamizi hao. Bado Halmashauri haijawaondoa wavamizi hao.
• Eneo la wazi nyuma ya Ubungo terminal ("buffer zone" ya reli) limejengwa vibanda vya biashara. Kamati ilibaini kuwa eneo hilo lilitengwa kwa ajili ya reli hivyo basi vibanda hivyo viondolewe ili kuacha eneo litumike kama ilivyokuwa imepangwa. Bado haijafahamika utaratibu mbadala ambao Halmashauri imeuweka wa kuwapa wafanyabiashara hao maeneo ya biashara ikiwa bado kuna azma ya kuboresha matumizi ya reli kwa usafiri wa ndani ya mkoa wa Dar es salaam.
• Eneo lipo jirani na kiwanja Na. 148 ambalo limejengwa nyumba ya makazi ya kudumu ya mtu binafsi. Kamati ilishauri kuwa Halmashauri iwasilishe taarifa kuhusu mwendelezaji huyo na kama ni mvamizi apelekewe notisi na kumtaka aondoe jengo hilo. Bado haijafahamika endapo taarifa ya halmashauri iliwashilishwa au lah!.
• Nyuma ya jengo la RUBADA na Kanisa la KKKT na Anglikana. Eneo hilo limejengwa shule ya msingi Ubungo Plaza kwa mpango wa MMEM. Kamati ilishauri kuwa eneo lililobakia litumike kwa matumizi michezo na burudani na si vinginevyo. Inasemekana kwa mujibu wa wakazi karibu ya eneo hilo, bado kuna baadhi ya watu wanalipangia mipango ya kulimega na kutumia kwa matumizi yao binafsi.

6. zumbemkuu

zumbemkuu JF Bronze Member

#6
Jul 1, 2011
Joined: Sep 11, 2010
Messages: 9,004
Likes Received: 585
Trophy Points: 280
iiiiiiiii.....uuuuuwiiiiiiii.....jamaniieeeee.....na imekuwaje juzi kati tu hapa mwenyekiti wa CCM taifa akijivika cheo cha uraisi wa JMT alisimama eneo la jangwani kukemea aliyevamia kiwanja kumbe ni working station ya contractor, kumbe chama chao ndo wavamizi?

7. Kamakabuzi

Kamakabuzi JF-Expert Member

#7
Jul 1, 2011
Joined: Dec 3, 2007
Messages: 1,499
Likes Received: 82
Trophy Points: 145
ikishindikana, nenda step by step anza na kuingia kwenye website yao yaani http://www.corruptiontracker.or.tz then upande wa kulia utaona latest news, na chini yake kuna articles nyingi, mojawapo ni hiyo ya corruption nemesis eats dar open spaces

8. Paul Kijoka

Paul Kijoka JF-Expert Member

#8
Jul 1, 2011
Joined: Oct 25, 2010
Messages: 1,400
Likes Received: 6
Trophy Points: 135
404 - Article #0 not found
You may not be able to visit this page because of:

1. an out-of-date bookmark/favourite
2. a search engine that has an out-of-date listing for this site
3. a mistyped address
4. you have no access to this page
5. The requested resource was not found.
6. An error has occurred while processing your request.
Please try one of the following pages:

If difficulties persist, please contact the System Administrator of this site.
Article #0 not found

Hiyo hapo juu ndo taarifa inayojitokeza.

Loading...