Viwanja vya ndege migodini vyatumika kutorosha madini- Kamati ya bunge yafichua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viwanja vya ndege migodini vyatumika kutorosha madini- Kamati ya bunge yafichua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Mar 24, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), wameitaka serikali kufunga viwanja vya ndege vilivyojengwa katika maeneo ya migodi kwa kuwa vinatumiwa na wawekezaji kutorosha dhahabu nje ya nchi bila kulipa mapato.
  Wamesema hakuna haja ya makampuni ya madini kuwa na viwanja maeneo ya migodini, badala yake watumie viwanja vikubwa vilivyopo nchini wakati wakisafirisha dhahabu ili iwe rahisi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukusanya mapato.
  Akichangia katika kikao kati ya Wizara ya Nishati na Madini na wajumbe wa kamati hiyo, kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam, Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele, alisema ana ushahidi kwamba, wawekezaji wanatorosha dhahabu nje ya nchi kwa kutumia viwanja wanavyomiliki maeneo ya migodini.“Mheshimiwa Mwenyekiti, hili sio jambo la siri. Hawa wawekezaji wanatumia viwanja hivi kuvusha dhahabu kwa kutumia ndege zao, ambazo hazipiti kwenye viwanja vya kawaida,” alisema.
  Alisema serikali wamekuwa wepesi kufanya ukaguzi katika mazao ya pamba, ambayo yanasafirishwa nje ya nchi kwa kukagua kontena moja baada ya lingine, lakini kwenye madini wameshindwa kufanya hivyo ingawa huko ndiko kwenye fedha nyingi.
  Masele alisema pia ana mfano hai kwamba, mgodi wa Mwadui, mkoani Shinyanga ingawa hivi sasa umefungwa, wawekezaji wanafanya uzalishaji kinyemela, huku wakikwepa kulipa mapato ya serikali.

  Mbunge wa Chwaka, Yahya Kassim Issa, akichangia katika kikao hicho, alisema wawekezaji ni watu waliokuja kuchuma, hivyo sio watu wa kuaminiwa, wafanyekazi nwenyewe bila kusimamiwa na kisha waweze kulipa mapato sahihi.
  Aliitaka serikali kuwafuatilia na kuwabana badala ya kuwafanyia uzembe na kuwaacha wakichota dhahabu nyingi bila kulipa mapato halisi ya serikali.
  Kamishna wa Madini wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Peter Kafumu, alipingana na hoja hizo na kusema ndege zote zinazochukua vifurushi vya dhahabu zinapitia kwenye Viwanja vya Ndege vya Kimataifa vya Kilimanjaro (KIA) na Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam. Alisema katika viwanja hivyo, kuna maofisa wa TRA na wa madini, ambao wanahakikisha mzigo wote umekaguliwa kabla ya kuondoka nchini.

  Hata hivyo, Dk. Kafumu aliwashangaza wabunge baada ya kusema kuwa wawekezaji wakubwa ni watu wema na waaminifu na kwamba wanaoweza kufanya uhuni kama huo, ni wachimbaji wadogowadogo, ambao ni wazawa kwa madai ya kugopa kufungiwa biashara zao kwenye soko la hisa.
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zainabu Vulu, alimtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, kutoa msimamo wa serikali kuhusu madai ya wabunge hao, ambapo alisema amepokea mawazo yao na atayafanyia kazi. Akitoa taarifa ya mapato ya serikali yanayotokana na madini, Jairo alisema ukusanyaji wake ni mzuri na ndiyo sekta inayoongoza kwa mapato kuliko wizara nyingine.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kauli ya Dr. Kafumu inatia shaka kutetea hoja ya kamati bunge kufichua siri ya wawekezaji kutorosha dhahabu bila kupitia viwanja vya kukagulia. Labda wanammegea kitu.
   
 3. Rugambwa31

  Rugambwa31 JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hii nchi inawatu waajabu sana. Kwann serikali hiliruhusu viwanja kujengwa kwenye migodi? kwann wasingo tengeneza barabara hao mnao waita wawekezaji wakati ni waporaji wa mali zetu? mm nashangaa a hapa halafu unakuta kiongozi mzima anasema kwamba tunawashukuru wawekezaji (waporaji) kwamsaada wao wakisima cha maji/madawati/nyumba ya mwalimu du kweli nashangaa kweli. Yani hakuna kiongozi mwenye kujiamini na kusema hapana kwa hili. Sipati picha siku tutakapo pata viongozi kama wakina Nyerere/Mandela/Sokoine/ nawengine wengi kuongoza tz mpya ninayo hiona mbeleni.
  Wewe unakubali kirahisi wachimbe uranium kweli kweli, madini mengine tunaibiwa halafu mnaleta utani.
  ninauchungu sana sana. Mungu nisaidie niweze kuwana moyo wa huruma kwawananchi wa tz hasa wanaosumbuka vijijini bila UMEME/MATIBABU/CHAKULA/MARADHI/AMANI MOYONI na mengine mengi.

  mungu ibariki tanzania na watu wake.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kamwe mfanyibiashara hawezi kuwa mtu mwema na mwaminifu wakati anaendeshwa na profit motive. Ni wajibu wa mwenye ardhi kuhakikisha kuwa hapunjwi na yule aliyeingia kuchimba. Na hatufanyi hivyo.
   
 5. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Wamekuja kutoka wapi??? Si ni watu wa humuhumu ndani?? Kwani wewe humjui rostam Azziz??
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Yaani hata mamlaka ya anga yanaruhusu mtu wa nje ya nchi ajenge uwanja wa ndege ndani ya rasilimali za taifa bila uthibiti wa wahusika? Ovyo kabisa serikali ya nchi hii.
  Katibu wa wizara anatetea bila aibu.
   
 7. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2011
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Rostam huyu muiran wa igunga!!??
   
 8. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Halafu mnataka kujenga nuclear reactors...tutaweza kuzidhibiti?
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Angalau ingekuwa ni kupitisha dhahabu tu; silaha haramu nyingine hupitishiwa wapi?
   
 10. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  Msilaumu wakati hakuna barabara za kwenda huko. Hao wabungu kable ya kufunga viwanja wajenge barabara!. Huwezi kumwambia investor huturuhusu viwanja wakati hata barabara huna!!
   
 11. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Where is TRA and Takukuru?
   
 12. m

  matawi JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hii hadithi inafanana sana na yule Mzungu aliyekuja kupanda mlima kilimanjaro kwa mara ya kwanza akajitangazia ndo kuwa ndo binadamu aliyegundua mlima kilimanjaro wakati njia alionyeshwa na wachaga na siku hiyo walipanda wote. Hii dhahabu kubebwa na vindege vya ndani kwa ndani mbona kahama mpaka watoto wadogo wanajua. Tatizo hapa anayesema(Masele) haaminiki maana alishindwa na Shilembi lakini Makamba akaamuru tume ya uchaguzi kutangaza Masele kashinda
   
 13. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hii nchi inahitaji ukombozi wa mali asili zake. Huu wizi utakomeshwa mpaka pale watu kama Dr. Kafumu watakapojua kuwa katika biashara hakuna wa kumwamini hasa hawa mashetani, Marekani na Ulaya. Ina maana mbunge anadanya? Sema utafanyia kazi ili tuelewe ulikuwa hujui. Au ulishakula cha kwako. Siku ya ukombozi tutachoma vingi na wengi kweli wengine wakiwa watanzania wezetu.

  Kwa heri.
   
 14. Papa Diana

  Papa Diana JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Best option ni kuwa na wakaguzi ndani ya hivyo viwanja ingawa rushwa itakua tatizo lakini hata huku kwenye viwanja vya kawaida bado ipo pia!

   
 15. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160

  Ndiyo. Badala ya kuvifunga TRA inashindwaje kuwepo kwenye viwanja hivyo?
   
 16. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  Mbona hata hapa KIA wanapitisha Tanzanite kwenda kwa makaburu na india chini ya ulinzi mkali, why bcz wanahu
   
 17. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Hiyo ni kweli kabisa kwa nini wasitumie barabara hadi shinyanga au tabora au mwanza ndiyo wapande ndege....

  Hawa mawaziri wetu hawajui nini cha kufanya wao wako busy na maslahi binafsi tu na siyo maslahi ya nchi.....

  Tuone waziri wa wizara husika kama atatoa majibu ya kamati ya bungu...
   
 18. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hivi Rostam ni mtu wa humu humu? Mwenye data atusaidie shule ya msingi alisomea wapi? Sekondari alisoma shule gani? Chuo baada ya sekondari na inawezekana alienda JKT je alikuwa operation gani, kombania gani? Tusaidie
   
 19. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #19
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hao hao wanapinga kujenga barabara kupitia mbuga za wanyama kwa vile madini hayachimbwi huko?
   
 20. TITAN

  TITAN JF-Expert Member

  #20
  Mar 25, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 309
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani sikuzote walikua wapi wasione ilo? nathani ni kutaka kujisafisha,
   
Loading...