Viwanja vya ikulu ya tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viwanja vya ikulu ya tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Panga la Yesu, Feb 17, 2011.

 1. Panga la Yesu

  Panga la Yesu JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ALELUYAH!

  Habari za leo wana JF?

  Katika pita pita yangu nimesikia fukuto la vijana wengi wakiwa na tamanio la kuhamia nje mwa viwanja vya ikulu ya Tanzania kwa lengo la kuwaunga mkono wasomi ambao wamemaliza migomo yao hivi karibuni na wengi kuishia kufukuzwa chuo.
  Hii inatokana na watu wengi ambao wanasimamishwa kazi kutokana na mgao wa umeme, na wale ambao walikuwa na biashara ndogo ndogo lakini kutokana na gharama za maisha kuwa juu mambo yamekuwa tight na hawawezi tena kuendelea kusurvive ukijumlisha na wale wote wasio kuwa na kazi basi tunategemea kuwa na kusanyiko kubwa sana. Lakini pia nimesikia wafanyakazi wengi pia wanautayari wa kuwaunga mkono hii ni kumaanisha kuwa kutakuwa na kusanyiko kubwa sana.
  Lakini pia pia wanataka Viongozi ambao wamekuwa na skendo basi wawajibike mara hii ikiwa ni pamoja na JK.
  Sasa hapo ndo nikajiuliza hawa watu wana akili kweli? je ninani aliyeandaliwa kuchukua nafasi ikiwa JK ataondoka ghafla? Je amani ya Tanzania itabaki kama ilivyo? Au ndo Jeshi litachukua nchi? Mimi nikaonelea ni vema wakawa na subira kidogo walau iwe imendaliwa system itakayo chukua nafasi ili Taifa lisiyumbe. Lakini Serikali ya JK ijue tayari hili Jambo liko kwenye Pipe line hivyo wajitahidi kurekebisha mambo kwa haraka!
  Ninalo lifahamu mimi sisiem mwisho ni 2015 hivyo ni vema tuwape nafasi ya kuaga!
  Mungu awabariki!

  Mungu Ibariki Tanzania!
   
 2. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  jeshi la tanzania si kama la misri halina ujasiri wa kuwaunga mkono wanacnhi kama Misri nadhani watu wakiandamana watuwawa kama makaratasi, hawana ujasiri wa kuwaza kutumia maji ya chumvi au risasi za mpira wao ni kulipua risasi kali na mabomu moja kwa moja. Polis wa tanzania ndio kabisa hamnazo mfano halisi ni Arusha waliuwa wanachi ambao hawakuwa hata na fimbo mkonnoni bali vitambaa vyeupe lakini wao badala ya ktutumia risasi za mpira au maji ya kuwasha wao wakafyatua risasi kali nyingi tu,sasa hebu waza na linganisha akili za jeshi la Tanzania polisi na majeshi ya nchi zingine wkt wa maandamano.Labda watataka wananchi waaandike barua ya kuomba kuandamana wkt ni haki yao kikatiba kuandamana kudai haki zao za msingi.Sijui kama wanachi wa Misri au Tunisia waliomba kibali cha kuandamana kushinikiza viongozi wao waondoke, libya nako, Bahrain au Jordan. Siwalaumu bure labda pia akili zao manake wengi walio jeshini au polisi ni wale waliofeli form 4 au kupata alama hafifu za kusonga mbele hivo hata maamuzi yao ni ya kukurupuka. kama jeshi wangekuwa wanalinda maslahi ya umma na usalama wao lazima wengekuwa wanakagua ssilaha zao kila mara na zile mbovu wangeshaziharibu,Mbagala haiajawapa somo kabisa naona bado tuan safari ndefu mbele yetu.System bado ni mbovu,viongozi hawaeleweki,uzalendo hakuna,
   
 3. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ngoja wanajeshi na polisi wa kawaida waendelee kupigika na maisha nao ni binadamu watachoka na kuungana na wananchi.... hapo ndio ccm ijue hali mbaya.
   
 4. Panga la Yesu

  Panga la Yesu JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini hata hilo Jeshi lina ndugu zao ambao watakuwa kwenye maandamano, kama si shemiji basi ni shangazi, pia nimefuatilia maisha ya wanajeshi na polisi wa usalama wa raia pia sioni wanafaidika na nini kiasi cha kumsupport JK, Ninaamini tuna Basilio Matei wengi tu huku Tanzania ambao hawatakuwa tayari kuona wa TZ wakiumia.
  Swali langu linarudi pale pale je leo hii JK akipinduliwa kwa nduvu ya Umma tunamtu ambaye anaweza kukabidhiwa mamlaka ta Tanzania? Au tuseme Protokali zinakuwaje?
   
 5. f

  furahi JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 947
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Umenikumbusha machungu ya kumpoteza Basilio Matei Arusha. Serikali hii imewaumiza sana watu wake... Sijui
   
 6. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,827
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  Hata hapa jamii mbona wanajeshi wamejaa wanajua ili wapate kufaidi keki ya Taifa lazima tuwatoe ccm, ila shimbo ndio hatakubali mana kwanza yeye kapewa nafasi ile kwa ajili ya kupeleka ulongo kwa mkwere.
   
Loading...