Viwanja vilivyotumika wakati wa siku ya Uhuru, tuvitumie sasa kusema na kudai haki zetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viwanja vilivyotumika wakati wa siku ya Uhuru, tuvitumie sasa kusema na kudai haki zetu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by PERECY, Apr 24, 2012.

 1. PERECY

  PERECY Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WanaJF,

  Mkanganyiko ni mkubwa. Hatuamini. Nafuatilia mitandao na vyanzo mbamlimbali vya habari, mazungumzo makubwa ni utata na mkanganyiko wa taarifa ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha na mali za umma, na dhana ya uwajibikaji. Kilichotegemewa, sicho kilichotokea. Mkuu wa nchi alinukuliwa akisema ni upepo tu, utapita.

  Tukumbushane. Marehemu Gaddafi alisema mende nyie, hamna adabu, mmevuta madawa ya kulevya. Kilichotokea, wote tunakikumbuka. Pamoja kile kilichoonekana wema kwa wananchi wake! Syria, Misri, kote tumeona.

  Sasa, kwa kuwa imeonekana Waziri Mkuu, wala Rais hayuko tayari kuwawajibisha mawaziri wanaotuhumiwa, wabunge pia wameshindwa kusema kwamba kuanzia sasa wao pia wanaachana na ubunge na kwamba mawaziri wabaki wao tu waendeshe nchi; kwani tumeona wengine waliongea kwa mbwembwe, lakini kweye kutia saini wakaingia mitini, wamebaki kimya. Natoa wito kwa wabunge makamanda, waandae mpango wa kuwakusanya wananchi katika mikoa mbalimbali, kwa kutumia viwanja vilivyotumika wakati wa kudai uhuru ambavyo viko kila mkoa, ili wananchi waamue. Tufike mahali wananchi sasa tuamue, kwani inaonekakana tuliowaamini hawawezi!

  Tafakari njema!
   
 2. tindo

  tindo JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 10,069
  Likes Received: 10,246
  Trophy Points: 280
  Hilo ndilo lililobakia ndugu yangu.
   
 3. a

  ambwene_ambwene Member

  #3
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu...... Atajibu kwa wakati wake tena jibu lake halina madhara. Tuombe sana kila mtu kwa imani yake.
   
 4. a

  ambwene_ambwene Member

  #4
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Viwanja hivyo pia tuvitumie kwa maombi hadi mungu aliyetupa uhuru kwa amani ashuke atupe ukombozi kwa amani pia.... Ombeni bila kukoma.......
   
Loading...