Viwanja vilivyopimwa na serikali vinauzwa bei tsh 500per sqr mita

MAKOLA

Member
Jun 5, 2010
46
16
wakuu nimepita wilaya nyingi kutafuta maisha nimekutana na kitu adimu sana nchini humu. Nilifika wilaya ya kilindi mkoa wa tanga wilaya hii ni mpya imezaliwa kutoka wilaya ya handeni, nilifika nikakutana na maafisa ardhi ambao niliwashangaa. Kwani nilipewa fomu ya maombi nikalipia benki tsh 5000 halafu wakanipa ramani na bei ya kila kiwanja ipo kwenye kitabu cha bei nkachagua kiwanja wakanipa invoice nikalipa benki kwenye akaunti mbili za serikali nikarudi kwao wakanielekeza kwenda ofisi ya fedha nikakatiwe risiti.nikakatiwa risit nilichoshangaa nikaandaliwa offer yangu ya kiwanja sikuhiyohiyo. Wadau ardhi kuna urasimu lakini kama ofisi zote zingekuwa hivi mambo yangekuwa mstari.wakaniambia wanawakaribisha watanzania wote na wametangaza viwanja hivyo kwenye magazeti.kwa anayetaka fursa hii wasiliana na hao maofisa o787737616 au 0653792114 kazi kwenu wajasiliamali
 
Ingekuwa Wizara ya Ardhi ingekuchukua hata miaka mitatu kupata hiyo offer. Mara nyingine najiuliza kuna nini pale Wizara ya Ardhi document ya kureview tu kidogo inachukua miaka yote hiyo. Unakuta mtu amepewa kiwanja kinamakaburi na Wizara ndio yenye mamlaka ya kuyahamisha ila unakuta unaendelea kulipia kodi ya ardhi na huwezi kuendeleza kiwanja unafuatilia miaka inaenda tu. Ukiuliza ardhi watakuambia wako kwenye mchakato...yaani inakera kweli!
 
Vigezo na Masharti ya Offer kuzingatiwa.........ujenzi ufanyike ndani ya miaka 3.
 
Kilindi?
Oooh! My, kuna mama moja alikuwa anajua kupika supu ya kuku na chapati pale kati? Sijui yupo siku hizi?

anywayz, huko mkuu hatuji kabisaaa! Labda handeni bana!
 
huko kilindi kaeni wenyewe.....nani anataka matatizo saizi?

Kilindi?
Oooh! My, kuna mama moja alikuwa anajua kupika supu ya kuku na chapati pale kati? Sijui yupo siku hizi?

anywayz, huko mkuu hatuji kabisaaa! Labda handeni bana!


Naamini wakuu huko mnaujua vizuri sana, hebu tupeni maelezo zaidi kwa sisi ambao hatujawahi kufika kupoje hivi?
 
nmevutiwa na hii taarifa! naomba nipe inform za kutosha kuna barabara?,maji , umeme umeshafika? kuna umbali ngani kutoka Tanga mjini. pls im serious nitumie kwenye e-mail yangu j.maruma@hotmail.com. Fanya hima ndungu
 
Back
Top Bottom