Viwango vya mishahara kwa walimu: Ualimu ni mateso

watumishi nasubiri mtaje mishahara ya wenzenu wa mashirika ya umma maana baadhi yenu mnaishia kusema tu mishahara ya mashirika ya umma ni mikubwa bila kuitaja
 
Hivi unafikir mishahara ya serikali ni kiasi gani!?? Kwa fani zoote pesa ni ndogo zaid ya hiyo
kuna watu wana mishahara kama hii ya walimu tu but kwa mwez wanapiga 1m+ za deals jumlisha na kama laki tano posho na bado tuvikao so jamaa anaweza kuvuta 3m kwa mwezi
 
Biashara yenye faida ya laki 1 kwa mwezi ni milioni 3,.....mtaji wake si chini ya milioni 30, hongereni sana wapambanaji
Ila inategemea na biashara, mm nna biashara laki 3 zinajizungusha ila faida kwa mwezi laki na nusu mpk laki 2
 
TGTS E1=940000/= Basic Nimepanda juzi tu kwa Mama samia!!!
Msiseme tuna maisha magumu!ugumu wa maisha unaanzia kichwani mwako mwenyewe!!sema jpm ndio alitutesa sana kwa miaka hii sita!tunamshukuru Mungu:-
Mwaka wangu wa saba huu kwenye job:-Nyumba tatu,frem nne za biashara,glossary,ukumbi wa mikutano na Kuonyesha mpira live!Mashamba ya miti eka tano huko njombe!!!Duka la nyumbani hapa anauza mama watoto!!Baba wa watoto mbili Tatu loading... Please wait!!na mwakani mama ataongeza mishahara aliahidi mei mosi mwaka huu!!AKILI !AKILI!AKILI!!!WATUMISHI WENGI AKILI HAMUNA KABISA KAZI POMBE NA MIKASI TU!NAWAONA HAPA KIJIWENI FULL VITUKO!!!
Nimejifunza kitu kwako mzee!
 
! Huo mpango niliwahi ufanya! Nilitamani kununua nyumba, hela toka mkopo wa bank A ikawa haitoshi!

Nilichofanya ni kuongea na kijana wangu wa hazina anisimamishie makato kwa mwezi mmoja ikaja pay slip "safi", nikachukua tena fomu na kwenda bank B kukopa na nikafanikiwa.

Sasa bank zote zikawa zinanyang'anyana mshahara wangu kama mafisi wagombeavyo mzoga, mi nawachora tu nikiwa ndani ya mjengo.

Zoezi hilo hadi kumalizika inabidi uwe umejizatiti kisaikolijia hasa na uwe na miradi ya kukuongezea kipato iliyosimama sawasawa, vinginevyo utakuwa kama umefukuzwa kazi kwa aibu.

Maana na ile furaha ya mwisho wa nwezi ya: "leo mshahara umetoka",inakuwa haikuhusu na hautakiwi kulalamika popote!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viwango Vya Mshahara Wa Walimu 2021/2022 | Teachers Salary Scale Range
New Government Salary Scales: Approved

  • TGTS B1 = 419,000/- and TGTS C1 = 530,000/-​
  • TGTS D1 = 716,000/- and TGTS E1 = 940,000/-​
  • TGTS F1 = 1,235,000/- and TGTS G1 = 1,600,000/-​
  • TGTS H1 = 2,091,000/- and TGTS I = 2,810,000/-​
B1 = Basic 419,000
  • Cwt = 8,390.​
  • Pension = 20,950.​
  • Income = 46,090.​
  • Insur = 12,570​
  • Take home = 331,000​
C1 = Basic 530,000
  • Cwt = 10,600.​
  • Pension = 26,500.​
  • Income = 58,300.​
  • Insurance = 15,900​
  • Take home = 418,700​
D1= Basic 716,000
  • Cwt = 14,320.​
  • Pension = 35,800.​
  • Income = 78,760.​
  • Insurance = 21,400​
  • Take home = 565,640​
E1 = Basic 940,000
  • Cwt = 18,800.​
  • Pension = 47,000.​
  • Income = 103,400.​
  • Insurance = 28,200​
  • Take home = 742,600​
F1 = Basic 1,235,000
  • Cwt = 24,700.​
  • Pension = 61,750.​
  • Income = 135,850.​
  • Insurance = 37,050​
  • Take home = 975,650.
Kazi ni kwako ndugu mwalimu
NAOMBA KUFAHAMU KIREFU CHA TGTS TAFADHALI
 
Back
Top Bottom