FikraPevu
JF-Expert Member
- Jan 2, 2010
- 303
- 236
Serikali ya Tanzania inakusudia kuagiza tani 100,000 za sukari kutoka nje ili kukabiliana na uhaba wa sukari nchini utakaosababishwa na kufungwa kwa muda kwa viwanda vyote vinavyozalisha sukari nchini, hali ambayo tayari imesababisha uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo, huku katika baadhi ya maeneo nchi ikianza kuuzwa kwa bei ya kuruka.
Taarifa zilizoifikia FikraPevu zinasema viwanda vyote vikubwa vya sukari nchini vitasitisha uzalishaji wa bidhaa hiyo muda wowote kuanzia sasa, wakati kwa ujumla, vyote vikiwa na shehena ya akiba ya sukari inayofikia tani 40,000 tu wakati mahitaji halisi ya nchi kwa mwezi ni tani 35,000.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hali hiyo ya kuadimika kwa sukari katika baadhi ya maeneo nchini hata kabla viwanda hivyo havijasitisha uzalishaji, kumeelezwa kusababishwa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu, ambao wanadaiwa kuhodhi bidhaa hizo wakisubiri bei ya bidhaa hiyo iadimike zaidi baada ya viwanda vilivyopo nchini kusitisha uzalishaji hali itakayosababisha kupanda kwa bei zaidi kwa bidhaa hiyo na kuwawezesha kuvuna faida kubwa.
Hadi sasa katika baadhi ya maeneo nchini, sukari imeanza kuuzwa kwa mwendo wa kuruka wa kati ya Sh 2,500 na 3,000 badala ya bei iliyozoeleka ya kati ya Sh 1,800 na 2,000 kwa kilo.
Kwa sasa viwanda vya sukari vilivyopo nchini vilivyokuwa vikizalisha sukari na ambavyo vinakusudia kusitisha uzalishaji kwa muda kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati, ni pamoja na kiwanda cha Kilombero na Mtibwa vilivyopo mkoani Morogoro, TPC kilichoko mkoani Kilimanjaro na Kagera sugar kilichoko mkoani Kagera
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, amethibitisha kuwepo kwa mpango huo wa Serikali wa kuagiza tani 100,000 za sukari nje ili....
Habari zaidi, soma=>Viwanda vya sukari kufungwa, Serikali yajiandaa kuagiza tani 100,000 za sukari nje.