VIWANDA vs CHAKULA

Tuluway

New Member
Apr 1, 2012
1
0
Miaka 55 ya UHURU wa TANZANIA ( TANGANYIKA?)

Mtazamo wangu;

VIWANDA VS CHAKULA



Hivi ni kipi cha muhimu kwanza?

Hebu tuangalie Historia, nchi zote zenye maendeleo makubwa ya viwanda, zilianza kwanza na mapinduzi ya Kilimo... ndiyo... the Agrarian revolution.... Hii maana yake ni kwamba kwanza kulikuwa na malighafi ya kutosha ndiyo vikafuata Viwanda.... maana kubwa zaidi ni kwamba walikuwa na "CHAKULA" cha kutosha. Hata hizo nchi zenye viwanda visivyotumia mazao ya kilimo, kwanza walianza na kuhakikisha kwamba wana supply ya kutosha ya chakula ili kuweza ku attract rasilimali, kubwa ikiwa ni WATU.
Tukifupisha hayo yote, tunapata hitimisho moja tu; Kwamba moja ya rasilimali kubwa, na pengine ya MUHIMU kuliko zote, katika maendeleo yoyote ya kiuchumi, basi ni CHAKULA.
Ni kosa kubwa kudhani mafanikio ya Kiuchumi ni FEDHA! Kwani fedha ni nini? Fedha ni "wazo" tu. Ndiyo maana dunia inaendeshwa kwa mfumo wa "credit". Nilisoma mahali fulani, inakadiriwa jumla ya Dollari za kimarekani HALISI (physical) zilizoko duniani kote ni Trillion 1.2 tu. Sina uhakika na hilo, lakini hiyo maana yake ni kwamba, leo hii mfumo wa "credit" ukifa leo, uchumi utaanguka, maana hapatakuwa na "FEDHA"ya kuitosha dunia nzima. Fedha hazina thamani, chenye thamani ni bidhaa na bidhaa ya thamani kubwa kuliko zote ni CHAKULA.

Rafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia; "Nchi moja ikiwa na wanajeshi Millioni Mbili wenye ujuzi na silaha nzito, na nyingine ikawa na akiba ya chakula cha kuwalisha watu million mbili, basi automatically nchi yenye akiba ya chakula ina "NGUVU" kuliko ile yenye wanajeshi. Ninapotafakari usemi huu katika hali ya sasa, basi ninamwelewa vizuri sana mtu huyu...
Nimeamua kuibua hoja hii, nikiwa natafakari uamuzi wa nchi yetu, baada ya miaka 55 ya Uhuru, kwamba tunataka kuwa na uchumi wa VIWANDA... Wazo zuri!!!
Mashaka yangu ni kwamba, hakuna mahali popote paliwahi kuwa na mapinduzi ya Viwanda bila kuwa na Mapinduzi ya "CHAKULA". Sisi ni nani kuamini tunaweza kufanikiwa vinginevyo??
Takwimu zinaonyesha kwamba, 60% ya chakula chote duniani kinazalishwa na nchi nne tu, Marekani, Brazil, India na China. Na katika hizo, India na China wameanza kufika mahali ambapo hawana ziada ya kuuza nje. Kumbe Dunia inaelekea kutegemea zaidi nchi ya Marekani na Brazil kuzalisha chakula cha Ziada!
Lakini hebu tujiulize, Marekani na Brazil wana nini kinachowawezesha kuwa na chakula cha ziada ambacho nchi nyingine duniani, especially za Kiafrika, hazina? Barani Afrika, nchi pekee zenye 'angalao' unafuu wa kujitosheleza kwa chakula ni mbili tu, Afrika ya kusini na Misri. KWA NINI?

Hebu tuingalie nchi yetu ya Tanzania; kwa mujibu wa Takwimu za NBS, nchi ina hekta zipatazo million 29 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji... HEKTA MILLION ISHIRINI NA TISA!!. Katika hizi tunaambiwa ni kama Million 2 au 3 tu ndiyo zimeendelezwa. Zingine zote zipozipo tu.
Lakini najiuliza, ni Mamlaka gani ambayo mtu akienda, anaweza kuonyeshwa hizi Hekta Mamilioni zilipo? Je zinafaa kwa shughuli zipi? Kama kuna Mamlaka yenye taarifa hii kwa kina, naomba nifahamishwe, kwani hii ndiyo Mamlaka yenye majibu ya "Mkwamo" wetu baada ya Miaka 55 ya Uhuru.
Nimejaribu kupita kwenye ofisi kadhaa za halmashauri za wilaya na miji; unakuta kuna ofisi ya idara ya Ardhi, Idara ya maji, idara ya uvuvi, misitu!!!! Na hawa wote wana mipango isiyoshabihiana. Kila idara ina "priorities" zake!!!

Hebu tujiulize, kwa maendeleo haya ya teknolojia ya setilaiti tuliyo nayo; inachukua muda na budget resources kiasi gani ku identify na kufanya LAND USE PLAN ya hizi hekta Mil 29????
Na Kama tukiweza kufanya LUP ya maeneo yote haya na kuainisha aina ya mazao yanayoweza kuzalishwa , halafu kama Taifa, tuka incentivize investiments kwenye maeneo haya ( hata kama inamaanisha kusubiri kujenga standard gauge railway na badala yake kuweka miundo mbinu ya kuyafikia maeneo haya),
Halafu ndani ya Miaka mitatu au minne ijayo tukahakikisha kwamba Tanzania ina akiba kubwa ya chakula kuliko nchi yoyote Afrika?

Hivi ni nani mwenye mafuta, au dhahabu, au mali nyingine yoyote atakayetaka kufa na njaa? Ala? Na kwa sababu hao wenye teknonolojia zao hawatakubali kufa na njaa, hivi ni nini kitawazuia kuwekeza Viwanda kwenye Nchi yenye "Maziwa na Asali" ili wapate bidhaa zinazostahili kwenye masoko yao? Hivi nini kitatuzuia kubadilishana chakula na China ili wao watujengee Standard gauge Railway? Au ni nini kitawafanya ulaya watunyime teknolojia ya kuchimba mafuta yetu kwa kubadilishana na chakula?

Yapo mengi ya kuchangia, leo naishia hapa nikiwakumbusha kitu kimoja.....
Marekani waliibuka kuwa taifa kubwa na lenye nguvu duniani baada ya Vita kuu ya Pili ya dunia.... na siri yao haikuwa silaha kubwa kubwa.... siri yao ilikuwa ni chakula tu!!! Leo hii ulaya haina cha kusema kwa Marekani kwa sababu moja kubwa.... CHAKULA.

TAFAKARI! CHUKUA HATUA
 
Back
Top Bottom