Viwanda Tanzania

Haika

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,347
560
nimemsikia waziri wa viwanda akisema kuwa wanafuatilia viwanda ili viongeze mchango wake kwa pato la taifa.
Naona ni wazo zuri,
Sasa naomba tujadiliane, je viwanda vipi vya kukuzwa au kuanzishwa?
viwekwe wapi?
Je kuna viwanda vya kufunga au kuhamisha?
 
nimemsikia waziri wa viwanda akisema kuwa wanafuatilia viwanda ili viongeze mchango wake kwa pato la taifa.
Naona ni wazo zuri,
Sasa naomba tujadiliane, je viwanda vipi vya kukuzwa au kuanzishwa?
viwekwe wapi?
Je kuna viwanda vya kufunga au kuhamisha?

Swali zuri sana!
Ila nitarudi hapa na ideas baada ya kukusanya tudata tuwili tutatu!
Kama tunataka uchumi wetu uimarike kwa kasi kubwa basi viwanda ni one of the most important issues.
Tatizo ambalo ni kubwa sana limekuwa ni umeme!
Na serikali yenyewe ina subsidies lakini mambo ni mbaya na huu ufisadi wananchi hawaelezwi ni kwa vipi wanaweza kuchangia kwenye uchumi wa nchi.
Kwa hiyo wakati tukiendelea na mjadala huu then tusisahau kuwa lack of electricity ni mojawapo ya factors kubwa zenye ku hinder our economic development.
Wakati nilipokuwa Dar two yrs ago nilikuta mgao wa umeme na uchumi ulikuwa umelala!
 
Kwa sasa hivi hakuna mgao wa umeme, ni bahati sana.
Je ni vitu gani vizingatiwe wakati wa kufanya maamuzi?
 
Kwa sasa hivi hakuna mgao wa umeme, ni bahati sana.
Je ni vitu gani vizingatiwe wakati wa kufanya maamuzi?

OK, nafikiri kuwepo na msisitizo wa kufungua viwanda maeneo maalum yaliyotengwa kama ni vile vyenye uzalishaji wenye kusababisha high polution!

Hata hivyo viwanda viko pia vya aina nyingi...

Tukiweka msisitizo kwenye viwanda maeneo ya vijijini then tunaweza kuwasaidia kwenye maendeleo na pia kulizika tatizo la njaa!

Viwanda vya usindikaji vyakula,mboga, matunda, nafaka nk.

Pia kuna ardhi kubwa tu ya kuweza kujitengea eneo la uzalishaji wa maua biashara ambayo ina uwezo wa kulitajirisha taifa letu kama ikisimamiwa vyema. (Tumeshindwa kutumia EPZ, AGOA)

Viwanda ambavyo vinakazi ya kuproccess raw materials viwe huko huko zinakopatikana hizo raw materials (ie rural areas) ili kuinua uchumi wa eneo husika na kuepuka gharama za usafirishaji na upotevu wa mapato, na pia kuwapatia kazi na mapato wakazi wa maeneo hayo na hivyo kusaidia kupunguza mrundikano wa nguvu kazi mijini.

Ninashangazwa sana na vitendo vya kufungua viwanda mijini kunakofanywa na wengi..Na hapo unashangaa kwanini watu wanahama vijijini.

Na pia nashangazwa sana na vitendo vyetu va kuendelea ku export raw materials na kuendelea ku encourage mitumba!

Naishia hapo kwa sasa.
 
Naungana na wewe moja kwa moja, hata mimi inanishangaza sana kuexport raw materials! Hivi inachukua miaka mingapi kugundua, kufanya research na kufanya maamuzi na kutekeleza uamuzi wa kuacha kuexport raw materials?
Manake tumeyasikia haya sana majukwaani, utekelezaji wake hauonekani.
Mfano madini hadi leo tunexport raw!!! Hivi kuna kiongozi ambaye hajui tunapoteza sh ngapi?
Ni jambo la kusikitisha sana.
Tanzania tunachohitaji ni rais mjasiri na mzalendo, sio vyeti, watu wenye vyeti wapewe kazi za kushauri na kutekeleza.
Kama alivyosema Cheyo miaka mingi huko nyuma, ni muhimu watu wa karibu na migodi wakae kidhahabu dhahabu, watu wenye gesi wakae kama matajiri wa gesi.
Kila resource itawaliwe na walio hapo si serikali kuu, serikali kuu itoe ushauri an ipate commission in %age.
Kama watu wa kilimanjaro wanavyoupenda mlima, wanajua unachowapa, je watu wa mara wanapenda migodi yao?
Hivi kuna mtu anafuatilia viwanda vilivyopo katika makazi ya watu, je inashindikana kuhamisha watu au viwanda? basi tuna tatizo kubwa sana.
Nawatakia wizara ya viwanda mafanikio mema
 
Back
Top Bottom