Viwanda, plastiki na uchafuzi wa mazingira

Mlanga

JF-Expert Member
Jun 7, 2014
1,023
467
VIWANDA,PLASTIC NA MAZINGIRA.

Rais wetu JPM alipoingia madarakani alitangaza kuwa nchi yetu Tanzania itakuwa ni nchi ya viwanda .Viwanda vingewapatia wananchi ajira na vingesaidia kukuza uchumi wa Taifa letu.Viwanda vipo vya aina nyingi ila vimegawanywa katika makundi matatu

1. Viwanda vikubwa

2. Viwanda vya kati

3. Viwanda vidogo vidogo

Katika kundi la pili na la tatu, vifungashio (packaging material) ni vya muhimu sana katika kufikisha bidhaa kwa mlaji.

Sambamba na ujenzi na uendeshaji wa viwanda Watanzania tuna jukumu la kutunza Mazingira yetu.

Kutunza mazingira ni zaidi ya kufanya usafi katika miji na majiji yetu.

Kutunza mazingira ni pamoja na kuhifadhi vyanzo vya maji.Kutunza ardhi ,misitu na maliasili zingine.

Hivi karibuni kumekuwepo na viongozi wanaosisitiza sana usafi wa mazingira,nawapongeza.

Lakini wakati huohuo tunapoteza fursa (opportunities) za kufikia azma/lengo letu la kuwa nchi ya viwanda kwa mfano:
Kupiga marufuku mifuko ya plastiki ambayo inarudufika(recycable) badala ya Halmashauri za miji /majiji/wilaya kuanzisha viwanda vya kurudufu (recycle)mifuko hiyo na plastiki nyingine ambazo kwa sasa ni nyingi na zitaendelea kuwa nyingi kwani viwanda vingi sasa vinaachana na vifungashio asilia kama maboksi ya karatasi, chupa za kioo, makopo/madebe ya bati na alluminium na kutumia chupa ,mokopo, ndoo na katoni za plastiki.
 
Back
Top Bottom