Vivutio vya Tanzania kuwekwa kwenye jengo la Burj Khalifa ina maana gani kwa Taifa?

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Na Bwanku M Bwanku.

Dubai pale Falme za Kiarabu (UAE) kwa sasa ni moja ya maeneo maarufu yanayotembelewa na watu wengi sana kila siku na kila mwaka. Kwasasa Dubai kunasifika ulimwenguni kote kwa Utalii wa hoteli, kupumzika, mikutano mikubwa ya Kimataifa, maonyesho na mikutano mikubwa ya kibiashara, kumbi za starehe na mengine mengi ya kupendeza na kuvutia.

Watalii wengi wa mahoteli na kujivinjari kutoka Bara la Ulaya na Marekani wanaohitaji kupumzika na kurefresh mind kwenye mapumziko yao ya wikendi, ya kikazi, sikukuu, sherehe, mwisho wa mwaka na mengine, wengi wanakwenda Dubai kupumzika na kuhave fun hasa nyakati hizi ambazo Dubai kwenye ulimwengu mzima kunasifika kwa kuwa na kila aina ya Utalii wa hoteli, majengo, starehe na kila kitu.

Hiyo haitoshi, Matajiri, Wafanyabiashara na Wawekezaji wakubwa kutoka kila pembe ya Dunia huingia na kutoka kila siku Dubai kuhudhuria maonyesho na mikutano mikubwa ya kibiashara, kufanya biashara, kufanya vikao vikubwa vya Bodi na kushiriki kwenye majadiliano makubwa ya makampuni makubwa ya Ulimwengu. Kifupi, kwasasa Dunia ni moja ya Centre kubwa za Kibiashara, kitalii, kupumzika, kujivinjari na kimajadiliano.

Sasa, moja ya eneo lenye umaarufu mkubwa Dubai na linalopata kutembelewa na watu wengi sana kila siku kutoka kila pembe ya Dunia pale ni Dubai ni Tower maarufu kote Duniani inayoitwa Burj Khalifa.

Kwa Mujibu wa Researcher's Note ya Height of Buildings, Burj Khalifa ndiyo jengo refu zaidi Duniani likiwa na ghorofa 162 zenye urefu wa wastani wa miguu 2,717 sawa na Metres 828 likijumuisha jengo lote lenye maeneo ya biashara, ofisi, makazi na maeneo ya kutolea huduma mbalimbali.

Burj Khalifa lilifunguliwa rasmi mnamo tarehe 04 Januari mwaka 2010 na toka hapo limeendelea kushikilia rekodi ya kuwa jengo refu zaidi Duniani na linalotembelewa na watu wengi zaidi kila siku kutoka kila pembe ya Dunia. Kwa Mujibu wa Mamlaka za Falme za Kiarabu zilizopo hapo Dubai, watu zaidi ya Milioni 2 hufika Burj Khalifa kila siku kutembelea jengo hilo na kufanya biashara, utalii na kadhalika.

Burj Khalifa ni eneo na jengo la kimkakati kibiashara, kiuchumi, uwekezaji, utalii ambapo watu wengi hufika hapo kuona fursa mbalimbali, kufanya biashara na mengine mengi.

Sasa toka Mwishoni mwa mwezi Februari kuanzia Februari 28, 2022 mpaka sasa kwenye Jengo hilo refu kuliko yote Duniani kumekuwa kukishuhudiwa picha zenye nakshi ya Bendera ya Tanzania, vivutio vyake kama Mlima Kilimanjaro, picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, maneno ya kuwavuta Wawekezaji wote kuwekeza Tanzania hasa kwa namna ilivyojaliwa fursa kedekede na mengine mengi yakipamba jengo hilo zima la Burj Khalifa huku maelfu kwa maelfu ya watu kutoka kila pembe ya Dunia wanaotembelea eneo hilo lenye mchanganyiko na muingiliano wa watu wengi sana wakishuhudia maajabu hayo ya kuonyeshwa kila fursa ya Uwekezaji na Utalii uliopo nchini Tanzania kupitia picha za vivutio vya Utalii vya Tanzania na upekee wake vinavyoonyeshwa kila mara vikipamba jengo zima.

Tumeshuhudia Bendera ya Tanzania, baadae tukashuhudia picha ya Rais Samia Suluhu na maneno makubwa yanayong'aa ya kuwakaribisha watu wote kuja kuwekeza na kutalii Tanzania.

Baada ya hatua hii na picha za jengo hilo kunakshiwa na picha za Bendera ya Tanzania na vivutio vyake, kumezuka mjadala Watanzania wengi wakihoji, Je hatua hiyo ina maana gani? Tanzania inafaidika na nini na kama Taifa limetoa kiasi gani cha fedha kufanikisha jambo hilo kubwa hasa kwa eneo kama Burj Khalifa lenye hadhi ya Kidunia. Sasa tuendelee.

Kifupi, hii ina maana kubwa sana sana kwenye kuongeza thamani vivutio vyetu vya Utalii, kutangazia ulimwengu mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyopo Tanzania kwasasa hasa Tanzania ikiwa moja ya Mataifa 10 ya Afrika kulingana na ripoti ya Rand Merchant Bank (RMB) yenye mazingira mazuri zaidi ya Uwekezaji.

Narudia, hii ina maana kubwa sana kwenye Uchumi, uwekezaji na utalii wa nchi yetu. Dunia nzima sasa inatazama maajabu haya kwenye Jengo hilo refu zaidi Duniani huku Utalii wa Taifa letu ukizidi kutangazwa. Yote hii ni matunda ya ziara ya siku 3 ya Rais Samia Suluhu Hassan Dubai na heshima inayopewa Taifa letu baada ya ziara hiyo iliyokuwa na mafanikio makubwa sana ya Kiuchumi na Uwekezaji ikiwemo kusainiwa kwa Hati 36 za Makubaliano ya Ushirikiano kwenye sekta mbalimbali yenye thamani ya Shilingi Trilioni 17.1 ambayo itatoa ajira 204,575 kwa Watanzania.

Kwa siku ya 3 mfululizo jengo hilo refu zaidi Duniani la Burj Khalifa limeendelea kupambwa kwa nakshi ya bendera ya Tanzania na safari hii ikiwa na vivutio vya Tanzania na picha ya Rais Samia Suluhu Hassan inayosindikizwa na maneno yanayosomeka 'Tanzania Ready For Taking Off' ikiwa na maana ya kuiambia Dunia kwamba Tanzania iko tayali kwa kupokea uwekezaji na biashara hasa kwa namna ilivyobarikiwa kila aina ya fursa za uwekezaji na namna ilivyoboresha sera zake.

Jambo lingine la kufurahisha zaidi ni kwamba licha ya eneo hilo kuwa strategical sana na gharama kubwa kulipia ili upate kutangaziwa kitu chako hasa kwa kuzingatia ni eneo linalofuatiliwa na watu wengi sana Duniani lakini Serikali kupitia kwa Msemaji Mkuu wa Serikali Ndugu Gerson Msigwa imesema Serikali haijalipia pesa yoyote kuweka tangazo la Tanzania katika jengo hilo refu kuliko yote Duniani la Burj Khalifa.

Tangazo hilo limewekwa kwa lengo la kuitangaza Tanzania kutokana na uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi yetu na Umoja wa Falme za Kiarabu.
:
Utawala wa Dubai umeweka tangazo hilo kwa kutambua ziara ambayo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kaifanya Dubai iliyokuwa na mafanikio makubwa sana na imeahidi kuendelea kuitangaza Tanzania kupitia jengo hilo maarufu. Safari za Nje ya Nchi za Rais Samia na Diplomasia ya Uchumi aliyoipa uzito mkubwa kwasasa inazidi kuipaisha nchi Kimataifa zaidi. Hii ndiyo tafsiri ya nchi yetu na vivutio vyake kuonekana Burj Khalifa.

bwanku55@gmail.com.

Screenshot_20220302-114331.png
 
Attachments

  • 8a42849d47e94c8eb842d9cf85bfb146.mp4
    3.4 MB
  • gersonmsigwa~tv~CakqtFwjKLV~1.mp4
    462.5 KB
  • VID_49510605_221748_915.mp4
    5.3 MB

View attachment 2136412
hili ni tamko la serikali au la mtu binafsi anayeitwa Gerson Msigwa? Na kwa nini matamko ya kiserikali anatumia akaunti yake?.....aondolewe haraka huyu, atakwiza kumwingiza rais chaka kama walivyomdanganya kuwa magaidi wenzake mbowe walishafungwa jela.
 
Tatizo lao uongo wakitoto na kutuona nchi nzima viazi.

Burj Khalifa sio jengo la serikali so mamlaka ya Dubai hawana uwezo wakuagiza wamiliki waitangaze Tanzania bure.

Wamiliki wa Burj Khalifa ni Emaar Properties which is partly a ‘public listed company’ registered to trade in Dubai financial market.

Hivi kuna shareholders watakao kubali kutoa sandakalawe mwezi mzima, halafu mkurugenzi asitumbuliwe.

Maza anawashauri wa ovyo kweli hawajui ata dunia inazungukia upande gani. Uongo wakizamani kweli.

Wananchi wameamka usingizi, CCM original bado wanadhani tupo zama za giza werevu ni wao tu; hizi ni dharau.

Bila ya kubadili fikra za hawa wanaojiita CCM original we are doomed.
 
hili ni tamko la serikali au la mtu binafsi anayeitwa Gerson Msigwa? Na kwa nini matamko ya kiserikali anatumia akaunti yake?.....aondolewe haraka huyu, atakwiza kumwingiza rais chaka kama walivyomdanganya kuwa magaidi wenzake mbowe walishafungwa jela.
Na Ashatu Kijaji nae karudia kauli hiyo hiyo leo tena. Tangazo bure mwezi mzima awajamaa wanatuchukulia poa kweli.
 
Tatizo lao uongo wakitoto na kutuona nchi nzima viazi.

Burj Khalifa sio jengo la serikali so mamlaka ya Dubai hawana uwezo wakuagiza wamiliki watangaze Tanzania bure.

Wamiliki wa Burj Khalifa ni Emaar Properties which is partly a ‘public listed company’ registered to trade shares in Dubai financial market.

Hivi kuna shareholders watakao kubali kutoa sandakalawe mwezi mzima, halafu mkrugenzi asitumbuliwe.

Maza anawashauri wa ovyo kweli hawajui ata dunia inazungukia upande gani. Uongo wakizamani kweli.

Wananchi wameamka usingizi, CCM original bado wanadhani tupo zama za giza werevu ni wao tu; hizi ni dharau.

Bila ya kubadili fikra za hawa wanaojiita CCM original we are doomed.
Ujengewe sanamu kubwa sana na picha zako zibandikwe katika mabasi yaote yaendayo mikoan na nchi jiran.
 
Back
Top Bottom