Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Kasi ya upanuzi wa Bagamoyo Road ni nzuri. Nimepita wiki hii nikielekea katikati ya jiji, naona ujenzi unaendelea. Ukimalizika upanuzi wa barabara hii kuanzia mwenge mpaka morocco, ipo haja ya kuweka vivuko vya waenda kwa miguu, ambavyo vitajengwa juu ya barabara, kama kile kivuko cha Manzese. Hii itapunguza kama sio kuondoa kabisa ajali, kwa maana ya waenda kwa miguu kugongwa na magari.
Ni hatari sana kwa raia wanaojaribu kuvuka barabara ya njia nne za magari, njia mbili zinakwenda mjini, njia mbili zinaelekea Tegeta. Wizara ya miundo mbinu na ujenzi, kazi kwenu, huu ushauri ni wa bure kabisa.