Vive la différence! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vive la différence!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Mar 30, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Vive la différence!


  Kuna sentensi moja ambayo wanandoa wengi hupenda kuitumia ambayo ina makosa makubwa kupindukia nayo husema;

  “Kama mume/mke wangu angebadilika na kuwa kama ninavyotaka mimi basi ndoa yetu ingekuwa nzuri sana na ya kuridhisha”

  Ukweli ni kwamba kitu kama hicho hakipo na haiwezekani na ikiwezekana itakuwa kituko.


  WHY?

  Kwa sababu wewe ni mwanamke na mume wako kuwa kama wewe unavyotaka maana yake unataka awe mwanamke, afanye mambo kama mwanamke hapo nyumbani. Swali kwa nini uliolewa na mwanaume?


  Kama wewe ni mwanaume ukitaka mke wako awe kama wewe unavyotaka, maana yake unataka awe mwanaume na afanye mambo kama mwanaume kitu ambacho kitafanya nyumba yako iwe na wanaume wawili, guess what? Vita ya tatu ya dunia itatokea.


  Mungu alituumba mwanaume na mwanamke kuwa tofauti na hizi tofauti ndizo zinatufanya tuwe mwanaume na mwanamke hivyo badala ya kulazimisha kila kitu kiwe kama wewe unavyotaka badala yake zikubali na kuzisherehekea, vive la différence!


  Kuna tofauti ambazo zipo kati ya mke na mume na haziwezi kubadilika na haitawezekana na kujaribu kumbadilisha mke wako au mume wako ni kupoteza muda wako bure.

  Punguza matarajio ya mfurahie na kumpenda kama alivyo!


  Mwaka 1981, Dr Roger Sperry alipokea Tuzo (Prize) katika masuala ya Medicine/Physiology kutokana na ugunduzi wa namna ubongo unavyofanya kazi kwa watoto tumboni.


  Daktari aligundua kwamba katika mimba ya watoto wa kiume kuna kuwa na chemical reaction katika umri wa wiki ya 16 hadi 26 tofauti na watoto wa kike.

  Hiki kitendo hudhoofisha utendaji wa ubongo wa mtoto wa kiume sehemu ya kulia ambayo huhusika na utunzaji, uleaji, uuguzi au uuguzaji (caring) na matokeo yake upande wa kushoto kunakohusika na mantiki (logic) hutumika zaidi ya mtoto wa kiume hadi akiwa mtu mzima.


  JE, HII INA MAANA GANI?

  Hii ina maana ubongo wa mwanaume na mwanamke ni tofauti kwa maana kwamba mwanamke hutumia sehemu ya kulia ya ubongo unayohusika na uleaji, uuguzi, kumbukumbu nk wakati mwanaume hutumia ubongo sehemu ya kushoto ambayo huhusika na mantiki (logic).

  Hii ina maana pia mwanaume huzaliwa na udhaifu wa ubongo upande wa kulia


  JE, HII INA MAANA GANI KATIKA NDOA

  Suala la mwanamke kutumia right brain na mwanaume kutumia left brain huathiri kila eneo la ndoa na husababisha tofauti kubwa mno kati ya mke na mume.

  Bila kufahamu hizo tofauti na kuzikubali ndoa inaweza kujikuta inaishi kwenye vita kuu ya tatu ya dunia.


  Mr, inawezekana Mrs. akikwambia hupo sensitive au rejecting inawezekana tatizo ni ubongo wako namna upo wired ndiyo maana wakati mwingine hakuna kuelewana ndani ya ndoa.


  MIFANO

  Mke anaweza kuongea na simu kwa dakika 20 na bado anaweza kuanza kumsimulia mume details zote za ile simu kile alikuwa anaongea hata kama mume hahitaji kujua.

  Pia mwanaume anaweza kuongea na simu kwa dakika 20 na mke akiuliza nini alikuwa anaongea, mume atajibu neno moja tu na imetoka!


  Mke akienda kwenye sherehe na anaporudi atamsimulia mume kila kitu kimetoke na kila mtu aliyekuwepo kwa mume wake hata bila kuulizwa, na mwanaume akienda kwenye sherehe anaporudi mke akimuuliza sherehe Ilikuwaje atamjibu neno moja tu ‘ilikuwa safi” imetoka hiyo na mke anabaki kushangaza tu.


  Kama huamini kwamba mwanamke ana memory tofauti na mwanaume basi muulize mume mke wako honeymoon ilikuwa wapi na mlifanya kitu gani na kama kuna watu anawakumbuka aliowaona kwenye honeymoon, hata kama ni miaka 5 iliyopita bado anakumbuka hata nguo mlizovaa rangi zake nk.


  Mwanamke anatakiwa kufahamu kwamba, mwanaume kusahau au kutokuwa sensitive katika issue mbalimbali zinazowahusu (kama vile kusahau kukwambia kuhusu msiba unaowahusu) si kuonesha hajali bali wakati mwingine ni ubongo wake unafanya kazi tofauti na mwanamke.

  (this has a scientific facts)

  Si mwanaume kuwa logic au mwanamke kuwa emotional ndiko hujengwa ndoa bali ni kuishi kwa kutii neno la Mungu ambalo linasema mke na mume kuishi kwa hekima ya kimungu

  frm
  lazarus mbilinyi
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Mar 30, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  somo zuri mama!
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Aika mbe kanyi!!!
   
 4. P

  Preacher JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2010
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Somo zuri - pia hata mbavu za mwanamke na mwanamume ni tofauti -
  hata hivyo kuna wanaume wengine ni talkative sana - michapo - hata kuelezea mfano sherehe nzima iliiwaje - je hawa tuseme scientifically wako upande wa "mwanamke zaidi au"?? just asking.
   
 5. N

  Ntugwa Mbonyi Member

  #5
  Mar 30, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  upo juu
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Tofauti kati yetu (hata ndani ya jinsi) ndo inayofanya maisha yawe interesting. I can't imagine how boring life can be if you have the same interests, looks the same etc. Asante Mama Mia kwa kutushirikisha! Lakini huyu Lazarus Mbilinyi ni nani? pastor wako au?

  Nakuimbia ule wimbo wa Mamma Mia....kimoyomoyo
   
 7. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Lakini ubaya elimu juu ya huu utofauti haiwafikii wengi; Hii ingeokoa relationships nyingi sana
   
 8. M

  Mchili JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ahsante Mama Mia, hii ina ukweli. Kuna mambo mwanaume hana time nayo lakini unakuta wife anamind ile mbaya.
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  men were wired differently
   
Loading...