Viva Tanzania, Viva Afande SACP Susan Kaganda, Rais Samia ni Msikivu

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,483
54,853
Salaam Wakuu

Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) Susan Kaganda alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni kabla ya kupelekwa kuwa Mkuu wa Kitengo cha Mafao cha Jeshi la Polisi.

20210831_115935.jpg
Anapigiwa Chapuo kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP).

Nashauri Kaganda aongezewe Ulinzi mapema hadi ulinzi wa nini anakula sababu nyota njema huonekana asubuhi.

Screenshot_20210831-120031.png

Kaganda ni Matunda ya Watanzania, hivyo ni heshima kubwa kwa taifa kuongozwa naye. Hakika nchi itapona na mgawanyiko utaisha.

20210831_115943.jpg

Nimekuwa nikimfuatilia kwa muda sasa. Nimeona ni mtu anayefanya kazi zake kwa Weledi, mnyenyekevu, anajua mipaka ya Askari, anaheshimu Wakubwa zake wa kazi, ni msikivu. Pia ni Mcha Mungu. Hana Matabaka. Anachangia misiba na harusi. Ni mwingi wa Huruma(Mzazi).

Anajua kwamba cheo ni dhamana.

20210831_104830.jpg
Nimejitahidi kutafuta CV yake bila mafanikio, lakini nimepata video zake ambazo kila mtu akisikiliza na kuangalia, atajua ni Mtu wa aina gani.

Wapo wenye CV nene lakini wameisaliti Nchi. Hivyo CV si chochote.

Tanzania tunao watu wengi wanaofaa kuwa IGP lakini na Kaganda ni Mmoja wapo, hata kama akiachwa sio kwamba hafai. Nitazidi kumheshimu.

Kama tunataka Mungu aibariki Tanzania, kama tunataka mabadiliko ndani ya Jeshi la Polisi, dawa sio kutukana, kukejeli wala kudharau Viongozi wa Kitaifa. Toa Ushauri au Pendekeza nini kifanyike. Mimi siwaungi Mkono wanaotumia lugha chafu dhidi ya IGP wetu Sirro anayemaliza muda wake kwa sababu mimi ndo nilipendekeza Sirro awe IGP na amefanya Mambo mengi makubwa. Ili Nchi iwe na amani, Simon Sirro awe Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP) , ana hofu ya Mungu

Silkiliza hekima zake kwenye hizi Video mbili kabla ya kuandika chochote. Tumhukumu kwa haki.
 
Nyie ndio mnamuharibia dada wa watu. Nyambaff zenu
Mkuu, unao uhuru wa kuandika chochote. Lakini ulichokiandika hapa hakisaidii nchi wala hakikusaidii. Hukuwa na sababu ya kitukana. Bali sema dukuduku lako utaeleweka. Siku zote nitaendelea kukufunza hadi uache matusi. Unaheshima sana.
 
Video imekufanya umuone anafaa, lakini kiundani humjui. Wanaomjua wanabaki kushangaa.
Tatizo kubwa la sasa mitandaoni ni kusifia na kutukana wasiowajua.
Mimi ninakuambia huyo mama hafai, na hawezi kuwa IGP.
Wala ubishi sihitaji
Amekaa Kinondoni muda mrefu. Sijasema simfahamu bali nimesema sijapata CV yake. Kama nikiipata au kama unayo ibandike hapa. Pia useme kwanini unasema hafai. Angekuwa hafai asingekuwa anapandishwa Vyeo.
 
Mbona mimi nikitaka kufungua attachment kama hiyo haifunguki badala yake inakuja orodha ya forums!? Maxence Melo kunanini? Kuna siku nime unstall na ku install lkn yale yale. Nifanyeje?
Mkuu, kuna thread alipost kipindi fulani. Jaribu kufuata hizi hatua, nadhani inaweza tatua changamoto zako.

 
44 Reactions
Reply
Back
Top Bottom